UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA NYAMBONO KWA NJIA YA KUJITOLEA WAFIKIA HATUA NZURI

Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyambono Unavyoendelea Kupiga Hatua

Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge.
Wananchi wa Kata ya Nyambono wameendelea na UJENZI wa Kituo cha Afya baada ya kuwa wamesimama kwa muda kutokana na kukusanya nguvu (MICHANGO) toka kwa WANANCHI na WADAU wengine wapenda MAENDELEO kutoka ndani na nje ya Kata ya Nyambono.
Wananchi wanaendelea na UJENZI huo, ambao Mbunge wa Jimbo la MUSOMA VIJIJINI aliweka Jiwe la Msingi Desemba 25, 2017 na baadaye akachangia SARUJI MIFUKO
MIA MOJA (100) iliyotumika kufyatua matofari kwa ajili ya UJENZI wa Jengo la OPD.
Aidha, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyambono, Ndugu Ernest Maregesi ametoa shukrani zake kwa niaba ya Wananchi na Viongozi wa Kata ya Nyambono kwa kuwepo mpangokazi  wa uhakika wa ujenzi wa Kituo hicho. Hatua za awali za ujenzi huo zinatia matumaini makubwa.
Kiongozi huyo wa Kijiji cha Nyambono AMETOA SHUKRANI NYINGI SANA  kwa WAZAWA wa Kata ya Nyambono walio nje ya Kata hiyo kwa MICHANGO yao wanayoendelea kutoa hadi hapo walipofikia, na vilevile kwa Mhe Prof Muhongo, kwa kazi kubwa za MAENDELEO anazozitekeleza KWA VITENDO Jimboni humo.
Viongozi wa Kata ya Nyambono wanaendelea kutoa hamasa kwa Wakazi wote wa Vijiji vya Nyambono na Saragana kuwiwa na shughuli hiyo, na kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha wanakamilisha majengo hayo mapema, na kuanza kupata huduma katika Kituo hicho cha Afya.
WANA-KATA YA NYAMBONO WANASEMA – “Nyambono iko wazi, Ujenzi wa Kituo chetu cha Afya bado unaendelea, tunaendelea kuwakaribisha wote mnaoguswa na ujenzi huu kuungana nasi kwa hali na mali.”
MRADI WA MAJI BULINGA – BUSUNGU WAANZA KUTEKELEZWA

Hatua ya uunganishaji wa mabomba yatakayotumika katika mradi wa Maji wa Busungu – Bulinga

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
MRADI wa Maji wa Bulinga – Busungu katika kata ya Bulinga umeanza kutekelezwa ili kuondoa changamoto ya uhaba wa Maji katani humo na vijiji vya Jilani
Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa kata ya Bulinga wamesema, sasa wameshuhudia ahadi za Mbunge wao Prof Muhongo ambazo amekuwa akiwataka wananchi wake kuwa wavumilivu katika kusubiria miradi ya serikali
 Wamesema ukamilikaji wa Mradi huo utaondoa tatizo la uhaba wa maji na kuongeza muda wa kushiriki shughuli nyingine za uzalishaji tofauti na kipindi cha nyuma
Wananchi walisema kuwa, wamekuwa wakilazimika kutumia muda mrefu kutafuta maji katika visima vya asili ambavyo vimekua vikikauka haraka wakati wa kiangazi
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bulinga Ndg Maira Masaule kwa niaba ya wananchi wa Bulinga ameipongeza Serikali kuwapatia Mradi wa Maji unaojengwa na kisema, ” Mradi huu utasaidia kuondoa adha ya ukosefu wa maji katika kata ya Bulinga na Vijiji vya Jilani” Alisema Masaule
Kwa upande wake kaimu Mtendaji Kata  ya Bulinga ndg Obadia Sendi  amesema kuwa, Vijiji Vitakavyonufaika ni Busungu, Bulinga, Bujaga, Bukima na Kwikerege
Ameongezea kuwa, Mkataba huu unatekelezwa na kampuni ya ujenzi ya  EDM NETWORK LTD JV FAU CONSTUCTION LTD, Mkataba ambao ni wa mwaka mmoja na unagharimu kiasi cha Tsh 1,022,531,876/=
Miundombinu itakayotekelezwa katika zoezi hili ni pamoja na ujenzi wa Mantenk na ofisi, vituo vya kuchotea maji (DP’s) 18, Viosk vya kuuzia maji 2 kata ya Bukima,  Birika za kunyweshea mifugo ( Busungu na Kwikerege) na ujenzi wa Bomba kuu na Mabomba ya kusambaza Maji
Wananchi na Viongozi  wa Vijiji na kata zinazonufaika na Mradi huu wamehaidi kulinda Miradi ya Serikari inayoletwa Jimboni kwa faida ya Jamii
UJENZI WA SEKONDARI YA KATA YA BUSAMBARA WAFIKIA HATUA NZURI

Ujenzi wa Madarasa ya Shule ya Sekondari Busambara Ukiendelea

Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge
Oktoba 08, 2018
UJENZI wa Sekondari Busambara umefikia hatua nzuri baada ya WANANCHI wa Kata hiyo kuendelea kwa kasi kubwa ambapo hadi hivi leo, WANANCHI hao kwa pamoja wamekamilisha MABOMA mawili ya MADARASA na OFISI moja.
Kata ya Busambara inavyo vijiji vitatu – Maneke, Kwikuba na Mwiringo.
Wananchi wa Vijiji vya Kwikuba na Maneke hivi sasa wapo katika hatua ya kufunga renta wakati Kijiji cha Mwiringo wamekifikia hatua ya madirisha.
Ujenzi wa Sekondari hiyo unaojumuisha na kushirikisha WANANCHI wote wa Kata ya Busambara. Ujenzi wa Sekondari hiyo ya Kata ni wa KUJITOLEA KWA KUCHANGIA FEDHA na NGUVU ZA WANANCHI. Mhe. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo anashirikiana na wanavijiji wa vijiji hivyo vitatu kwa kuwachangia vifaa vya ujenzi.
Hadi hatua ulipofikia ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo ameishachangia SARUJI MIFUKO 150, yaani Mifuko 50 kwa kila Kijiji. Vijiji hivi vitatu vimewekeana makubaliano ya kufanikisha ujenzi huo kwa kugawana vyumba vya madarasa na ofisi za kujengwa hadi Sekondari kukamilika.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa ngazi ya Kata na Vijiji kwa ujumla wao wanatoa shukrani nyingi kwa Mbunge wao kwa jitihada za maendeleo anazozifanya kwa wananchi wa Jimbo lake (k.m. kuboresha elimu, huduma za afya na kilimo cha kisasa). Mbunge ataendelea kuchangia Ujenzi wa Sekondari hiyo.
Wananchi wa Kata ya Busambara na Vijiji vyake Vitatu wanaendelea kuwakaribisha WADAU WENGINE WA MAENDELEO wajitokeze ili kufanikisha ujenzi huo.
KATA YA BUSAMBARA HAINA SEKONDARI KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI YA KATA YA BUSAMBARA
WANANCHI KUENDELEA KUJITOLEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO YA KATA NA VIJIJI VYAO

Wananchi wa Kijiji cha Bwai Kwitururu wakiwa kwenye Mkutano wa kuamua kuanza Ujenzi wa Zahanati

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge
Tarehe 07/10/2018
WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wamesema wataendelea KUJITOLEA kwa hali na mali katika kutekeleza MIRADI mbalimbali ya MAENDELEO ndani ya Kata na Vijiji vyao ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya, Ujenzi wa Shule mpya za Sekondari na Msingi, kuongeza Vyumba vya MADARASA, MAKTABA na MAABARA ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika Sekta za Afya na Elimu Jimboni mwao.
Hayo yamebainika kupitia ZIARA ZA WASAIDIZI WA MBUNGE  (Ofisi ya Mbunge) za Kuhamasisha shughuli za Maendeleo iliyofanyika mapema wiki hii katika Vijiji mbalimbali vya Jimbo la Musoma Vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Ziara hizo, WANANCHI walisema kuwa, KUJITOLEA KWAO ni ishara tosha ya kuungana na Serikali, Wadau wa Maendeleo na Mbunge wao Prof Muhongo kuharakisha na kuboresha huduma za kijamii Jimboni mwao.
Wananchi wa Kata ya  Ifulifu, Kijiji cha Kabegi wao wameanza kusomba mawe, mchanga, n.k. kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya  Chekechea ili kupunguza mwendo mkubwa wa watoto wadogo ambao kwa sasa wanaenda Shule za Vijiji jirani.
Wananchi wa Kijiji cha Bwai Kwitururu, baada ya kukaa kipindi kirefu bila Zahanati, kwa kauli moja waliazimia KUWEKA TOFAUTI ZAO PEMBENI na kuanza utekelezaji wa MRADI wa Ujenzi wa Zahanati kwa VITENDO. Hatua hiyo nzuri ilipelekea Diwani wa Kata ya Kiriba Mhe Msendo kuahidi kuungana na Wananchi wa Bwai Kwitururu kwa kutoa Saruji Mifuko 50  kwa ajili ya kuanza ujenzi huo utakaofanyika kwa wakati muafaka katika eneo la Chanyauru. Wakianza ujenzi huo Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo atatembelea eneo la ujenzi na kutoa mchango wake kama afanyavyo kwenye MIRADI YA UJENZI Jimboni mwao.
Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji cha Kamguruki, Kata ya Nyakatende, waliishukuru Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Muhongo kupitia Mkutano uliofanyika Kijijini hapo na kusema hamasa hiyo imewafanya kuongeza kasi katika maamuzi ya Ujenzi wa Zahanati na kukamilisha Ujenzi wa Shule mpya katika Kitongoji cha Kiunda ili kupunguza umbali hadi ilipo Shule ya Msingi Kamguruki. Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo amekubali kuchangia UJENZI HUO.
Leo Jumapili, 7.10.2018 Sekondari ya Bwasi, Kata ya Bwasi imepiga HARAMBEE YA UJENZI WA BWENI KUBWA LA WASICHANA. Mbunge wa Jimbo amechangia. Taarifa ya Tukio hilo inatayarishwa. Wiki ijayo Mbunge atafanya ZIARA ZA KUHAMASISHA UJENZI wa Madarasa na Zahanati kwenye Kata za Rusoli, Bukima na Etaro.
Katika Ziara zote hizo, pamoja na mambo mengine, Ofisi ya Mbunge ILIENDELEA KUWASHAWISHI Wananchi Vijijini kuendelea kujitolea kwa hali na mali, na kukaribisha wazawa na wadau mbalimbali wa maendeleo waishio ndani na nje ya Jimbo la Musoma Vijijini kuungana na ndugu zao katika kuchangia shughuli za maendeleo vijijini mwao ikiwa ni njia muhimu ya kuunga  mkono SERIKALI, Madiwani na Mbunge wao na Wadau wengine wa maendeleo katika kuharakisha MAENDELEO ya Jimbo la Musoma Vijijini.
WANANCHI WA KJIJI CHA MUSANJA WAJITOLEA KUJENGA DARAJA KURAHISISHA MAWASILIANO KATI YA JAMII NA SHULE YA MSINGI MUSANJA

mwanzo wa Ujenzi wa Daraja Kijijini Musanja

Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge
18 – 09 – 2018
WANANCHI wa Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja WAMEJITOLEA kwa hali na mali KUJENGA DARAJA linalounganisha Vitongoji vya Kaharaga na Kukema (ilipo S/M Musanja) ili kurahisisha mawasiliano kati ya Shule na Jamii inayozunguka Shule hiyo.
Wanafunzi wanapata shida sana kufika Shuleni wakati wa Mvua.  Wakati mwingine UBOVU wa njia hiyo umekuwa ukisababisha WANAFUNZI kushindwa kabisa kuhudhuria masomo hasa wanaposhindwa kuvuka eneo hilo wakati wa mvua.
Ujezi ulianza  mapema wiki iliyopita. MICHANGO YA KUJITOLEA ikiwemo NGUVU za WANANCHI  wenyewe ndiyo inayoendesha UJENZI wa DARAJA HILI.
WAZALIWA wa Kijiji cha Musanja,  waishio nje ya Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA KUTOA MICHANGO YAO wakishirikiana na wakazi wa Kijijini hapo.
Awali, akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Musanja, Ndugu Emmanuel Eswaga alisema, “Hadi kukamilika kwa ujenzi huo, Jumla ya Tsh Milioni 15.9 zinahitajika ikiwa ni gharama za Mchanga, Mawe, Saruji, Nondo, Kokoto na Malipo ya Fundi.”
Ameongezea kuwa katika gharama hizo WANANCHI wa Kijiji cha Musanja wamebeba jukumu la kusomba mchanga, mawe, maji na kokoto.
Aidha, Afisa Mtendaji huyo akieleza hatua walizokwishafikia katika Mradi huo, alisema kuwa tayari wameanza kupokea michango kutoka kwa WADAU/WAZAWA wa Kijiji hicho ambao ni pamoja na Ndugu Vedastus Mlegi Tekere ambaye amechangia SARUJI MIFUKO 100 na NONDO  ROLA 4 huku Diwani wa Kata hiyo, Mhe Elias M. Ndaro akichangia TRIPU 1 ya MCHANGA na MAWE TRIPU 2.
Sambamba na juhudi hizo, bado kuna UPUNGUFU WA SARUJI MIFUKO 65, na PESA YA FUNDI Tsh. Milioni 2.6 ili kukamilisha ujenzi huo KABLA ya MSIMU wa MVUA kuanza.
Uongozi wa Kijiji cha Musanja unaomba WADAU wengine kuwasaidia WANANCHI wa Kijiji cha Musanja KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA HILO mapema iwezekanavyo.
Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ataenda KUTEMBELEA MRADI HUO na KUTOA MCHANGO WAKE ndani ya wiki 2 zijazo.
Kwa Mawasiliano zaidi:
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji
Ndugu Denis J. M. Kuyenga
Simu: +255759 922760
VEO Musanja
Emmanuel Eswaga
Simu: +255692 972571
Wana-Musanja wanasema:
MUSANJA ni yetu na Musoma Vijijini ni yetu sote. KARIBUNI TUCHANGIE.

