Utangulizi

Prof. Sospeter Muhongo

[metaslider id=227]

line2

HABARI MPYA

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – KILIMO CHA ZAO LA MIHOGO

TAARIFA – Meneja wa Mradi wa Mihogo kutoka China ameomba kufika Jimboni mwetu tarehe 06.08.2018 angali yuko UGANDA kikazi.
Samahani kwa usumbufu kwa wale waliojitayarisha kuonana nae tarehe 10.07.2018.
KIKAO CHETU cha tarehe 10.07.2018, Saa 4 Asubuhi, Ofisini kwa DC, Musoma KITAKUWEPO – KUJADILI NA KUCHANGIA UPATIKANAJI wa Mbegu za Mtama, Mihogo na Mahindi.

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – RATIBA

(1) 10.07.2018: MBEGU
WADAU wote wanakaribishwa KUCHANGIA upatikanaji wa MBEGU za Kilimo cha Vuli.
(2)  12 &13.07.2018: CCM
Vikao vya Chama vya Wilaya
(3) 14.07.2018: SHULE
Saa 4-6: Mwikoko S/M, Kijiji cha Chitare (MICHANGO)
Saa 9-11: Busambara Sec  Kijiji cha Mwiringo  (MICHANGO)
(4) 15.07.2018: SHULE
Saa 3-5: Nyegina B S/M, Kijiji cha Nyegina. Jiwe la Msingi (MICHANGO)

MAZAO MAPYA YA BIASHARA KWA WAKULIMA JIMBONI

Mbali ya PAMBA kuwa ZAO kuu la BIASHARA kwa muda mrefu, muda umewadia kupanua wigo wa mazao yetu ya biashara na kuanza kulima MAZAO MENGINE yenye MASOKO ya UHAKIKA ambayo ni:
(1) ALIZETI
(2) MIHOGO
(3) UFUTA
Kwa mfano Soko la CHINA liko tayari KUNUNUA MIHOGO MIKAVU kutoka TANZANIA kwa wingi wa takribani TANI 150,000… Jimbo letu nalo LIUZE MIHOGO MIKAVU NCHINI CHINA.
Tarehe 10 Julai 2018, Mbunge wa Jimbo atafanya KIKAO na DC, DED, MADIWANI na WATAALAMU WA KILIMO WA HALMASHAURI na WILAYA kujadili na kujitayarisha kwa UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO CHA MVUA ZA VULI (Septemba-Disemba 2018) za MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA Jimboni mwetu.
Ofisi ya Mbunge

NANE NANE 2018 – JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wanavijiji wa KILA KATA wanashauriwa kusherehekea Sikukuu ya Nane Nane kwa kushiriki MASHINDANO ya NGOMA ZA UTAMADUNI na KWAYA.
Kila KATA itatoa Kikundi Kimoja cha NGOMA na Kikundi Kimoja cha KWAYA kushiriki kwenye mashindano hayo.
Mashindano haya tulishayafanya na zawadi zikatolewa kwa WASHINDI WATATU wa kwanza.
MAHALI: Kijiji cha Suguti
TAREHE: 8.8.2018
MATAYARISHO: Wasaidizi wa Mbunge wataorodhesha VIKUNDI vitakavyoshiriki mashindano.
TAREHE YA MWISHO YA KUJIORODHESHA: Jumanne, 31.7.2018
TUENDELEE KUDUMISHA UTAMADUNI WETU

line2

Vipaumbele vya Mbunge
Elimu Afya Kilimo Ajira Maji
Elimu kwa wote na kuinua ufaulu Huduma za afya zinazo kidhi uhitaji Kilimo endelevu na chenye tija Ajira zaidi zitokanazo na maliasili za jimbo Maji safi na salama kwa kila kaya

line2

Jimbo la Musoma vijijini ni jimbo jipya lililoundwa rasmi mwaka 2015. Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ndiye Mbunge wa kwanza wa jimbo hili. Katika jitihada za kuliletea jimbo hili maendeleo, tovuti hii inawezesha mawasiliano ya haraka kati ya Mheshimiwa Mbunge, uongozi wa Jimbo na wananchi kwa ujumla.

(Taarifa Kamili Kuhusu Jimbo)

line2

Baadhi ya shughuli za mandeleo zilizofanyika jimboni kupitia ofisi ya Mbunge
Tangu kuchaguliwa kwa Mh. Prof. Muhongo kuwa Mbunge wa jimbo hili, ofisi ya Mbunge kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya nchi wameendelea kuweka bidii katika kuleta maendeleo kwa wakazi wa jimbo. Baadhi ya shughuli zilizofanyika katika nyanja za Elimu, Afya, Maji na kilimo zinaelezewa zaidi katika ukurasa wa Miradi ya Maendeleo na Matukio.