 

TAARAIFA YA MAENDELEO NA HALI YA KILIMO KWA MSIMU WA 2017/2018 NA MATARAJIO YA WAKULIMA KATIKA ZAO LA MHOGO NA MTAMA KWA MSIMU WA KILIMO WA 2018/2019 KWA KILA KIJIJI – MUSOMA VIJIJINI

S/N KIJIJI MIHOGO MTAMA ZANA ZA KULIMIA JUMLA

KAYA

KATA
AWALI TARAJIA AWALI TARAJIA TREKTA POWER TILLER PLAU
NZIMA MBOVU NZIMA MBOVU NZIMA MBOVU
01 BUKUMI 221 411 345 457 0 0 0 1 28 8 722 BUKUMI
02 BUIRA 291 394 44 142 0 0 0 0 2 0 480
03 BURAGA 584 764 721 984 0 0 0 0 4 0 575
04 BUSEKERA 614 724 52 572 0 0 0 0 11 2 718
JUMLA 1710 2293 1162 2155 0 0 0 1 45 10 2495
05 MAKOJO 418 418 418 418 1 0 1 0 0 0 445 MAKOJO
06 CHIMATI 499 570 414 470 0 0 0 0 2 0 457
07 CHITARE 492 492 492 492 0 0 0 0 3 0 683
JUMLA 1409 1480 1324 1380 1 0 1 0 5 0 1585
08 BWASI 50 55 15 20 0 0 0 0 0 0 614 BWASI
09 BUGUNDA 125 130 17 20 0 0 0 0 0 0 682
10 KOME 125 127 18 20 0 0 0 0 0 0 825
JUMLA 300 312 50 60 0 0 0 0 0 0 2121
11 BULINGA 417 419 116 223 0 0 0 0 0 0 445 BULINGA
12 BUJAGA 306 538 79 109 0 0 0 0 0 0 378
13 BUSUNGU 435 502 69 98 0 0 0 0 0 0 347
JUMLA 1158 1459 264 430 0 0 0 0 0 0 1170
14 RUSOLI 220 250 355 360 0 0 0 0 16 0 630 RUSOLI

 

15 BUANGA 180 350 140 204 0 0 0 0 18 0 512
16 KWIKEREGE 185 190 15 18 0 0 0 0 2 0 204
JUMLA 585 790 510 582 0 0 0 0 36 0 1346
17 BUKIMA 280 800 175 600 0 0 1 0 2 0 930 BUKIMA
18 BUTATA 370 400 150 300 0 0 0 0 1 0 537
19 KASTAM 110 412 125 150 0 0 0 0 3 0 516
JUMLA 760 1612 450 1050 0 0 1 0 6 0 1983
20 MURANGI 300 600 201 450 0 0 0 0 42 0 1009 MURANGI
21 LYASEMBE 126 340 109 215 0 0 0 0 18 2 632
JUMLA 426 940 310 665 0 0 0 0 32 2 1641
22 MUSANJJA 429 549 352 516 0 0 0 0 79 32 646 MUSANJA
23 MABUI 132 223 74 137 0 0 0 0 97 15 433
24 NYABAENGERE 285 349 218 337 0 0 0 0 136 22 476
JUMLA 846 1121 644 990 0 0 0 0 312 69 1555
25 KABONI 102 210 27 180 0 0 0 0 89 0 260 NYAMRANDIRIRA
26 KASOMA 245 555 180 560 0 0 0 0 36 2 620
27 CHUMWI 64 606 169 509 0 0 0 0 36 1 620
28 SEKA 182 341 120 608 0 0 0 0 104 5 660
29 MIKUYU 214 248 212 250 0 0 0 0 58 3 254
JUMLA 807 1960 708 2107 0 0 0 0 323 11 2414
30 SUGUTI 570 600 20 200 0 0 0 0 12 2 716 SUGUTI
31 KUSENYI 340 642 16 190 3 0 0 0 18 4 480
32 WANYERE 621 739 78 405 1 0 0 0 78 2 846
33 CHIRORWE 258 400 56 595 0 0 0 0 32 0 648
JUMLA 1789 2381 170 1390 4 0 0 0 140 8 2690
34 BUGWEMA 38 60 220 311 3 1 1 0 486 2 402 BUGWEMA
5 MASINONO 18 104 52 189 0 1 0 0 312 1 231
36 MUHOJI 285 349 218 337 0 0 0 0 298 2 362
37 KINYANG’ERERE 20 40 100 150 3 0 0 0 248 0 306
JUMLA 361 553 590 987 3 2 1 0 1344 5 1301
38 BUGOJI 112 182 99 175 0 0 0 0 63 5 185 BUGOJI
39 KABURABURA 98 118 43 120 0 0 0 0 32 2 125
40 KANDEREMA 120 347 78 314 0 0 0 0 116 6 407
JUMLA 330 647 220 609 0 0 0 0 211 13 717
41 NYAMBONO 850 850 30 100 1 0 0 0 14 0 850 NYAMBONO
42 SARAGANA 900 930 30 100 2 0 0 0 35 0 940
JUMLA 1750 1780 60 200 3 0 0 0 49 0 1790
43 MANEKE 450 500 30 120 1 0 1 0 38 0 829 BUSAMBARA
44 KWIKUBA 170 185 50 70 0 0 0 0 18 0 331
45 MWIRINGO 427 430 70 100 0 0 0 0 20 0 552
JUMLA 1047 1115 150 290 0 0 1 0 76 0 1712
46 KIRIBA 721 721 89 194 0 0 1 0 12 4 731 KIRIBA
47 B. KUMUSOMA 856 1654 28 213 1 0 0 0 10 0 1755
48 B. KWITURURU 746 896 6 123 0 0 0 0 23 0 916
JUMLA 2323 3271 123 530 1 0 1 0 45 4 3402
49 KWIBARA 623 872 23 308 1 0 0 0 40 0 1443 MUGANGO
50 NYANG’OMA 312 420 28 480 0 0 0 0 8 0 615
51 KURWAKI 320 320 50 300 0 0 0 0 26 0 355
JUMLA 1255 1612 101 1088 1 0 0 0 74 0 2413
52 TEGERUKA 459 513 149 500 0 0 0 0 21 0 578 TEGERUKA
53 MAYANI 443 450 301 396 0 0 0 0 20 4 670
54 KATARYO 103 224 607 624 0 0 0 0 48 13 1120
JUMLA 1005 1187 1057 1520 0 0 0 0 89 17 2368
55 KABEGI 12 386 96 428 0 0 0 0 10 0 504 IFULIFU
56 KIEMBA 48 420 84 341 0 0 1 0 12 0 547
57 NYASAUNGU 8 9 111 144 0 0 0 0 130 25 221
JUMLA 68 815 291 913 0 0 1 0 152 25 1272
58 NYAKATENDE 140 322 32 302 0 0 0 0 8 0 477 NYAKATENDE

 

 

59 KAMGURUKI 86 331 26 314 0 0 0 0 15 0 360
60 KIGERA ETUMA 354 618 227 379 1 0 1 0 99 18 1130
61 KAKISHERI 278 456 98 460 0 0 0 0 12 3 528
JUMLA 858 1727 383 1455 1 0 1 0 0 21 2495
62 NYEGINA 450 544 300 554 0 0 0 0 0 0 617 NYEGINA
63 MKIRIRA 509 581 298 511 0 0 0 0 0 0 554
64 KURUKEREGE 158 341 141 321 0 0 0 0 12 0 452
JUMLA 1117 1466 739 1386 0 0 0 0 12 0 1623  
65 ETARO 308 527 98 188 0 0 0 0 12 0 762 ETARO
66 BUSAMBA 251 436 181 286 1 0 0 0 14 3 500
67 MMAHARE 125 212 92 180 0 0 0 0 9 0 268
68 RUKUBA 117 140 0 0 0 0 0 0 0 0 600
JUMLA 801 1315 371 654 1 0 0 0 35 3 2130

 

MCHANGANUA KWA NGAZI YA KATA

S/N KATA MIHOGO MTAMA ZANA ZA KULIMIA JUMLA

YA

KAYA

AWALI TARAJIA AWALI TARAJIA TREKTA POWER TILLER PLAU
NZIMA MBOVU NZIMA MBOVU NZIMA MBOVU
01 BUKUMI 1710 2293 1162 2155 0 0 0 1 45 10 2495
02 MAKOJO 1409 1480 1324 1380 1 0 1 0 5 0 1585
03 BWASI 300 312 50 60 0 0 0 0 0 0 2121
04 BULINGA 1158 1459 264 430 0 0 0 0 0 0 1170
05 RUSOLI 585 790 510 582 0 0 0 0 36 0 1346
06 BUKIMA 760 1612 450 1050 0 0 1 0 6 0 1983
07 MURANGI 426 940 310 665 0 0 0 0 32 2 1641
08 MUSANJA 846 1121 644 990 0 0 0 0 312 69 846
09 NYAMURANDIRIRA 807 1960 708 2107 0 0 0 0 323 11 2414
10 SUGUTI 1789 2381 170 1390 4 0 0 0 140 8 2690
11 BUGWEMA 361 553 590 987 3 2 1 0 1344 5 1301
12 BUGOJI 330 647 220 609 0 0 0 0 211 13 717
13 NYAMBONO 1750 1780 60 200 3 0 0 0 49 0 1790
14 BUSAMBARA 1047 1115 150 290 0 0 1 0 76 0 1712
15 KIRIBA 2323 3271 123 530 1 0 1 0 45 4 3402
16 MUGANGO 1255 1612 101 1088 1 0 0 0 74 0 2413
17 TEGERUKA 1005 1187 1057 1520 0 0 0 0 89 17 2368
18 IFULIFU 68 815 291 913 0 0 1 0 152 25 1272
19 NYAKATENDE 858 1727 383 1455 1 0 1 0 0 21 2495
20 NYEGINA 1117 1466 739 1386 0 0 0 0 12 0 1623
21 ETARO 801 1315 371 654 1 0 0 0 35 3 2130
JUMLA KUU 20705 29836 9677 20441 15 2 7 1 2986 188 39514

 

 

 UJENZI WA ZAHANATI WAPAMBA MOTO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge
(1) KIJIJI CHA KURUKEREGE, KATA YA NYEGINA
Mhe Diwani Majira,  Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Wakazi wa Kijiji cha Kurukerege WAMEAMUA KUANZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO.
Ujenzi UNAANZA RASMI WIKI HII na Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO kwenye UCHANGIAJI na UPATIKANAJI wa Vifaa vya Ujenzi.
UNAKARIBISHWA kutoa MCHANGO wako moja kwa moja kwenda Kijijini kupitia kwenye Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Kurukerege.
(2) WANANCHI WA NYASAUNGU WAONGEZA KASI YA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO
Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu,  Katani Ifulifu wamepiga hatua nyingine ambapo sasa wameanza UJENZI wa BOMA la ZAHANATI ya Kijiji hicho. Hatua hiyo imefikiwa siku chache baada ya kukamilisha hatua ya kumwaga Jamvi.
Awali,  akitoa TAARIFA ya hatua iliyofikiwa na WANANCHI hao kwa Mwandishi wa habari hizi, Mtendaji wa Kata ya Ifulifu Ndg Fred Yona amesema kuwa, “ili kufanikisha hatua hiyo ya BOMA, wananchi wa Nyasaungu wamekubaliana KUCHANGIA kati ya Tsh 30,000/= na Tsh 40,000/= kwa KILA KAYA ambapo mchango huo unatofautiana kutegemea Idadi ya KAYA za kila KITONGOJI kwa kiwango walichokubaliana Wanakijiji hao.”
Aidha, Kaimu Mtendaji wa Kijiji hicho Ndg Patrice Jonas AMEWASHUKURU WANANCHI wote wa Kijiji cha Nyasaungu kwa KUWEKEZA NGUVU na MALI zao ili kufanikisha upatikanaji wa Huduma za Afya Kijijini humo.
Kwa upande wao, WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu wamewapongeza WADAU mbalimbali  wa MAENDELEO akiwemo Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo kwa mchango wake wa SARUJI MIFUKO 100 aliyoitoa katika hatua ya awali ya umwagaji jamvi la Zahanati hiyo.
Pongezi nyingine zinawaendea Viongozi wa Halmashauri ya Musoma Vijijini, hasa Mwenyekiti Mhe Diwani Charles Magoma kwa ushirikiano wao wanaoendelea kuonesha katika usimamiaji na ufuatiliaji wa Mradi huo.
Picha hapo chini zinaonyesha  zoezi la ujenzi wa BOMA la Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu.
TUSHIRIKIANE NA SERIKALI YETU KWA KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO VIJIJINI MWETU – TUSISUBIRI TUNAJICHELEWESHA!

MRADI WA MAZINGIRA – KITALU CHA MICHE YA MITI KIMEPATIKANA

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vincent Naano, WATAALAMU wa MISITU wa Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma wamefanya ukaguzi wa eneo la kuanzishia Mradi wa BUSTANI/KITALU cha MICHE YA MITI MILIONI 10 (Picha hapo chini).
Kazi ya KUSOMBA UDONGO na MBOLEA ITAANZA WIKI HII chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya na Viongozi wa Idara ya Misitu wa Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Mkuu wa Wilaya ametupatia taarifa kwamba VIROBA MILIONI 1 tayari vimepatikana.
Wiki ijayo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ATANUNUA MATENKI YA MAJI 2 kila moja lenye UJAZO wa  LITA 5,000 (Jumla Lita 10,000, Tshs 2.4M).
Mbunge wa Musoma Mjini, Mhe V Mathayo Manyinyi anakamilisha utaratibu wa kupatikana MBEGU za kuanzia Mradi wetu.
Viongozi wa Nyanja Development Initiative (NDI) na WADAU wengine wa Maendeleo wanaombwa wawasiliane na Mkuu wa Wilaya kuhusu MICHANGO yao. KAZI IMEANZA.
MRADI WA MAZINGIRA NYANJA – VITALU VYA MICHE YA MITI
Ndugu zangu wa Nyanja (NDI): Tunashukuru Marehemu Mrs Esther Mutani tumempuzisha kwenye amani ya milele Kijijini Isanzu, Kwibara. Picha Na 1.

Picha Na 1.

Baada ya mazishi sikurudi Musoma kwa kupitia Bunda badala yake niliamua kuchukua MV Mara, Kivuko kati ya Jimbo la Musoma Vijijini (Buraga) na Jimbo la Mwibara (Kwibara).
Madhumuni ya kupita huko ni kuangalia hali ilivyo ya MV Mara,  Barabara, na Ukataji wa miti vijijini.
Picha Namba 2 na 3 hapo chini zinaonyesha umuhimu wa MRADI WETU… hata VISIWA NDANI YA ZIWA VICTORIA VINAGEUKA KUWA JANGWA – kuza picha hizo uone vipara!

Picha Na 2.

Picha Na 3.

Ndugu zangu:  nilipokaribia Kijiji cha Bhuling nilionana na wasichana kama 10 wamebeba KUNI – mabua ? njiti? majani ya mkonge?… Nilisimama na kuongea nao….ni kilio kitupu!
Ndugu zangu: tusonge mbele na mradi huu.. ni muhimu kwetu na kwa vizazi vijavyo.

FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO ZAPUNGUZA CHANGAMOTO SEKTA YA ELIMU

Mafundi wakiendelea na zoezi la uezekaji wa chumba kimoja cha darasa kwenye shule ya msingi Busamba ambayo ni moja ya shule ambazo zimepokea mgao wa fedha za mfuko wa Jimbo la Musoma vijijini.

Na Fedson Masawa

FEDHA za Mfuko wa Jimbo la Musoma vijijini zimeendelea kuleta mafanikio makubwa na kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwenye shule mbalimbali za msingi na sekondani ndani ya jimbo hilo.

Shule ya Msingi Busamba iliyopo Kata ya Etaro ni moja kati ya shule ambazo zimepokea mgao wa fedha hizo na kununulia mabati 54 kwa ajili ya kuezeka chumba kimoja cha darasa katika shule hiyo.

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Busamba wakizungumza kijijini hapo walisema, kukamilika kwa chumba hicho kimoja kunatokana na mwamko mzuri wa wananchi katika kushiriki shughuli za maendeleo na kuungana na serikali kuboresha miundombinu ya elimu kijijini hapo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Busamba Kadenge Maanya alisema, kuongezeka kwa vyumba vya madarasa shuleni hapo kutasaidia wanafunzi kukaa kwa amani na kujisomea vizuri wakati wote wa masomo.

Aidha, Mwenyekiti huyo alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo na viongozi wengine wa ngazi zote kwa kuipa kipaumbele sekta ya elimu hasa uboreshaji wa miundombinu ya elimu, hali ambayo itasaidia hata walimu kutekeleza vizuri majukumu yao.

Mbali na shule ya msingi Busamba, fedha nyingine za mfuko wa Jimbo zilielekezwa katika shule za msingi 12 na sekondari mbili ambako pia yatanunuliwa mabati 54 kwenye kila shule kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa ya shule hizo.

 

Shule za msingi zilizopata mgao huo ni pamoja na Nyegina “B”, Kambarage, Mugango, Tegeruka, Chanyauru “B”, Busekera, Rusoli “A”, Butata “A”, Bugoji, Kamatondo, Kanyega na Kusenyi huku shule mbili za sekondari zilizonufaika na fedha hizo za mfuko wa Jimbo ni Bulinga na Mabui.

KINYANG’ERERE WAANZA UJENZI WA VYUMBA VINNE VYA MADARASA

Msaidizi wa mbunge James Francis (mwenye fulana nyeupe) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Kinyang’erere muda mfupi baada ya kuwakabidhi matofali 2,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vya shule ya msingi iliyopo kijijini hapo.

 

Na Hamisa Gamba

MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ameungana na wananchi wa kijiji cha Kinyang’erere, Kata ya Bugwema katika ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vya shule ya msingi iliyopo kijijini hapo.

Prof. Muhongo ametoa mchango wa kusafirisha matofali 2,000 kutoka Wilayani Bunda yalipokuwa yanafyatuliwa kwenda Kinyang’erere kwa ajili ya ujenzi huo unaoendelea kwa kasi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Muhagwa Shilumba na diwani wa Kata ya Bugwema Ernest Magembe wakati wakipokea matofali hayo yaliyofikishwa kijijini hapo na msaidizi wa mbunge James Francis, walimshukuru Prof. Muhongo kwa kuwaunga mkono kwenye ujenzi huo ambao ukikamilika  utasaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo.

“Wananchi na viongozi wote wa kata yetu na kijiji wamehamasika na kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, wanajitolea kwa hali na mali na hii ni kutokana na hamasa ya mbunge wetu Prof. Muhongo” alisema Ernest Magembe.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kinyang’erere walimshukuru mbunge wao kwa kuchangia ujenzi huo, ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwenye shule za sekondari na msingi kwenye jimbo la Musoma vijijini linakwisha.

Wakati huo huo, wananchi hao wa Kinyang’erere walitumia nafasi hiyo kumshukuru Prof. Muhongo kwa jitihada anazozifanya ikiwemo suala la kuwagawia mbegu za mihogo, alizeti na ufuta bila malipo na kuahidi kuzitumia mbegu hizo kama ilivyokusudiwa; kulima kwa tija ili kuondokana na umaskini.

HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI ZASHIKA KASI 

Baadhi ya wananchi na viongozi wa kata ya Nyegina na kijiji cha Mkirira wakiwa katika eneo ambalo linajengwa zahanati ya kijiji hicho.

 

Na Fedson Masawa

HARAKATI za ujenzi wa zahanati zinazidi kushika kasi ndani ya Jimbo la Musoma vijijini na kufufua matumaini makubwa kwa wananchi wa Jimbo hilo ya upatikanaji wa huduma bora za afya kwenye vijiji vyao.

Hayo yamebainika baada ya Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini kutembelea eneo la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mkirira kata ya Nyegina na kushuhudia kazi ya ujenzi wa zahanati inayoendelea katika eneo hilo.

Akizungumza na msaidizi wa Mbunge, mtendaji wa kijiji cha Mkirira Iddy Rukonge alisema, wananchi wazawa na wapenda maendeleo wa kijiji hicho waishio nje ya Jimbo la Musoma vijijini wapo tayari kuungana na wananchi na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo katika ujenzi wa zahanati ya kijiji chao ili kuwarahisishia ndugu zao upatikanaji wa huduma ya afya karibu na maeneo wanayoishi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mkirira walisema tayari wamefikia hatua ya msingi (jamvi) kwa kutumia michango yao ya hali na mali na kuthibitisha kuwa, umoja na mshikamano wa serikali na wananchi kijijini hapo ni nyenzo pekee itakayowasaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyegina Majira Mchele alisema, hatua waliyofikia wananchi wa Mkirira inaleta matumaini ukilinganisha na muda walioanza ujenzi huo na kuahidi kushirikiana na wananchi na wapenda maendeleo wa kijiji hicho pamoja na wafadhili kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo mapema.

Naye Paschal Magati ambaye ni mwananchi wa kijiji cha Mkirira alisema: “kwakuwa Mbunge wetu wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ni Mbunge mpenda maendeleo, kwa kushirikiana na serikali tutakuwa ni sehemu ya ratiba yake ili afike aone jitihada zetu wananchi na kuungana na sisi kufanikisha zoezi la upatikanaji wa huduma ya afya kijijini Mkirira.”

Wananchi wa Jimbo la Musoma vijijini kwa kushirikiana na Mbunge wao wamehamasika kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya vijijini kwa kujenga zahanati katika vijiji mbalimbali, zoezi ambalo ukiachilia mbali elimu, nalo limeonekana kuwa kipaumbele cha maendeleo Jimboni, ambapo zaidi ya vijiji 10 vinaendesha miradi ya ujenzi wa zahanati huku zahanati nne za Kigeraetuma, Chirorwe, Mwiringo na Mmahare zikiwa zimefikia katika hatua nzuri ya utekelezaji.

WANANCHI KWIKUBA WAMUUNGA MKONO MBUNGE WAO KWA VITENDO

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwikuba, Kamnyiro Kubega akiwa mbele ya jengo la vyumba viwili vya madarasa ambavyo vinajengwa kwenye shule ya Msingi Kwikuba.

Na. Hamisa Gamba

WANANCHI wa kijiji cha Kwikuba, Kata ya Busambara wamemuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa vya shule ya msingi Kwikuba.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Kamnyiro Kubega, akizungumza kijijini hapo alisema, wananchi wameonyesha kufurahishwa na jitihada zinazofanywa na Mbunge wao katika suala la maendeleo hususani kwenye sekta ya kilimo na elimu, hivyo wameamua kumuunga mkono kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa vya shule hiyo.

Kubega alisema, Prof. Muhongo amekuwa mfano mzuri kwa wananchi wake kwa kuwahamasisha kujitolea kutafuta maendeleo husasani katika kuboresha mazingira ya elimu, ambapo amekuwa akichangia vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani ya jimbo lake.

Naye diwani wa kata ya Busambara Ngero Anthony Kibuyu alisema, jitihada anazozifanya Prof. Muhongo zimekuwa chachu kwa wananchi na viongozi ndani ya kata yake, na sasa wanatarajia kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ambao ulikuwa umesimama kwa muda mrefu.

Diwani huyo alisema, ujenzi huo ukikamilika utawapunguzia wanafunzi usumbufu wa kutembea umbali mrefu kwenda Mugango kufuata elimu na kukutana na hatari nyingi wakiwa njiani.

KIJIJI CHA KASTAM WAJENGA VYUMBA VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Kastam.

Na. Verdiana Mgoma

SERIKALI ya kijiji cha Kastam imefanikiwa kuezeka vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu kwenye shule ya msingi Mkapa baada ya kupokea fedha za Mfuko wa Jimbo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo David Nyakusanja alisema, baada ya serikali kutekeleza mpango wa elimu bure, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi imeongezeka na kusababisha upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na kuwalazimu wanafunzi wake kusoma kwenye mazingira magumu.

Mwalimu Nyakusanya alisema, licha ya jitihada zinazofanywa za ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo, lakini ongezeko la wanafunzi ni kubwa siku hadi siku na kuwalazimu kuwagawa wanafunzi hao katika mikondo miwili, ingawa anaamini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Bukima January Simula alisema, jitihada za uhamasishaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na umoja kutoka kwa wananchi wa kata yake, umetoa mafanikio makubwa hasa baada ya kuona wanakabiliwa na changamoto nyingi za kielimu na kuamua kuungana kuzikabili.

“Kutokana na changamoto kwenye shule, tuliamua kuchukua jukumu la kubadili hali hii, lakini pia tunamshukuru sana Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa dhamira yake kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kastam kurejesha miundo mbinu ya elimu. Hadi sasa kata yangu imefanikiwa kujenga vyumba 8 na kuezeka vyumba 7 kwa nguvu ya mbunge wetu na kila shule imepata vitabu na madawati” alisema diwani Simula.

Diwani huyo aliongeza: “Inaonesha dhahiri jinsi mbunge wetu anavyopenda kuona wananchi wake wakipata elimu na kukua kimaendeleo, ndio maana ameipa elimu kipaumbele jimboni kwake na kila mara amekuwa akiwasihi wazazi kuwekeza kwenye elimu.”

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Kastam wameipongeza Serikali na Mbunge wa Musoma Vijijini kwa kuwaunga mkono kuwasaidia watoto wao kuepukana na mazingira magumu ya kujisomea.

Wananchi hao walisema, wamefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Mbunge wao na serikali katika kuchangia maendeleo ya elimu na kuwawezesha watoto kupata elimu iliyo bora na itakayo wasaidia katika maisha yao ya baadaye, hivyo watajitoa kwa hali na mali kuunga mkono jitihada hizo.

MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI NYANG’OMA WAANZA KUTEKELEZWA

Eneo ambalo mradi wa ufugaji wa samaki utafanyika kwenye kijiji cha Nyang’oma.

Na. Mwandishi Wetu

MRADI wa Ufugaji samaki wa kikundi cha Nyanja kilichopo kwenye Kijiji cha Nyang’oma, Kata ya Mugango umeanza kutekelezwa kwa hatua za awali.

Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wametembelea mradi huo 25, Januari, 2018 na kukuta uzio kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa ya samaki umekamilika.

Msimamizi Mkuu wa mradi huo Shida Mabeba alisema, hatua za awali za ujenzi huo zimekamilika na wanatarajia kumalizia ujenzi baada ya kupata fedha za kujengea mabwawa na hatimaye kununua vifaranga vya samaki na kuanza uzalishaji.

 

VIJANA WA SARAGANA WAUNDA KIKUNDI CHA KILIMO

Na. Mwandishi Wetu

VIJANA wa kijiji cha Saragana kilichopo Wilayani Musoma vijijini, wameunda kikundi kinachoitwa Kwetu Shambani kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo cha bustani ya matunda na mbogamboga.

Kikundi hicho kimelenga kupunguza tatizo la ajira kwa vijana ambao wengi baada ya kumaliza masomo, wamejikuta wakishinda vijiweni na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo vijana hao walisema, baada ya kujadiliana kwa muda mrefu katika kutafuta shughuli itakayowasaidia kuwainua kiuchumi, wakakubaliana kufanya kilimo cha bustani kwa njia ya umwagiliaji.

“Vijana hawa walikaa na kubuni njia na miradi mbalimbali inayoweza kuwainua kiuchumi, na wakaona kitu cha kwanza kinachoweza kuinua maisha yao ni kilimo kwa kuwa nguvu za kulima wanazo” alisema Manyama David mmoja wa wana kikundi hao.

Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho Amos Magesa alisema: “sisi wanakikundi wa Kwetu Shambani, tumeazimia kufanya kazi kwa moyo na kwa nguvu zetu zote na kwa jitihada zaidi, tutaendelea kupanua kilimo chetu baada ya kuwa tumeongeza mtaji na kupata pembejeo za kutosha baada ya mavuno yetu.”

Kwa upande wake Msaidizi wa Mbunge wa eneo kilipo kikundi hicho, Hamisa Gamba aliwaasa vijana hao kujituma zaidi na jina la kikundi chao lisadifu shughuli wanazozifanya.

“Pamoja na kilimo cha bustani ya matunda bado pia mna fursa ya kulima mazao mengine zaidi ya biashara hususani zao la alizeti lisilohitaji gharama kubwa na badala yake mtatumia nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hilo kwa kuwa mbegu za alizeti na ufuta zitatolewa bure hivi karibuni kutoka ofisi ya Mbunge” alisema Hamisa na kuongeza kuwa, vijana hao wakilima alizeti itawainua zaidi kwa kuwa zao hilo wataliuza kwa kilo na kukamua mafuta badala ya kuuza kwa tenga.

WANANCHI NYASAUNGU WAUNGANA KUJENGA ZAHANATI

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyasaungu wakifuatilia kwa makini mkutano wa kujadili kuanza upya kwa ujenzi wa zahanati ya kijiji chao ambao ulisimama kwa miaka mingi.

 Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kusimama kwa muda mrefu bila kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyasaungu, Jimbo la Musoma vijijini, wananchi wa kijiji hicho wamerudi kwa nguvu mpya ya kupanga mikakati ya kuendelea na ujenzi wa zahanati hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa na wananchi wa kijiji hicho mara baada ya kutolewa taarifa kwamba, changamoto zilizokuwa zinakwamisha ujenzi huo uliosimama kwa takribani miaka 12 zinatafutiwa ufumbuzi na hivyo ujenzi unatakiwa kuendelea.

Tayari ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini imekutana na Mganga Mkuu wa wilaya ya Musoma na kupata ufumbuzi wa changamoto hizo na kuwataka wananchi wa kijiji cha Nyasaungu kuungana pamoja kwa kushirikiana na viongozi wao ili kufanikisha huduma ya afya katika kijiji chao.

Kwa upande wao, wananchi wa kijiji hicho kwa kauli ya pamoja wamekubali kuendeleza zoezi hilo haraka iwezekanavyo na kuungana na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo ili kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Wananchi hao wamewaomba viongozi wao wa serikali ya kijiji wakae mapema kwa ajili ya kupanga bajeti na kuirudisha kwao kwa ajili ya kuanza michango na shughuli nyingine ndani ya wiki hii ili kuharakisha ujenzi huo.

Naye Diwani wa kata ya Ifulifu Rashidi Meru kwa niaba ya wananchi wa kata ya Ifulifu na kijiji cha Nyasaungu, ameipongeza ofisi ya Mbunge kwa kuona umuhimu wa kuwa na zahanati katika kijiji cha Nyasaungu na kuungana na wananchi wa kijiji chake katika kufanikisha zoezi la ujenzi huo.

 

NYAMBONO WAFYATUA MATOFALI KWA AJILI YA KUJENGA MADARASA

Mhandisi wa Halmshauri ya wilaya ya Musoma James Gibai (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mafundi waliopewa tenda ya kuendesha zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Nyambono.

Na. Hamisa Gamba

WANANCHI wa kata ya Nyambono wameanza zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba  viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Nyambono ili kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Hatua hiyo ni katika kujiandaa kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza wanaotarajia kuanza muhula wa kwanza wa masomo Januari 2018.

Mtendaji wa kata ya Nyambono Ernest Maregesi akizungumza na mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Musoma James Gibai alisema, mradi huo wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa unaendeshwa na vijiji vya Nyambono na Saragana.

Maregesi alisema, wananchi wamekubali kuchangia nguvu zao kushiriki katika ujenzi huo, hivyo aliwaomba wananchi na viongozi wote ndani ya eneo hilo kushirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha wanaondoa tatizo la wanafunzi kukosa madarasa ya kusomea kabla ya tarehe ya kufungua shule Januari, 8, 2018.

Kwa upande wake mhandisi Gibai aliwaasa viongozi wa kata hiyo kusimamia kwa uangalifu miradi yoyote inayoendeshwa katika eneo hilo ili kutowavunja moyo wananchi wanaochangia nguvu zao katika shughuli hizo za maendeleo.

KUSENYI WAPATA MTAMBO WA KUKAMULIA ALIZETI

Pichani ni mashine ya kukamulia alizeti uliosimikwa katika kijiji cha Kusenyi, unaosimamiwa na Yahya Chogero na Martha Simiti wanaotoa huduma kwa wakazi wa Musoma vijijini.

Na. Verdiana Mgoma

WANANCHI wa Jimbo la Musoma vijijini wameonesha furaha yao baada ya kufanikiwa katika kilimo cha zao la alizeti kwa kuamini kupitia zao hilo wanaweza kuinuka kiuchumi.

Afisa kilimo wa kijiji cha Kusenyi Masinde Mjarifu alisema, alizeti hulimwa kwa wingi kwenye mikoa tofauti Tanzania na zao hilo hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara na hivi sasa wameamua kulipa kipaumbele zao hilo ikiwa ni mbadala wa zao la mahindi ambalo walilitegemea hapo awali.

“Kupitia zao hilo ambalo ni jipya kwa wakazi wa Musoma vijijini tumetoa semina mbalimbali juu ya kilimo hiki kuanzia hatua ya upandaji, namna ya kudhibiti wadudu na magonjwa na elimu juu ya uvunaji, kupitia mafunzo haya tuna uhakika wa kupata mavuno mengi msimu ujao kutokana na mwitikio wa wakulima” alisema Mjarifu.

Mjarifu alisema, licha ya wakazi wa eneo husika kulipokea zao hilo la alizeti lililohamasishwa na mbunge wao wamehaidi kulifanya kama zao la biashara ili kuinuka kiuchumi.

“Wanafurahishwa na juhudi za mbunge kusogeza huduma ya mtambo wa kukamulia mafuta na bidhaa nyingine kama mashudu huku wakionesha kuwa na mwamko wa kulima zao hilo” alisema.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kusenyi Magesa Mashauri alimshukuru Prof. Sospeter Muhongo kwa juhudi anazoendelea kuzionyesha hasa kuwapatia kipaumbele kwenye sekta ya kilimo mbali na uhamasishaji, walipokea mbegu za mihogo, mtama na alizeti bila ya malipo lengo kuu ni kukuza kilimo jimboni.

“Tunaendelea kumuunga mkono mbunge wetu kwa kujivunia, hatutategemea tena zao la aina moja tena jimboni” alisema Magesa Mashauri.

MKAZI WA NYAMBONO AANZISHA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI

Mafuru Maganira mkazi wa kijiji cha Nyambono (mwenye suruali nyekundu) akitoa maelezo juu ya mradi wake wa ufugaji wa samaki kwa watu waliomtembelea.

Na. Hamisa Gamba

MKAZI wa kijiji cha Nyambono Mafuru Maganira ameanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kijijini hapo ili kukidhi mahitaji ya jamii kwenye suala la kitoweo na kujipatia ajira na kipato.

Maganira akizungumza kwenye eneo analofuga samaki hao alisema, hivisasa anafuga samaki aina ya sato ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakipatikana kutoka ziwa Viktoria, lakini yeye anawafuga kwenye mabwawa na kufuata taratibu zote za ufugaji.

“Nimeanzisha mradi huu kwa kuanza na samaki elfu mbili (2,000) ili kwa baadaye nitakapokuwa nimezalisha natarajia kuukuza mradi huu” alisema mjasiriamali huyo.

“Iwapo wananchi watakuwa wazalendo kwenye mradi huu, na kuacha suala la wizi wa kuvua samaki kinyume na utaratibu na hila mbaya za kuua samaki kwa sumu, baada ya muda mfupi tu, samaki watakuwa tayari kwa mavuno, ajira na kitoweo vitapatikana kwa wananchi ndani na hata nje ya kijiji” alisema Maganira.

Aidha, mjasiriamali huyo ameomba wataalamu kumtembelea na pia kuitika wito mara atakapohitaji msaada wao ama tiba ili kuokoa maisha ya samaki hao.

Hata hivyo, Mafuru Maganira amewakaribisha  wanaohitaji kutembelea bwawa hilo kwa lengo la kujifunza na kufahamu jinsi ya kuanza mradi huo.

“Nashauri watu wawe wabunifu kwenye ujasiriamali ili kujiongezea kipato kitakachokidhi mahitaji yetu, pia nawaomba viongozi, na serikali kuniunga mkono pale nitakapokuwa na hitaji juu ya upanuzi wa mradi wangu”

KOME WAONGEZA KASI UEZEKAJI WA VYUMBA VYA MADARASA

 Na. Fedson Masawa

SERIKALI ya kijiji cha Kome kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho wameongeza kasi katika zoezi la utekelezaji na usimamizi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa baada ya kuezeka chumba kingine cha darasa katika shule ya msingi Kome B.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kome Kwanjula Jeremia alisema, kijiji chake kilipokea jumla ya mabati 60 kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono kwa jitihada kubwa wanazoendelea nazo katika kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Tulipokea mabati 60 kutoka kwa DC kwa ajili ya kuezeka chumba kimoja cha darasa na sisi kama serikali tunapenda kutoa shukrani kwa wadau waliotuchangia na wanaoendelea kutuunga mkono akiwemo Mbunge wetu Prof. Muhongo na halmashauri ya wilaya ya Musoma” alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo kukamilika kwa zoezi la uezekaji wa chumba hicho kimoja inafikisha jumla ya vyumba viwili na ofisi moja ambavyo tayari vimeezekwa kati ya vyumba 10 na ofisi tano katika shule ya msingi Kome B vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kome “B” Sijaona Sokoro alisema amefarijika na hatua ya serikali kuendelea kuichangia shule yake kwani hatua hiyo itaokoa taaluma ya wanafunzi ambao kipindi hiki cha mvua wanaweza kukosa masomo kutokana na kurundikana madarasani wanapokimbilia kujikinga mvua.

“Ninafarijika sana ninapoona viongozi na serikali kwa ujumla wakiendelea kujitoa katika kusaidia watoto wetu ili kuimarisha taaluma yao. Pia nizidi kuwaomba viongozi wetu, Prof. Muhongo na wananchi kuendelea kutupa sapoti katika vyumba vilivyobakia kwakuwa zoezi hili ni sehemu ya majukumu yetu” alisema mwalimu Sokoro.

SHULE ZA MSINGI MUSOMA VIJIJINI ZAONGEZEKA

Muonekano wa shule ya msingi AGAPE yenye mchepuo wa Kiingereza (English Medium) iliyopo katika kata ya Bukima kijijini Bukima karibu na barabara ya kuelekea kijiji cha Busungu. Shule hii ina jumla ya madarasa sita na wanafunzi 70.

Na. Mwandishi Wetu

SHULE za msingi za jimbo la Musoma vijijini zimeongezeka kutoka shule 111 na kufikia shule 112 baada ya shule ya msingi AGAPE ambayo ni shule ya binafsi kupata usajili rasmi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmiliki wa shule hiyo iliyopo katika kata ya Bukima kijiji cha Bukima Andrea Kayola alisema, kwa sasa shule hiyo ina madarasa sita likiwemo darasa moja la awali.

“Jamii ina mahusiano mazuri sana na shule, lakini ukiachilia mbali walimu wa shule, wafanya kazi wengine nimewapa kipaumbele vijana wa eneo la kata hiii ya Bukima” alisema Kayola na kuongeza kuwa, endapo kutakuwa na uhitaji zaidi bado anatoa kipaumbele kwa wakazi wa jimbo la Musoma vijijini.

Mmiliki huyo aliwaomba wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kufanikisha mahitaji ya elimu kwa watoto wanaosoma katika shule hiyo ikiwa ni pamoja na vitabu na kompyuta kwani shule ina kituo cha TEHAMA.

Kwa upande wake ofisi ya Mbunge imeahidi kuijumuisha shule hiyo katika mgao wa vitabu kwakuwa imetambulika rasmi na pia inayo maktaba ambayo inaifanya shule hiyo kuwa moja ya shule zinazotimiza vigezo vya kupewa vitabu ili kuwasaidia watoto hao katika masomo yao.

UJENZI WA MABWENI SEKONDARI YA KASOMA WAENDELEA VIZURI 

Mafundi wakiendelea na zoezi la ujenzi wa mabweni ya wavulana kwenye shule ya sekondari Kasoma iliyopo kata ya Nyamrandirira.

Na. Verdiana Mgoma

UJENZI wa mabweni ya wanafunzi shule ya Sekondari Kasoma unaendelea vizuri huku wananchi na viongozi wa kata ya Nyamrandirira wakiwa na matumaini ya kupunguza changamoto za elimu zinawakabili watoto wao.

Diwani wa kata ya Nyamrandirira Ruteli Maregesi alisema, ujenzi unaoendelea shule ya sekondari Kasoma ni msaada uliotolewa na serikali ili kuunga mkono shughuli za maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo na jimbo la Musoma vijijini kwa ujumla.

Maregesi alisema, wazo la kuanza kwa mradi huo lilitokana na kuwapo kwa changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo hasa kwa upande wa mabweni na vyumba vya madarasa na kusababisha kero kubwa kwa walimu, wanafunzi na hata wazazi.

Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kasoma Nelson Makaro akizungumzia changamoto zinazowakabili shuleni hapo alisema, hawana nyumba za walimu, wana upungufu wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya choo.

Alisema, kutokuwepo kwa nyumba za walimu kunasababisha walimu wengi kuishi mbali na shule na pengine kushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

“Mabweni ni ya muhimu sana maana yana faida nyingi kwa wanafunzi, kama hakuna mabweni kunawapa ugumu hasa walimu kusimamia usomaji wao na kwa kuwa mazingira tuliyopo siyo rafiki sana hasa kwa wanafunzi wa ‘day’” alisema Mwalimu Makaro.

Mwalimu huyo aliongeza: “wanafunzi waliowengi wanatoka mbali, kufika shule ilipo wanalazimika kutembea umbali mrefu, hivyo wengine wanajiingiza katika makundi mabaya na hivyo kupotea katika mwelekeo wa masomo.”

Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Nyamrandirira Joseph Lyakurwa alisema, kuna baadhi ya vitu ambavyo wameona wao viongozi wakivisimamia vinakuwa ni nguzo hasa katika kuboresha sekta ya elimu.

“Tumeamua kuweka ushirikiano bora na wadau wetu wa elimu; yaani wazazi, walimu, wanafunzi na viongozi wa kisiasa kuwekeza katika elimu. Juhudi zetu zinaonekana na zimetupa matumaini zaidi hasa kusimamia shughuli ya maendeleo shuleni hapa. Mpaka sasa ujenzi unaoendelea shuleni tumekamilisha vyumba sita vya madarasa na sasa tupo kwenye ujenzi wa vyumba 40 vya mabweni na matundu ya choo sita pamoja na mabafu” alisema Mtendaji wa kata ya Nyamrandirira Joseph Lyakurwa.

WANANCHI KINYANG’ERERE WAPAMBANA NA UHABA WA MADARASA

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kinyang’erere wakishikiriana kwenye zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Na. Mwandishi Wetu

WANANCHI wa kijiji cha Kinyang’erere na viongozi wao wameanza shughuli ya ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi iliyopo kijijini hapo.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kero ya muda mrefu ya wanafunzi kusoma chini ya miti kutokana na uhaba wa madarasa na wakati mwingine watoto wa madarasa mawili tofauti kusoma ndani ya chumba kimoja hali ambayo inachangia kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu hafifu kwenye mitihani ya kitaifa.

Mtendaji wa kijiji cha Kinyang’erere Paulo Ndoro akizungumza na msaidizi wa mbunge aliyefika kijijini hapo kukagua shughuli za maendeleo, aliahidi kuimarisha mpango kazi wake katika kijiji hicho na kuhakikisha shida ya vyumba vya madarasa inapungua na kwisha kabisa kwa siku za usoni.

Ndoro mbali na kupongeza jitihada anazofanya mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo katika kuboresha mazingira ya elimu jimboni mwake, aliomba Ofisi ya Mbunge kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wananchi wa kijiji hicho hivi sasa.

Mtendaji huyo aliomba mbunge awasaidie mifuko ya saruji ili kukamilisha shughuli za ujenzi wanaotarajia kuanza hivi karibuni baada ya zoezi la ufyatuaji matofali kukamilika.

Naye diwani wa kata ya hiyo, Ernest Maghembe aliwaomba walimu wa shule ya msingi Kinyang’erere kuwa wavumilivu na kuendelea kujitoa kwa moyo katika ufundishaji licha ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa makazi na huduma nyingine za elimu.

Kwa upande wake msaidizi wa Mbunge, Hamisa Gamba aliwaomba viongozi wa kata hiyo, kushirikiana na ofisi ya Mbunge kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo ya elimu ili kuondoa adha ya wanafunzi kusoma chini ya miti.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUINUA UCHUMI  MUSOMA VIJIJINI

Diwani wa kata ya Rusoli, Boazi Nyeula akikagua moja ya bustani ya matikiti wakati wa ziara yake ya kutembelea wakulima wa bustani ndani ya kata yake.

Na Mwandishi Wetu

VIKUNDI mbalimbali vya kilimo cha bustani vinavyotumia teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Musoma vijijini vimesema kilimo cha umwagiliaji ndio njia pekee itakayosaidia jamii za jimbo hilo kujiinua katika kipato chao na uchumi kwa ujumla.

Akizungumza katika kijiji cha Bugunda kata ya Bwasi, Gudrack Wambwe ambaye pia ni msimamizi mkuu wa kikundi cha No Sweat No Sweet kinachojishughulisha na kilimo cha bustani alisema, jimbo la Musoma vijijini limezungukwa na Ziwa Victoria, ni eneo lenye mashamba ya kutosha kulima kwa kutumia hata teknolojia ndogo ya umwagiliaji inayoweza kumuongezea mkulima kipato chake hasa wakati wa kiangazi.

Wambwe alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo kusambaza mashine 15 kwa vikundi 15 jimboni kwake na vikundi hivyo kwa sasa vimekuwa mfano bora na kivutio tosha kwa vijana wengine kuhamasika na kuamua kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji.

Msimamizi huyo alisema, ili kufanikisha zoezi la kuinua uchumi wa jamii ya Musoma vijijini, ni muhimu pia vikundi vipya vilivyojitokeza kwenye kilimo hicho kusaidiwa vifaa vitakavyowawezesha kufanikisha shughuli hizo ikiwa ni pamoja na mashine na mipira mirefu.

Naye Diwani wa kata ya Rusoli, Boazi Nyeula alisema ni jambo la kushangaza kuona eneo la Musoma vijijini kufikia hatua ya kuwa na upungufu wa chakula wakati mikoa isiyo na maji ya kutosha inazalisha chakula kingi kwa kutumia maji ya mito na mabwawa, wakati Musoma vijijini wakishindwa kutumia maji ya ziwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji jambo ambalo linapelekea jamii zao kutumia fedha nyingi kununua chakula kidogo kuliko kutumia fedha kidogo kuzalisha chakula cha kutosha.

Diwani Nyeula alisema, muda umefika sasa kwa viongozi kuona ni namna gani ya kupata mashamba makubwa ya kutosha na kupata mashine kubwa ili kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji na jimbo kujilisha kwa kutumia rasilimali zao walizonazo na hata kujiongezea kipato cha kaya.

Alisema, sambamba na kuwaza kupata miradi mikubwa ya kuzalisha kwa wingi, ni vyema kuongezea mashine ndogondogo kwa ajili ya wakulima wadogowadogo waliopo kwenye vikundi ili kuwapa nguvu ya kutumia muda mfupi kufanya kazi inayoeleweka.

“Nadhani ni muda muafaka sasa sisi kama serikali kukaa na kutafakari ni namna gani tunaweza kutumia rasilimali za jimbo letu ili kuzalisha chakula cha kutosha bila kutegemea chakula kutoka maeneo mengine. Kinachotakiwa hapa ni kupanga, kupata uwezeshwaji na kubaini maeneo yetu yanayoweza kuwekezwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji” alisema diwani Nyeula.

Kwa upande wao maafisa kilimo Mshangi Salige wa kata ya Bukima na Hassan Magili kata ya Bwasi, wanaamini endapo wakiwa na vikundi vya kutosha na maeneo yatakayoweza kupendekezwa na jamii au serikali za vijiji husika, upo uwezekano wa jimbo kukomesha kabisa tatizo la upungufu wa chakula ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara hasa wakati wa kiangazi kwani kutakuwa na muendelezo wa kuzalisha chakula kisichokuwa cha msimu.

Wameongeza kuwa, mipango yote hiyo itawezekana endapo tu wakulima wakiwezeshwa na serikali za vijiji kuwa na mipango bora yenye tija kwa jamii.

KIJIJI CHA MABUI WADHAMIRIA KUMALIZA CHANGAMOTO ZA ELIMU

Mafundi wakiwa katika zoezi la ujenzi wa jengo la vyumba vitatu vya madarasa vya Shule ya Msingi Mabui. Wengine ni diwani wa kata ya Musanja Elias Ndaro (aliyebeba tofali) na Mwenyekiti Julius Tumbo (aliyevaa suti nyeusi).

Na. Verdiana Mgoma

WANANCHI wa kijiji cha Mabui, viongozi wao pamoja na watendaji wa wilaya na Halmashauri ya Musoma vijijini wamedhamiria kupunguza changamoto wanazo kabiliana nazo hasa kwa upande wa sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa.

Mratibu elimu kata ya Musanja, Mahendeka Kasanje akizungumza kijijini hapo alisema, baada ya serikali kuanza kutekeleza mpango wa elimu bure, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi imeongezeka na kusababisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa.

Kasanje alisema, ongezeko hilo la wanafunzi mbali na kusababisha upungufu wa vyumba vya madarasa, wanakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo na vifaa vya kufundishia.

“Tuna changamoto nyingi kama nyumba za walimu, matundu ya choo, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, lakini uhaba wa vyumba vya madarasa unaathiri sana upande wa taaluma mpaka sasa bodi ya shule kwa upande wa shule ya msingi tumejiwekea mikakati kuhakikisha tunatatua changamoto tulizo nazo” alisema Kasanje.

Naye mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mabui Merafuru, Kimodoi Nyauri alisema, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 522 vyumba vilivyopo ni vitano, mahitaji ni vyumba 13, upungufu ni vyumba vinane.

“Tatizo la vyumba vya madarasa ni kubwa na imepelekea wanafunzi wa madarasa hasa ya chini kusomea nje. Kwa juhudi alizofanya mbunge wa Musoma Vijijini tunamshukuru maana kwa msaada wake tumejenga boma la vyumba vinne na ofisi mbili za walimu” alisema.

Aidha, mwalimu Nyauri aliongeza kuwa, walipokea madawati na vitabu kutoka kwa mbunge, hivyo changamoto ya madawati na vitabu imepungua na kuahidi hawatomuangusha, watajitahidi kuinua taaluma.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Musanja Elias Ndaro alisema, wanaendelea kuwashawishi jamii kuwekeza zaidi kwenye elimu na kuhamasisha jamii kuonyesha mchango wao wa hali na mali kwa kumuunga mkono mbunge aliyejitoa kwenye kata hiyo hasa kwenye upande wa elimu.

“Mimi kama mwakilishi wao nitajitahidi kuwa mstari wa mbele hasa kuboresha miundo mbinu kwa upande wa elimu hasa mifumo ya maji, vyumba vya madarasa na matundu ya choo na tunaimani hilo litawezekana” aliahidi diwani huyo.

Hata hivyo, diwani Elias Ndaro alisema, kata hiyo imepokea misaada mbalimbali kutoka ofisi ya mbunge ikiwemo shilingi milioni 70 kwa ajili ya uezekaji wa vyumba vya madarasa ambazo zilitoka kwenye mfuko wa jimbo.

“Tulipokea mifuko 60 ya saruji, tumejenga boma la vyumba vitatu ambalo awali liliezuliwa na upepo, tulipokea madawati kwa kata nzima na vitabu vya kujifunzia kwa shule za msingi na sekondari” alisema Elias Ndaro.

BUSTANI ZAWAINUA VIJANA SARAGANA

Mmoja wa wanachama wa kikundi cha Tujitume kilichopo kijiji cha Saragana akiwa mbele ya shamba la mahindi linalomilikiwa na kikundi hicho.

Na. Hamisa Gamba

VIJANA wa kikundi cha Tujitume kilichopo kijiji cha Saragana wamekiri kuanza kuona matunda kutokana na kilimo cha bustani walichoanza baada ya kuhamasishwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo.

Kikundi hicho tangu kilipoanza, kimekuwa kikilima nyanya, kabichi, na baadhi ya mazao ya chakula ikiwa ni pamoja na mahindi.

Mmoja wa vijana wa kikundi hicho Masatu Malima ambaye pia ni Mwenyekiti alisema, sasa ni msimu wa tatu tangu walipounda umoja huo, ambapo katika awamu zote walizovuna wamefanikiwa kuingia sokoni na kile walichokipata kimewasaidia kujiendeleza na uzalishaji mwingine na hata kutimiza mahitaji yao ya kila siku.

“Hali hii inachangia kutupa moyo na kuendelea kujituma katika shughuli za maendeleo hususani kilimo” alisema Malima.

Kwa upande wake Mkaka Mashauri ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi hicho aliwasihi vijana wenzake kutupilia mbali suala la uvivu na kuzurura hovyo mitaani, kujiepusha na matendo mabaya kama wizi na pia kujikwamua kutoka kwenye umaskini, kwani mali iko shambani na hakuna mafanikio bila kujishughulisha.

Mbali na mafanikio hayo, vijana hao waliomba wasaidiwe vitendeakazi mbalimbali kwa ajili ya shughuli zao za kilimo ili waweze kupanua uzalishaji wao.

WAHAMASISHWA KULIMA BILINGANYA

Mkulima wa bilinganya Mariamu Makaranga akiwa shambani kwake aking’olea magugu huku akisaidiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Chumwi Mafwiri Mkama.

Na. Verdiana Mgoma

ZAO la bilinganya ni zao ambalo lipo katika jamii ya mimea inayohusiana na nyanya, pilipili, viazi mviringo na nyanya mshumaa. Bilinganya ina madini aina ya chokaa na chuma pia ina vitamin A, B na C.

Matumizi ya zao hili hutumika kama mboga au kiungo cha mboga pekee na wengine huchanganya na mboga nyingine mahitaji ya zao hili ni hali ya hewa yenye joto la wastani na udongo tifutifu wenye kina kirefu usiotuamisha maji.

Maandalizi ya shamba ni muhimu na miezi mizuri inayoshauriwa kitaalamu ni miezi isiyokuwa na mvua nyingi, huoteshaji wa mbegu unaweza kuanzia kwenye vitalu au kupanda moja kwa moja kwenye mashimo.

Afisa kilimo wa Kata ya Nyamrandirira Eliakimu Mwanga anasema, mavuno kwa kawaida hupatikana kwa wingi iwapo zao hili litatunzwa vizuri na kitaalamu, pia mavuno mengi hutegemea aina ya bilinganya, umwagiliaji na rutuba ya udongo. Kwa upande wa masoko, halina ushindani mkubwa katika masoko ya ndani kama yalivyo masoko ya nyanya.

Mkulima wa bilinganya Mariam Makaranga ambaye analima na familia yake anasema, aliamua kulima zao tofauti maana walio wengi wamejikita katika kilimo cha nyanya, matikiti na mboga mboga.

Mkulima huyo anasema, alivutiwa na kilimo cha bilinganya baada ya kupata mafunzo kwenye baadhi ya semina za kilimo alizofanikiwa kuhudhuria.

“Nimeanza na heka moja kwa majaribio lengo langu ni kuwataka akina mama na vikundi kuwa wabunifu hasa kwenye upande wa kilimo,  tulime mazao tofauti kuliko kujikita kwenye kilimo cha aina moja tu” anasema Mariamu.

Aidha, Mariamu Makaranga aliomba wapatiwe wataalamu watakao elimisha sekta ya kilimo ili wapate mavuno mengi zaidi ya wanayopata hivisasa.

“Serikali ituongezee nguvu kazi (mashine, madawa, pampu na mbegu) tupate mikopo itakayo tuwezesha vikundi kujikimu, kuwepo na masoko ya uhakika kwa mazao tunayolima, wengi walio kama mimi tumeamua kujiajiri, hivyo tunaomba kuogezewa nguvu kutoka serikalini” anasema Mariamu.

KIJIJI CHA BUJAGA WAONGEZA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Kurugongo B. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mtendaji wa Kijiji cha Bujaga Frank Anatory.

 Na Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Bujaga wamefikia hatua nyingine muhimu ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Kurugongo B na kukamilisha idadi ya vyumba vinne na ofisi moja shuleni hapo.

Ujenzi huo umefikia hatua nzuri ambapo boma hilo linaelekea usawa wa lenta, hatua ambayo kwa taarifa iliyotolewa na mafundi wa jengo hilo litakamilika ndani ya wiki itakayoanza Jumatatu ya 14, Agosti 2017.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mtendaji wa kijiji hicho Frank Anatory alisema, kwa kutumia mchango mzuri wa saruji 60 waliyopewa na Mbunge wao, kijiji chake kilifyatua matofali ya kutosha na anaamini jengo hilo litakamilika kwa wakati muafaka.

Mtendaji huyo alisema, anaamini licha ya mapungufu kujitokeza, idadi ya matofali yaliyopo ni mengi na yatamaliza madarasa hayo mawili na yatakayobakia watayatumia kufunga awamu za vyumba vyote viwili vya jengo lililoezekwa kwa mara ya kwanza.

“Sina hofu kabisa na mahitaji ya jengo tunaloendelea kulijenga kwani tulifyatua matofali mengi kwa kutumia saruji tuliyopewa na Mbunge Prof. Muhongo na yatakayobaki tutayatumia kufungia awamu ya jengo lililoezekwa mapema ndani ya mwezi huu” alisema Mtendaji Anatory.

Aidha Anatory alingeza, kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kurugongo B na hamasa waliyonayo wananchi wa kijiji cha Bujaga, ameomba kama kuna saruji nyingine wapewe ili kukamilisha mapungufu hayo.

Hata hivyo, ofisi ya Mbunge imeitaka serikali ya Kijiji cha Bujaga kwa kushirikiana na wananchi wao kuendelea kutumia jitihada na umoja wao walionao ili kuhakikisha uhaba wa vyumba vya madarasa unakwisha katika shule hiyo.

Sambamba na hilo viongozi hao pia wamezidi kukumbushiwa suala la muda wa matumizi ya vifaa vinavyotolewa na Mbunge.

 

IFULIFU WAJIDHATITI KWENYE KILIMO CHA BUSTANI

Matiku Chacha akinyunyizia dawa ya kuulia wadudu miche ya nyanya katika moja ya bustani zao.

Na. Mwandishi Wetu

WANANCHI wa Jimbo la Musoma vijijini wameendelea kujikita katika kilimo cha bustani ili kujikwamua kiuchumi na kupambana na umaskini.

Hayo yamedhihirika wakati wa ziara ya msaidizi wa Mbunge Ramadhan Juma kwenye baadhi ya maeneo yanayolimwa bustani katika Kata ya Ifulifu.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wakulima hao, Msaidizi huyo wa Mbunge aliwapongeza kwa juhudi wanazozionyesha katika kupambana na umaskini na kujiajiri.

“Sisi wananchi wa Musoma tulikuwa na mawazo hasi kwa muda mrefu, tulitegemea sana misaada wakati uwezo wa kufanya kazi tunao, tunalo ziwa hivyo hatuna sababu ya kulia umaskini, tutumie maji ya Ziwa Victoria kujikwamua kiuchumi nanyi mmeonesha mfano kwa jinsi mlivyotumia maji ya ziwa katika kilimo. Nawapongezeni sana na niwaombe kile mnachozalisha, mkitumie kwa matumizi sahihi” alisisitiza.

Wakiwasilisha kilio chao mbele ya Msaidizi wa Mbunge, wakulima hao wameelezea changamoto wanazokumbana nazo na kuomba kama upo uwezekano, ofisi ya Mbunge iwasaidie.

Baadhi ya changamoto walizotaja ni ukosefu wa vitendea kazi pamoja na kukosekana kwa soko la uhakika mara wanapovuna mazao yao.

“Tunakushukuru sana kwa kututembelea, tunakuomba mtusaidie kutafuta masoko kwa ajili ya mazao yetu. Tunakata tamaa pindi tunapovuna na kukosa soko la uhakika, ninyi mnaweza kutusaidia kutatua changamoto hii” alisema Matiku Chacha na kuungwa mkono na Kushaka Jumanne aliyeongezea kwa kuomba mashine za kumwagilia kama walivyopewa baadhi ya vikundi jimboni.

Akijibu baadhi ya changamoto hizo, Msaidizi wa Mbunge Ramadhan Juma amewataka wakulima hao kuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa idara ya kilimo kwa ajili ya kupata ushauri wa kitaalamu na pia kutambua zao lipi lina soko kwa kipindi hicho.

Kuhusu suala la mashine amewaomba wawe wavumilivu fungu likipatikana watasaidiwa na kuwahakikishia Mbunge yuko pamoja nao hivyo waongeze juhudi ili kulikwamua jimbo la Musoma vijijini katika dimbwi la umaskini.

TUMEAZIMIA KUKOMESHA NJAA – WASEMA BUGWEMA WARD GARDEN GROUP

Katibu wa kikundi cha BUGWEMA WARD GARDEN GROUP Moris Abuga akiwa kwenye moja ya mashamba ya kikundi hicho. 

Na. Hamisa Gamba

KIKUNDI cha kilimo cha bustani cha Bugwema Ward Garden kilichopo kijiji cha Bugwema kimeazimia kukomesha njaa ndani na nje ya kata hiyo.

Katibu wa kikundi hicho Moris Abuga, ameeleza wazi kwamba, hakuna haja ya wao kulia njaa wakati wana nyenzo za kilimo na viongozi wanaowatia nguvu kuwajibika.

Moris alisema, kutokana na hali ya hewa kubadilika hapo nyuma na baadhi ya familia kuwa na upungufu wa chakula, kikundi chao sasa kimeamua kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama viazi, mahindi, matikiti maji na mazao mengine ya bustani.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bugwema Ernest Magembe, alielezea kufurahishwa kwake na jitihada zinazofanywa na kikundi hicho na jinsi wanavyowajibika kikamilifu shambani na hivyo kukubaliana na kauli ya wanakikundi hao ya kukomesha njaa ndani na nje ya kata hiyo inawezekana.

Hata hivyo, vijana wa kikundi hicho wakizungumza kwa nyakati tofauti wamewataka vijana wenzao kujishughulisha na kazi badala ya kuzurura mitaani huku wakitoa angalizo kwa wafugaji wasiothamini kazi za wakulima hao na kuachia mifugo ikirandaranda kushambulia mazao yao.

UMOJA WA AKINAMAMA NYAMBONO WAJITOSA KILIMO CHA BUSTANI

Sehemu ya bustani ya kikundi cha Umoja wa akinamama Nyagogo.

Na. Hamisa Gamba

KIKUNDI cha Umoja wa akinamama Nyagogo kilichopo kwenye kijiji cha Nyambono, kimejitosa kwenye kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda ili kujipatia kipato kitakachowawezesha kuendesha maisha yao.

Hatua hiyo ya akinamama kuwajibika na kilimo cha bustani inakuja baada ya kauli za viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuwataka wananchi wa jimbo hilo kujishughulisha ili kupambana na umaskini.

Mmoja wa akinamama hao Semeni Joram alisema, mara kwa mara wamesikia kauli ya wanawake na maendeleo, hivyo nao wamehamasika nasasa wameamka na kuanza kilimo hicho.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Tabu Christopher alisema, pamoja na mafanikio waliyoanza kuyapata siku za nyuma kutokana na kilimo, zipo changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi, hivyo walimuomba Prof. Muhongo awasaidie vitendea kazi ili kuinua kikundi chao.

Mwenyekiti huyo alisema, hivisasa wamelima mbogamboga na vitunguu na wameahidi kupanua kilimo chao iwapo watapata msaada wa mashine za umwagiliaji.

KIKUNDI CHA NO SWEAT NO SWEET  WAUZA MATIKITI ZAIDI YA 5000

Wanachama wa kikundi cha No Sweat No Sweet wakiwa wameshika mazao waliyovuna tayari kwa ajili ya kupeleka sokoni.

 

Na. Fedson Masawa

WANACHAMA wa kikundi cha No Sweat No Sweet cha kijiji cha Bugunda wamejipanga kuanza msimu mpya wa kilimo baada ya kuuza mavuno yao ya matikiti maji zaidi ya 5000.

Katibu wa kikundi hicho Daudi Silasi alisema, baada ya kuvuna na kuuza mazao yao, tayari wameanza maandalizi ya kuingia msimu mwingine kwasababu hiyo ndio ajira yao, hivyo hawana muda wa kupoteza vijiweni.

Naye mwenyekiti wa kikundi hicho Gudrack Wambwe alisema, kikundi chao kilikuwa na mpango wa kulima mahindi, lakini kwa taarifa walizozipata kutoka kwenye vikundi vingine vyenye mradi kama huo, mahindi bado yana tatizo kubwa la kushambuliwa na wadudu, hivyo watashindwa kufikia malengo yao.

Mwenyekiti huyo alisema, kwasasa wanafanya uchunguzi wa kina juu ya tatizo hilo na kufikia 5, Agosti kama watabaini tatizo hilo linaendelea na hakuna ufumbuzi wa dawa za kudhibiti wadudu hao, kikundi chao kitaendelea na kilimo cha matikiti maji hadi hapo wataalamu watakapowasaidia kutatua tatizo hilo la wadudu wanaoshambulia mahindi.

“Tulipanga baada ya musimu huu tuanzishe mradi wa kilimo cha zao la mahindi kama zao la chakula, lakini kuna wenzetu wamekuja hapa juzi kutuomba dawa za kuuwa wadudu wanao shambulia mahindi kwani wamelima mahindi na yanaendelea kushambuliwa. Tutafanya uchunguzi ikishindikana tutaendelea na matikiti maji” alisema Wambwe.

Kwa upande wake Kunyoka Msilikale ambaye ni mwanachama wa kikundi hicho, aliwashukuru viongozi wa serikali kwa mchango wao ambao ndio unaowasaidia kupata mafanikio makubwa katika shughuli zao za bustani.

Msilikale pia alimpongeza Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kwa usimamizi wake mzuri kupitia wasaidizi wake jimboni na ofisi yake inaweza kufika muda na wakati wowote shambani ili kupokea changamoto zao.

“Tunapenda kuwashukuru viongozi wetu wa serikali, lakini pongezi nyingi zimfikie Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa usimamizi wake jimboni hasa baada ya kutuwezesha kupitia mfuko wa jimbo. Ofisi yake pia inaweza kufika muda wowote na kwa wakati hasa anapopigiwa simu anafika na kumueleza changamoto na mahitaji yetu” alishukuru Msilikale.

WANANCHI BUKUMI WASHIRIKI KUKAMILISHA UJENZI WA CHUMBA CHA DARASA

Wananchi wa Bukumi wakishiriki ujenzi unaoendelea wa chumba kimoja cha darasa.

Na. Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Bukumi wameshirikiana kwa pamoja katika ukamilishaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ambacho tayari kimeezekwa kwa mabati 54 yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo.

Hatua hiyo ya ukamilishaji ni sehemu ya msaada wa mifuko 60 ya saruji iliyotoka kwa Mbunge wao na ujenzi huo umefikia hatua nzuri ambapo hadi sasa mafundi wapo katika hatua ya upigaji ripu pamoja na kuweka sakafu, zoezi ambalo linakaribia ukingoni.

Akitoa taarifa ya ukamilishaji wa chumba hicho kwa mwandishi wa habari hizi, Mjumbe katika serikali ya kijiji na Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi katika shule ya msingi Burungu Dickson Samson alisema, kati ya mifuko 60 iliyotolewa na Mbunge, tayari mifuko minane imetumika katika jengo hilo.

“Kwa taarifa tulizopewa na fundi inaonyesha mifuko inayohitajika kukamilisha zoezi lote hilo ni kati ya 40 hadi 42, hivyo hakuna upungufu katika ukamilishaji wa chumba hicho” alisema Samson.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kukema Makunja Makunja alisema, mbali na ukamilishaji wa chumba hicho kimoja, lakini bado wananchi hao wanajituma kuchangia ili kupata fedha za kununua mbao na mabati ya kuezekea chumba kingine kimoja kilichobaki pamoja na kupata saruji kwa ajili ya umaliziaji wa chumba hicho kilichobakia.

“Wananchi kwakweli wanajituma kuchangia fedha ili kununua mabati pamoja na mbao kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba kimoja kilichobakia na hata kukidhi mahitaji ya vyumba kwenye shule yetu” alieleza Makunja.

Naye Magda Biseko kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Bukumi alitoa shukrani kwa Mbunge wao Prof. Muhongo kwa mchango mkubwa anaoutoa katika taasisi mbalimbali na kusema, wananchi wataendelea kupambana kuhakikisha kila kinachotoka kwa Mbunge kinafanya kazi inayoonekana.

Aidha Magda alitoa ombi kwa serikali, Mbunge na wadau mbalimbali kuendelea kutoa michango yao ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu vijijini, kwani wananchi pamoja na hali ngumu bado wapo pamoja nao na wanawaunga mkono ili kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyobakia shuleni hapo.

“Tunamshukuru sana Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa michango mingi anayoitoa, lakini pia tuwaombe serikali, wadau mbalimbali na Mbunge wetu waendelee na moyo huo wa kujitolea ili tuzitatue changamoto katika sekta muhimu ya elimu” alishukuru na kuomba Magda.

 KIKUNDI CHA ANGAZA WAKARIBIA KUVUNA MABOGA YA KISASA

Na. Ramadhani Juma

KIKUNDI cha Angaza kilichopo kijiji cha Buraga kata ya Bukumi, kinakaribia msimu wa mavuno ukiwa ni msimu watano tangu wakabidhiwe mashine ya umwagiliaji na Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo.

Kikundi hicho ambacho ni moja kati ya vikundi 15 vilivyonufaika na mgao wa fedha za mfuko wa jimbo, kinafanya shughuli zake za kilimo kwa asilimia kubwa katika kijiji cha Bukumi kutokana na wanachama wake wengi kumiliki mashamba yao katika eneo la Bukumi.

Mtunza hazina wa kikundi hicho Pius Makuke alisema, kikundi chao kipo katika hatua za mwisho kuelekea mavuno ambapo walipanda maboga aina ya Pop Vriend Vegetable (PV) na wanatarajia kuvuna ndani ya mwezi huu.

“Hili ni zao jipya kulimwa katika ukanda wa Musoma, linapendwa sana na watu wengi na hutumiwa na jamii kwa chakula na mboga katika hoteli kubwa za mijini na vijijini na hata jamii nyingi za vijijini” alisema Makuke.

Makuke aliendelea kusema: “pia zao hili ni la muda mfupi linalochukuwa kipindi cha miezi mitatu kutoka kupandwa hadi kuvunwa, hivyo nawaomba wananchi wengi wa maeneo ya karibu kujitokeza kununua maboga kabla ya kuingizwa sokoni ili wajiridhishe na uzuri wa zao hili na wao ndio watakuwa mabalozi kwa hilo.”

Aidha, Makuke aliongeza kuwa, Kikundi cha Angaza kina mpango wa kujenga matanki mawili kwa ajili ya kuvuna maji kutoka ziwani kwa lengo la kuanzisha mradi wa umwagiliaji utakaotumiwa katika kilimo cha mahindi katika mashamba yao.

“Pamoja na zao la maboga, matango na mchicha tuliyonayo kwa sasa shambani, kikundi chetu kina mpango wa kupanua miradi ya kilimo kwani tunatarajia kuanza ujenzi wa matanki mawili kwa ajili ya kuvuna maji kutoka ziwani na kuyatumia katika kilimo cha umwagiliaji cha zao la Mahindi” alisema Makuke.

Kwa upande wake mwanachama wa kikundi hicho, Atoti Malelema alimshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kwa kuwatambua vijana na kuwawezesha katika kuwapatia mashine kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, hivyo kazi iliyobakia ni wao kupambana kufa na kupo na kuhakikisha wanazalisha kwa wingi kwa faida ya jamiii inayotegemea mavuno kutoka kwenye mashamba ya kikundi chao.

Malelema alitoa wito kwa vijana ambao bado wana tabia za kupoteza muda mwingi vijiweni kwa kujadili mambo yasiyo na faida kwao, wajitokeze na kujiunga kwenye vikundi ili watumie nguvu zao kulea familia zinazowategemea.

“Tunawaomba wale vijana wengi ambao hawajaingia kwenye vikundi wajaribu hata kutusogelea sisi waone kazi tunayoifanya kuliko kukaa vijiweni na kuhangaika hangaika pasipo na sababu yoyote…” alisema Malelema.

KIRIBA WAENDELEA NA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Kiriba.

Na. Mwandishi Wetu

WANANCHI wa kijiji cha Kiriba wameendelea na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Kiriba baada ya zoezi hilo kusimama kwa muda wa mwezi mmoja.

Zoezi hilo limeendekea tena baada ya kikao cha wananchi na viongozi wa kijiji hicho kilichofanyika 1, Julai mwaka huu na kuazimia kufanya ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kuwalipa mafundi wanaojenga vyumba hivyo.

Akiongea na viongozi wa kijiji hicho baada ya kufanya zoezi la ukaguzi wa ujenzi huo, msaidizi wa Mbunge Ramadhani Juma, amewahimiza viongozi hao kusimamia zoezi hilo kwa umakini na kwa kasi ili liweze kukamilika kwa muda mwafaka.

“Naomba mjitahidi kuongeza kasi katika ujenzi huu, ninyi ni miongoni mwa vijiji vilivyopokea saruji mapema kwa ajili ya ujenzi, lakini hadi sasa bado mnasuasua wakati vijiji vingine vimekwisha kamilisha ujenzi huo, ifikapo mwishoni mwa mwezi wa saba ikiwa hamjamaliza ujenzi tutawanyang’anya saruji na kuipeleka maeneo yanayoendana na kasi” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa kijiji hicho Semeni Mahuta alimwakikishia msaidizi wa Mbunge kuwa ifikapo mwisho wa mwezi wa saba, jengo hilo litakuwa limekamilika,

“Napenda kukuthibitishia kwamba, kwa sasa tumekusanya michango kutoka kwa wananchi, hivyo hatuna budi kukamilisha ujenzi huo kwani fedha tunazo za kutosha, nakuomba utufikishie salamu zetu kwa Mbunge kwamba tuko nyuma yake katika kuliletea maendeleo Jimbo la Musoma Vijijini” alisema Mahuta.

Kijiji cha Kiriba kilipokea jumla ya mifuko ya saruji 120 kutoka Ofisi ya Mbunge kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbili ambazo ni Kiriba “A” na Kiriba “B”.

SHULE YA MSINGI KURUKEREGE WAPOKEA MILIONI 10

Mwonekano mpya wa shule ya Msingi Kurukerege baada ya ujenzi wake kumalizika.

Na. Juma Shabani

UONGOZI wa kijiji cha Kurukerege kata ya Nyegina umepokea shilingi milioni 10 kutoka Halmashauri ya Musoma vijiji kwa ajili ya kupauwa vyumba vinne vya madarasa ambao ujenzi wake unaendelea.

Fedha hizo ni sehemu ya mpango wa Halmashauri kutoa mchango kwa ajili ya zoezi la kupauwa vyumba vya madarasa linaloendelea kwa baadhi ya shule na zahanati zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza kijijini hapo diwani wa kata ya Nyegina Majira Mchele, alikiri kupokea fedha hizo kwa ajili ya kupauwa vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya shule ya msingi Kurukerege.

“Tulikamilisha maboma ya vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu ikiwa ni nguvu ya wananchi na msaada kutoka ofisi ya mbunge wetu wa Musoma vijijini mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo, ikiwa ni saruji mifuko 60” alisema diwani Mchele.

Diwani huyo aliendelea kusema: “shule hii ya Kurukerege majengo yake yote yalikuwa yamezeeka sana na baadhi ya vyumba vingine vikiwa vinanyofoka tofali sehemu za madirisha na milango maana havikuwa na milango wala madirisha na kushindwa kutambua mlango ni upi na dirisha ni lipi, hivyo viliendelea kuchakaa kwa kasi sana” alisema diwani huyo.

“Lakini wananchi walianza kuchangia michango kidogo kwa ajili ya kuanza kujenga vyumba vingine tulianza taratibu sana kutokana na hali ya kipato kwa wananchi”

Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Kurukerege Song’ora Bita, alianza kwa kutoa shukrani zake kwa wananchi na viongozi wote wa kijiji hicho na kwa Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini kwa kukamilisha ujenzi huu wa vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Mwenyekiti huyo alisema, walianza kujenga vyumba viwili vya madarasa kwa nguvu za wananchi baada ya kukamilika kwa sababu hawakuwa na ofisi nzuri ya walimu, walikuwa na chumba kimoja ambacho walikuwa wanakitumia kama ofisi ya walimu na ofisi ya Mwalimu Mkuu.

“Mwaka jana tulianza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa tukiwa tunajikongoja kwa michango ya wananchi, mara ghafla tulipokea saruji mifuko 60 kutoka ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini, tulipata nguvu kabisa ya kukamilisha maboma ya vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja” alisema Bita.

Mwenyekiti Bita alisema, baada ya maboma kukamilika walikuwa miongoni mwa shule zilizopewa fedha kutoka Halmashauri kwa ajili ya kupauwa, walikamilisha vyumba hivyo baada ya hapo walifanya mkutano mkuu wa kijiji na wananchi kukubali kuchangia kwa ajili ya kuweka majengo hayo kuwa ya kisasa.

“Tulipiga ripu ndani na nje, tukapaka rangi majengo yote yaliyo na jumla ya vyumba sita na ofisi mbili na stoo pia milango na madirisha kwa vyumba hivyo vyote. Nitaendelea kutoa shukrani tu kwa viongozi wote na wananchi wote wa kijiji changu kwa kweli shule imependeza sana na inavutia, nina imani kuwa hata ufaulu wa wanafunzi utaongezeka kwa kiasi kikubwa sana maana walimu wanakaa sehemu nzuri, hivyo watakuwa wanaandaa kazi zao vizuri kabisa” alisema mwenyekiti Song’ora Bita.

VIKUNDI VYA BUSTANI KUPANUA MIRADI YA KILIMO MUSOMA VIJIJINI

Baadhi ya wanakikundi wakijaza maji kwenye sehemu maalumu za kuhifadhia maji ili kupunguza gharama za mafuta ya kusukuma maji kwa kutumia jenereta.

 Na. Fedson Masawa

VIKUNDI vya kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda ambavyo vilinufaika na mgao wa fedha za mfuko wa Jimbo la Musoma vijijini, vimefikia uamuzi wa kupanua miradi yao kutoka kwenye kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda na kufikia hatua ya kilimo cha mahindi ambacho kitakuwa cha umwagiliaji.

Hatua hiyo imewekwa wazi na Gudrack Wambwe, Mwenyekiti wa kikundi cha No Sweat No Sweet cha Bugunda, wakati wa ziara ya msaidizi wa mbunge aliyetembelea kikundi hicho kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya kilimo cha Bustani na matumizi ya mashine waliyokabidhiwa.

Wambwe alisema, kuna umuhimu wa vikundi vyote vilivyokabidhiwa mashine za umwagiliaji kuzitumia katika maeneo yao ili kuzalisha mazao ya chakula kwaajili ya kukabiliana na tatizo la njaa.

Mwenyekiti huyo alisema, vikundi vyote pamoja na kwamba vinashughulika kwa kiasi kikubwa na ulimaji wa mbogamboga na matunda yakiwa ni mazao ya biashara, ni muda muafaka sasa wa kuliona suala la kilimo cha mazao ya chakula kuwa ni muhimu, kwani itakuwa hamasa ya pekee endapo wao wakianza na kuzalisha kwa wingi basi jamii nzima itahamasika na kuanza kujishughulisha na kilimo hicho tofauti na kusubiri mvua ambayo ni ya msimu.

“Kama wanavikundi wenzangu wasingejali sana, basi ningeomba vikundi vyote tuliokabidhiwa mashine tuanzishe pia kilimo cha mahindi. Kufanya hivyo kutasaidia kuhamasisha jamii zetu kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwaajili ya kuzalisha mazao ya chakula tofauti na kutegemea mvua za msimu” alisema Wambwe.

Wambwe alisema, wakulima ambao wanaishi kandokando ya Ziwa Victoria, kwenye maji ya kutosha na wana maeneo ya wastani yanayoweza kuzalisha chakula hicho kwa wingi tena kwa muda mfupi, wanapaswa kutumia vizuri fursa hiyo na kuacha kutegemea mvua ya kusuasua.

Akizungumzia hali halisi ya bustani yao kwa sasa, Wambwe alisema tangu waanze kutumia mashine katika kilimo hicho, haijawahi kutokea kushuhudia mavuno kama wanayotarajia kuvuna katika msimu huu.

“Kusema kweli tangu tuanze kulima kwa kutumia mashine hii, haijawahi kutokea tunatarajia kuvuna mavuno kama tunayotegemea kuyapata kwa kipindi hiki, bustani ni nzuri na tunatarajia kuvuna mavuno ya uhakika mapema ifikapo Julai 20, 2017” alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa kilimo wa kata ya Bwasi Hassan Magili alisema, kikundi hicho kinafanya kazi kwa kujituma japo kuna changamoto ndogondgo za ukosefu wa madawa sahihi yanayoweza kukabiliana na magonjwa tofauti  yanayoibuka kila kukicha.

“Mbali na ukosefu wa madawa, tuna tatizo la ukosefu wa soko, hivyo kwa sasa ingekuwa ni jambo jema kama tungepatiwa soko la uhakiki kwa ajili ya kuuza mazao yetu kwa bei nzuri” alisema Hassan Magili.

WANANCHI KANDEREMA WAITIKIA WITO WA MBUNGE    

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kanderema wakiwajibika na maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Na. Hamisa Gamba

SIKU chache baada ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuwataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha vifaa vya ujenzi wanavyopelekewa vinafanyiwa kazi haraka, wananchi wa kijiji cha Kanderema wamejenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu wa shule ya msingi Bugoji.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wananchi hao walisema, wameamua kutekeleza ujenzi huo ili kuepuka vifaa walivyopelekewa na mbunge wao ikiwemo saruji na mabati kuhamishiwa kwenye maeneo mengine.

Wakati akitoa tamko hilo, Prof. Muhongo alisema, iwapo wananchi wa eneo lolote ndani ya jimbo watawezeshwa vifaa vya ujenzi, na eneo hilo likashindwa kuvitumia vifaa hivyo, Mkuu wa wilaya ana haki ya kuhamisha vifaa hivyo na kuvipeleka sehemu nyingine walio tayari kufanya maendeleo.

“Kwa kweli sio jambo zuri ikatokea vifaa hivi vikachukuliwa na kupelekwa kwingine, ni aibu na ni jambo ambalo halina faida kwa watoto wetu wanaosomea chini ya mti, kwahiyo tunajitahidi kuhakikisha tunajenga madarasa ili kuwaondolea watoto wetu adha ya kusoma nje kwasababu ya ukosefu wa madarasa” alisema Hamis Mwenura, Mwenyekiti wa kijiji cha Kanderema.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Abiud Magesa alisema, licha ya hatua waliyopiga ya kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, lakini changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa maji hivyo kuchelewesha kazi yao.

“Hii haitatufanya tushindwe kutumia fursa tunazopewa na viongozi wetu, tutatumia hata maji yetu ya kunywa kuhakikisha jengo hili linakamilika” alisema Magesa.

 

 KIJIJI CHA ETARO WAANZA UJENZI WA VYUMBA VITANO VYA MADARASA

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa msingi wa jengo la shule ya msingi Etaro, kushoto ni mtendaji wa kijiji Sophia Charles, wengine wanaoonekana kwenye picha ni wajumbe wa kamati ya shule waliofika kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Na. Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Etaro wameanza ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi moja ya shule ya msingi Etaro ikiwa ni mradi unaotekelezwa kwa nguvu za wananchi, serikali ya kijiji na mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo.

Mtendaji wa kijiji hicho Sophia Charles, akizungumza kwenye eneo la ujenzi huo alisema, mradi huo umeanza baada ya kupatikana saruji na fedha taslimu kwa ajili ya kuwalipa mafundi, fedha zinazotokana na mapato mbalimbali ndani ya kijiji hicho.

“Wananchi wamejitolea kiasi cha fedha na nyingine tumezipata kutoka kwenye vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya kijiji chetu, lengo kubwa ni kujenga vyumba vitano vya madarasa na tayari mafundi wameshaanza kujenga msingi kwa kasi” alisema mtendaji Sophia.

Mtendaji huyo aliendelea kusema: “nina imani kuwa ujenzi utakamilika muda si mrefu, nawapongeza sana wananchi kwa juhudi zao kubwa wanazozionyesha katika kazi hii maana wamekuwa wakijitolea kusogeza mawe, mchanga na maji sehemu ya kazi” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo Patrick Makoba, alitoa shukrani kwa Prof. Muhongo na kwa wananchi wote wa kijiji cha Etaro kwa jinsi walivyoshiriki katika zoezi hilo la ujenzi wa msingi.

“Tunashukuru sana ofisi ya mbunge wetu kwa kutupatia mifuko 60 ya saruji na sisi tunasema, lazima tuhakikishe tunamuunga mkono kwa hali na mali mbunge kwa juhudi zake anazotuonyesha jimboni kwetu” alisema Makoba na kuongeza kuwa, katika shule hiyo ya Etaro walikuwa na vyumba saba vya madarasa na wanafunzi zaidi ya elfu moja, hivyo changamoto ilikuwa kubwa sana ilibidi wanafunzi kusoma kwa kubadilishana asubuhi na jioni hali ambayo ilisababisha utoro kwa wanafunzi wengi.

Aidha, Makoba alisema baada ya kuona changamoto hizo ilibidi wakae na wazazi na wadau wengine kutoka kijijini hapo na kuwaeleza changamoto hiyo na ilipokelewa vizuri na ikafanyika hamasa iliyochangia kuanza kwa ujenzi huo wa vyumba vitano vya madarasa.

“Sisi kamati ya shule na kushirikiana na serikali ya kijiji kazi yetu ni kuhakikisha tunasimamia vizuri ujenzi huu na baada ya haya maboma kuwa yamekamilika, tutaanza msingi mwingine wa vyumba vitatu na tutahakikisha tunasimamisha maboma tena ya vyumba vitatu” alisema Patrick Makoba.

KWIBARA WAELEKEA KUKAMILISHA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA

Mafundi wakiwa katika hatua za ukamilishaji wa jengo la shule ya msingi Kwibara “B.”

Na. Mwandishi wetu

WANANCHI wa kijiji cha Kwibara wamefikia hatua nzuri katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Kwibara “B”,

Hayo yamedhihirika baada ya ziara ya Msaidizi wa mbunge Ramadhan Juma wakati akikagua ujenzi wa madarasa katika shule hiyo na kuwapongeza wananchi hao kwa juhudi zao katika kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.

“Nimeziona juhudi zenu, hakika zinaleta matumaini kwa vijana wetu wanaosomea nje, mnachotakiwa ni kutokata tamaa katika mapambano dhidi ya maendeleo, mnahitaji kuongeza juhudi maradufu ili kuondoa tatizo la watoto kusomea nje” alisema Msaidizi huyo wa Mbunge.

Akiongea kwa niaba ya wananchi, Mwalimu mkuu wa shule hiyo Meja Juma, alimpongeza Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa jinsi alivyolivalia njuga suala la ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Hakika Musoma vijijini tuna kila sababu ya kujivuna kwa kumpata Mbunge mpenda maendeleo, juhudi zake za kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika jimbo letu linaelekea kumalizika muda si mrefu, hivyo tuna kila sababu ya kumpa ushirikiano” alisema mwalimu Meja.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mugango Irene Mathias, alimshukuru Mbunge kwa juhudi zake na kumuomba awe na moyo wa uvumilivu kutokana na misukosuko aliyoipata.

“Tunatambua juhudi, weledi na tabia za Mbunge wetu, anachukia rushwa kama ukoma, hivyo tuna imani kutenguliwa nafasi yake ya uwaziri siyo kwa sababu anahusika na michezo michafu ya rushwa, hata kwenye vitabu vya Mungu wapo manabii walikufa kwa sababu ya dhambi za wenzao, hivyo asikate tamaa kuwatumikia wapiga kura wake na watanzania kwa ujumla. Mungu atamwonyesha njia iliyojaa baraka na matunda mazuri kuliko hiyo ya mwanzo aliyoipita” alisema Irene.

Shule ya msingi Kwibara “B” ni miongoni mwa shule tatu za kijiji cha Kwibara zilizopata msaada wa vifaa vya ujenzi kutoka ofisi ya Mbunge, shule nyingine ni Mugango sekondari na shule ya msingi Mugane. Jumla ya mifuko ya saruji 190, mabati 162 na mbao 210 zilitolewa na ofisi ya mbunge kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kijiji hicho.

Hata hivyo, wananchi wa kijiji hicho wameendelea kutoa kilio chao kwa Msaidizi wa Mbunge ili akifikishe kwa Mbunge awasaidie mabati 54 kwa ajili ya kukamilisha chumba cha pili.

Naye msaidizi wa Mbunge aliwahakikishia wananchi hao kuwa, ombi lao litafika kwa mbunge, lakini aliwaomba wananchi wasiwe wazito kuchangia shughuli za maendeleo kwani kwa sasa hali ya chakula inaridhisha kwani ndilo lilikuwa kikwazo kwa maendeleo.

VIJANA CHUMWI WAHAMASISHWA KULIMA KABICHI   

Mmoja wa viongozi wa kikundi cha Tujitume kilichopo kijiji cha Chumwi, Matekele Mjarifu (kushoto) akiondoa maotea kwenye shamba la kabichi linalomilikiwa na kikundi hicho, kulia kwake ni Mtendaji wa kijiji John Rugumu akisaidia zoezi hilo.

Na. Verdiana Mgoma

KIONGOZI wa Kikundi cha Tujitume kilichopo kijiji cha Chumwi, kata ya Nyamlandirira Matekele Mjarifu amewataka vijana wa kijiji hicho na mengine ya jimbo la Musoma vijijini kujitokeza kwa wingi kulima kabichi.

Mjarifu alisema, baada ya kuhudhuria semina nyingi za kilimo na kujifunza vitu vingi, ameona kilimo hicho ni fursa pekee inayoweza kuwapatia vijana ajira na kuwaondoa kwenye umaskini.

“Naamini naweza kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa na kupata mtaji wa kutosha kwa kulima kilimo cha kabichi kwa njia ya umwagiliaji. Mimi na kundi langu tumejipanga vizuri na tunahitaji kuwa mawakala wazuri jimboni kwetu hasa kwa vijana wenzetu wale wanaotegemea zaidi ajira, nawajulisha kuwa kilimo ni ajira ya kujitosheleza” alisema Mjarifu.

Mtendaji wa kijiji cha chumwi Muswaga Hitla, amewapongeza vijana wa kijiji hicho kwa kufanya jitihada kwenye suala la kilimo tofauti na ilivyokuwa awali ambapo hapakuwa na mwamko.

“Viongozi wanaendelea kuhamasisha kwa kutengeneza vikundi  tofauti vya vijana ambao watasaidia kukuza uchumi kwa njia tofauti” alisema Hitla na kuongeza kuwa, hivisasa wana vikundi tofauti ambavyo vina jishughulisha na  kilimo, ufugaji na sanaa.

“Japo hatujaimarika vizuri kutokana na upungufu wa vitendea kazi (kama mashine na madawa), mtaji, masoko na wahamasishaji watakao tuinua zaidi kielimu, lakini bado  tuna imani tukivipata hivi tutafanikiwa zaidi” alisema mtendaji huyo.

Naye Afisa kilimo wa kata ya Nyamrandirira Eliakimu Mwanga akizungumzia kilimo hicho alisema, hulimwa zaidi kwenye hali ya baridi, mwinuko na udongo wenye rutuba nyingi, usiotuamisha maji na sehemu isiyo na chumvi nyingi.

Mwanga alisema, mbegu za kabichi huoteshwa kwenye kitalu na baadaye kuhamishiwa shambani, kabichi hukomaa katika siku 60 mpaka 210 tangu kupandikizwa kwa miche na ukomaaji wake hutegemea na aina ya kabichi.

“Kabichi ni aina ya mbogamboga ambayo inatunga majani yake kwa kujiviringisha na kutengeneza mduara. Mboga hii huliwa bila kupikwa au kuchemshwa, hutumika kutengeneza kachumbari, pia inaweza kupikwa na kuchanganywa na vyakula kama nyama na maharage. Kabichi ni nzuri kwa afya pia ina vitamin K na C” alisema Eliakimu Mwanga.

 UJENZI WA VYUMBA 10 VYA MADARASA WAANZA RASMI SHULE YA MSINGI BWASI

Na. Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Bwasi wameanza rasmi ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule ya msingi Bwasi “B” iliyopo katika kijiji cha Bwasi.

Ujenzi huo ni ufadhili wa Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo aliyetoa mifuko 60 ya saruji na kuwaomba wananchi wa kijiji hicho kushirikiana kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Akizungumzia ujenzi huo wa vyumba 10 katika shule ya msingi Bwasi “B”, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Bwasi Maregesi Mbogora alisema, wananchi wa kijiji chake kwa kipindi hiki wana moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi katika maendeleo, hivyo anawapongeza kwa hilo na anaamini zoezi la ujenzi huu litaenda kwa kasi zaidi.

Mbogora alisema, kutokana na moyo wa kupenda maendeleo kwa watu wa jimbo lake, Prof. Muhongo atapewa ushirikiano mkubwa na wananchi wa Bwasi pamoja na uongozi wote wa kijiji na kukitumia kila kitu anachokielekeza kwenye kijiji hicho katika matumizi sahihi.

“Wananchi wangu wapo tayari kupambana katika maendeleo kwa moyo mmoja kwani wanajituma, wanafanya kazi kwa pamoja, ninawashukuru kwa hilo. Lakini pia tupo tayari kumpa ushirikiano mkubwa mbunge wetu kwa kila kitu atakachokitoa kwenye kijiji chetu cha Bwasi” alisema na kushukuru Mbogora.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, Diwani wa kata ya Bwasi Masatu Nyaonge alisema, pamoja na hali ngumu waliyonayo wananchi wa kata yake, lakini bado hawakati tamaa na anahakikisha kasi waliyoanza nayo wananchi wa kijiji cha Bwasi inaweza kuwa zaidi ya kasi ya wananchi wa kijiji cha Kome endapo vitendea kazi vitakuwepo vya kutosha.

“Japo wananchi wa kata yangu wana misukosuko ya hali ngumu ya ukosefu wa mvua ya kutosha kwa ajili ya kilimo, bado wana ari  ya kufanya maendeleo kwa kasi. Nina hakika hao wananchi wa Bwasi kwa kasi waliyokuja nayo wanaweza kuwa zaidi ya wale wa Kome” alisema diwani Nyaonge.

Naye Ernest Kamese ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Buruma na msimamizi mkuu wa shughuli za ujenzi, amemshukuru mbunge wao Prof. Muhongo kwa msaada mkubwa anaoutoa hasa baada ya kubaini upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na mchango wake katika sekta ya afya.

Kamese alisema, licha ya hatua waliyofikia, changamoto itakayowakabili kwa siku za usoni ni upungufu wa mifuko ya saruji, lakini kasi wanayokwenda nayo ni nzuri na iwapo changamoto hiyo itatatuliwa, watakamilisha kazi hiyo mapema.

Hadisasa akiwa katika harakati za kupambana na uhaba wa vyumba vya madarasa jimboni mwake, Prof. Muhongo amechangia mifuko ya saruji katika shule mbalimbali za msingi na sekondari za jimbo la Musoma vijijini.

Miongoni mwa shule alizochangia ni pamoja na shule ya msingi Kome “B” kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 ambapo tayari vyumba 7 vimekwisha kukamilika, shule ya msingi Bulinga “B”, shule ya msingi Kurugongo “B” na shule nyingine nyingi za Musoma vijijini.

HALMASHAURI YATOA MILIONI 20 KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI NYEGINA

Mafundi wakipandisha kechi kwa ajili ya kupaua jengo jipya la zahanati ya Nyegina.

Na. Juma Shabani

HALMASHAURI ya Musoma vijijini imetoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya zoezi la upauwaji wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyegina inayokabiliwa na uhaba wa wodi za wagonjwa.

Diwani wa Kata ya Nyegina Majira Mchele, amethibitisha kupokea fedha hizo na kuongeza kuwa, wananchi walikamilisha ujenzi muda mrefu, lakini walishindwa kuendelea kutokana na kukosa fedha za kununulia vifaa vya upauwaji.

“Gharama zilikuwa kubwa sana, lakini tunashukuru Halmashauri kuweka mpango huu wa kupauwa jengo hili” alisema diwani Mchele.

Mtendaji wa kijiji cha Nyegina Josephat Maguya, naye alikiri kupokewa kwa fedha hizo na zoezi la kupaua linaendelea kwa kasi baada ya kununua mbao na bati bando 29.

“Baada ya kumaliza kupauwa jengo hili, nitakaa na serikali ya kijiji kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuendelea kupiga ripu, sakafu, milango na madirisha” alisema mtendaji huyo.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Judith Athony alisema, akinamama wamekuwa wakipata tabu kwa muda mrefu hasa baada ya kujifungua, kwani zahanati hiyo haina wodi za kutosha kulaza wagonjwa.

Judith alisema, akinamama wanapojifungua wanalazimika kurudi nyumbani, lakini sasa wana matumaini makubwa ya kupata huduma nzuri na za uhakika baada ya kukamilika kwa jengo hilo.

“Hiki tunachokiona kinaendelea katika kijiji chetu tunapata matumaini makubwa kuwa, tutapata zahanati nzuri na kubwa na akinamama wakijifungua watapata huduma nzuri wao na watoto wao tofauti na mwanzo” alisema Judith Antony.

 

BUSEKERA WAKAMILISHA UJENZI WA VYUMBA VINNE VYA MADARASA

Na. Fedson Masawa

SERIKALI ya kijiji cha Busekera kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili ambavyo vimekamilisha vyumba vinne vya madarasa.

Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Busekera Andrea Mwisira, alisema kila mwananchi wa kijiji hicho anawaza ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Busekera, kitu ambacho kinawapa wepesi wa kufanikisha zoezi hilo.

Mwisira aliongeza kuwa, mshikamano wao na moyo wa kujali vifaa vinavyotolewa na mbunge wao ndio unawapa msukumo wa wao kujituma kusimamia na kutekeleza majukumu na mipango ya kijiji na jimbo zima.

“Kilichotufikisha katika hatua hii ni mshikamano na moyo wa kujituma kwa wananchi wa kijiji cha Busekera, lakini pia wananchi wanaonekana kujali sana mchango wa mbunge anaoutoa kwenye kijiji chetu ndio maana kasi yote hii inakuwa yenye mafanikio kwenye kijiji hiki” alisema Mwisira.

Aidha, Mwenyekiti wa kijiji cha Busekera Zakayo Mayuya alisema, kwa utaratibu wanaokwenda nao wananchi na viongozi wa kijiji cha Busekera, kwa sasa wanasubiri mifuko mingine ya saruji kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa vyumba vingine vilivyosalia ili kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

“Tukishapata mifuko ya saruji iwe kesho au kesho kutwa sisi tunaanza kazi. Hapa sasa tunapumua, lakini bado tunajua tuna deni kwenye vyumba vilivyosalia, sasa tunasubiri mzigo ufike sisi tuendelee. Lakini pia mimi na serikali yangu tumejipanga kumuunga mkono mbunge wetu na kwa maendeleo haya hatutarajii kumuangusha kabisa” alisema Zakayo.

Naye Diwani wa kata ya Bukumi John Kurwijira ameeleza wazi kuwa, kwa mchango wa saruji kutoka kwa mbunge ulioelekezwa kwenye shule za kata yake, tayari umetumika kikamilifu bila wasiwasi wowote.

Kurwijira alizitaja shule zilizopokea msaada wa saruji kwenye kata yake kuwa ni shule ya msingi Busekera, Buira na Burungu ambazo zilipewa mifuko 60 kila shule na tayari mifuko hiyo imetumika kwa matumizi sahihi.

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Busekera Dorika Tongora, ameomba kuongezewa saruji nyingine ili aweze kukamilisha ujenzi wa madarasa na kumkaribisha mbunge kufika kuangalia kazi inayoendelea kufanywa na wananchi wa kijiji cha Busekera.

“Ombi langu kwenye ofisi ya Mheshimiwa Mbunge; nahitaji kama ratiba zake mbunge zikiwa vizuri, basi afike Busekera aone nguvu ya wananchi kwa kile anachokitoa na pia kama vifaa vikifika basi tupo tayari kuvipokea haraka sana” aliomba Mtendaji huyo.

Ujenzi huu upo kwenye mpango wa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuhakikisha anakabiliana na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa, ambapo amechangia mifuko 60 ya saruji na mabati 54 yaliyoezeka moja ya vyumba hivyo vinne katika shule hiyo ya msingi Busekera.

 

MKIRIRA WAANZA UBORESHAJI WA VYUMBA VYA MADARASA

Mafundi wakiendelea na shughuli za upigaji wa ripu na sakafu kwa vyumba vinne vya madarasa ya shule ya sekondari Mkirira.

Na. Mwandishi Wetu

UONGOZI wa shule ya sekondari Mkirira wameanza uboreshaji wa vyumba vinne vya madarasa baada ya kupokea shilingi milioni nne kutoka Halmashauri ya Musoma vijijini.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo James Chacha, alisema mara baada ya kupokea fedha hizo wameanza mara moja kupiga ripu, kuweka sakafu na kuweka madirisha na milango ya vyumba hivyo.

“Tunashukuru shughuli zote za uboreshaji wa vyumba hivyo tunaendelea vizuri kabisa, mafundi kwa kweli wanaendelea kwa kasi sana, maana tayari chumba kimoja kimeshakamilika na wanaendelea na chumba kingine” alisema mwalimu Chacha.

Aidha, mwalimu Chacha alimshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kutoa huduma ya magari kwa ajili ya kukusanya vifaa na kufikisha kwenye eneo la ujenzi huo.

“Tunamshukuru sana kiongozi wetu kwa huduma hii ya magari, yanatusaidia kwa kiasi kikubwa kwa kusogezea vifaa vya ujenzi kama mawe, mchanga na kokoto, hivyo kutupunguzia gharama kubwa katika usogezaji wa vifaa vya ujenzi” alisema Chacha.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Mkirira, Erick Manyama akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, wanafurahishwa na ujenzi huo unaoendelea na wanapata faraja ya kuona ndoto zao za kusoma kwenye mazingira mazuri inaelekea kutimia.

“Tumekuwa tukisomea kwenye vyumba vyenye vumbi sana, hivyo maradhi ya mara kwa mara kama kikohozi na mafua yamekuwa yakitusumbua, pia nguo zetu zinachafuka na kuchakaa haraka kutokana na kukaa chini” alisema Erick.

Mwanafunzi huyo alimshukuru Prof. Sospeter Muhongo kwa kuwapeleka vitabu vya kutosha ambavyo vinawasaidia kwenye masomo yao.

“Kwa miaka ya nyuma hatukuwa na vitabu kabisa, lakini baada ya Muhongo kuwa mbunge wa jimbo letu, tumesahau kabisa kilio cha upungufu wa vitabu shuleni hapa, hivyo tunashukuru sana na aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wa jimbo lake” alisema Erick Manyama.

Kwa upande wake Msaidizi wa mbunge Juma Shabani, akizungumza na wanafunzi hao aliwahakikishia kwamba tatizo la vitabu halipo tena jimboni humo, huku akiwapa taarifa kwamba tayari kuna vitabu vimewasili na vimehifadhiwa kwenye stoo na muda ukifika vitasambazwa kwenye shule mbalimbali.

UJENZI WA NYUMBA ZA WAUGUZI MURANGI WAKAMILIKA

Mafundi wakimalizia upakaji wa rangi katika nyumba ya wafanyakazi kituo cha afya Murangi.

Na. Verdiana Mgoma

ZOEZI la ukarabati na upanuzi wa kituo cha afya cha Murangi umekamilika na utakabidhiwa wakati wowote kuanzia sasa.

Akizungumzia kukamilika kwa ujenzi huo, mkandarasi  Coelestina Kato alisema, gharama za mradi ni shilingi 163, 136, 180, ambazo zimejenga nyumba ya wafanyakazi yenye uwezo wa kuishi wafanyakazi wawili, choo cha wagonjwa chenye jumla ya matundu manne, ujenzi wa plasenta na ujenzi wa insreta.

Kato alisema, kwenye miradi hiyo minne imekamilika vyema na anatarajia kuikabidhi mapema kama mkataba unavyoelekeza kuwa ujenzi ukamilike ndani ya siku 90 (miezi mitatu).

Mtendaji wa kijiji cha Murangi, Eliakimu Jumapili alithibitisha kukamilika kwa ujenzi huo na kumshukuru mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo na Halmashauri ya Musoma Vijijini kwa kutambua umuhimu wa wauguzi na kuchukua maamuzi ya kujenga nyumba za watumishi wa afya hasa maeneo ya vijijini.

“Kwa kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizi, itasaidia kupunguza changamoto za wagonjwa wa dharura ikilinganishwa na hali iliyopo kwa sasa watumishi walio wengi wapo nje ya kituo, tunashukuru kwa hatua tuliyofikia hasa kwenye suala zima la kusimamia sekta ya afya” alisema Jumapili.

Mganga Mkuu wa kituo hicho Dkt. Naomi Muyeli alisema, kukamilika kwa mradi huo kutawasaidia kufanya kazi katika mazingira mazuri na bora tofauti na ilivyokuwa awali.

Mganga huyo alisema: “kukamilika kwa nyumba hizi kutapunguza idadi ya watumishi kukaa mbali na kituo, ujenzi wa plasenta utasaidia sana, maana hapo nyuma hatukuwa nayo kabisa pia kuongezewa matundu ya choo itasaidia kuweka mazingira ya kituo kuwa safi zaidi, hivyo shukrani za pekee kwa mbunge wa Musoma vijijini.”

Dkt. Naomi aliongeza kuwa, ndani ya mwaka mmoja wamepokea misaada mingi kutoka ofisi ya mbunge ikiwa ni pamoja na miradi waliyopokea kutoka Ubalozi wa Japani kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya, mifuko ya saruji 232 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto, mabati ya kisasa 50 kwa kuezekea wodi.

“Pia tumepokea gari kubwa ya wagonjwa, vitanda vya wagonjwa, baiskeli za wagonjwa pamoja na dawa. Tunamshukuru mbunge kwa moyo wa kujitolea tunamuhaidi kumuunga mkono kwenye sekta ya afya” alisema Dkt. Naomi Muyeli.

 

MURANGI WAPAMBANA KUKABILIANA NA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA

Mafundi na viongozi wa kijiji cha Murangi wakiwa kwenye jengo la chumba kimoja cha darasa ambao ujenzi wake unaendelea kwa kasi. Kushoto ni Mtendaji wa kijiji cha Lyasembe Vedastus Chikonya akiwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Shabani.

Na. Mwandishi Wetu

UONGOZI wa shule ya msingi Murangi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji hicho, wanaendelea na ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa unaoikabili shule hiyo.

Shule hiyo yenye wanafunzi 1,140 kutokana na wingi wa wanafunzi na uhaba wa vyumba vya madarasa uliopo, imegawanywa kuwa A na B.

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Murangi Grace Magoti alisema, mpaka sasa mahitaji ya madarasa kwa shule zote mbili ni 24 yaliyopo ni 10 na pungufu ni 14 ambapo wanaendelea kupambana kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji na mbunge ili kutatua tatizo hilo.

Mbali na hilo, mwalimu Magoti alisema wanakabiliwa na changamoto nyingine ya upungufu wa matundu ya choo, nyumba za walimu na baadhi ya vitendea kazi wakati wa ufundishaji.

Mtendaji wa kijiji cha Lyasembe Vedastus Chikonya alisema, wamejipanga kutatua tatizo la vyumba vya madarasa kwa kuwashirikisha wananchi, kamati ya shule na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ambaye tayari amechangia mifuko 60 ya saruji ambayo imesaidia kuanza ujenzi.

Kwa upande wake Mratibu elimu Kata Ruge Bernad alisema, suala la taaluma katika kata ya Murangi lipo chini kutokana na changamoto wanazo kabiliana nazo hasa kwa upande wa vyumba vya madarasa.

Mratibu huyo alisema, watoto wengi wanasomea nje kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na kuwapa wakati mgumu hasa kipindi cha mvua, hivyo wanamuunga mkono mbunge ambaye anafanya jitihada za kukabiliana na changamoto za elimu kwenye shule mbalimbali za jimbo lake.

“Tunaendelea kuwashirikisha wananchi wajue umuhimu wa elimu katika kata yao, tunamshukuru mbunge wetu kwa sasa hatuna tena changamoto kwenye upande wa  madawati, tulipokea vitabu ambavyo vimesaidia kuwainua watoto wetu” alisema.

Katika hatua nyingine, mratibu huyo wa elimu alithibitisha kupokea mifuko 150 ya saruji kutoka ofisi ya mbunge kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwa shule tatu zilizopo ndani ya kata hiyo.

“Tumepokea saruji kwa dhumuni la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kata nzima ya Murangi, tumebakiza shule moja tulichodhamiria ni kuongeza juhudi ili kuboresha sekta ya elimu” alisema Ruge Bernad.

WANANCHI WA KISIWA CHA RUKUBA MBIONI KUPATA UMEME

Wananchi wa kisiwa cha Rukuba kilichopo kata ya Etaro, wakishusha vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa kusambazia umeme ambapo inaelezwa hadi kufika mwezi Julai, zoezi la ujenzi litakuwa limekamilika na kijiji hicho kuanza kupata umeme.

Na. Juma Shabani

WANANCHI wa kisiwa cha Rukuba kata ya Etaro, wamepokea vifaa vya ujenzi kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya umeme.

Msimamizi wa mradi huo Mathias Athanas, alisema vifaa vyote vimekamilika na tayari siku ambayo vifaa hivyo vimefika, ujenzi umeanza na wanatarajia utakamilika 15, Julai, mwaka huu.

“Ujenzi wa nyumba ya mtambo utakamilika kufikia tarehe 15 mwezi wa sita, na kuanza kufunga solar pamoja na betri, baada ya hapo kufika mwezi wa saba tutaanza kusambaza nguzo na kusuka waya kwenye nyumba za wateja wetu, kufikia mwezi wa kumi mwaka huu tutawasha umeme rasmi.” alisema Mathias.

Mmoja wa wananchi wa kisiwa hicho Mwanahawa Yusufu, alisema hatua ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya mitambo ya umeme ni kitendo ambacho kimewapa matumaini makubwa ya kupata umeme utakaowasaidia kiuchumi.

“Muda si mrefu nasisi pia tutakuwa miongoni wa sehemu zilizo na umeme, umeme ulikuwa kilio kikubwa sana hapa kisiwani, nakumbuka hata wakati mbunge wetu Sospeter Muhongo alipofika hapa, suala la umeme ndo lilikuwa la kwanza kabisa katika maombi yetu” alisema Mwanahawa.

Mwanahawa aliendelea kusema: “umeme ukiwa kisiwani hapa sisi kama wafanya biashara wa vinywaji na saluni tutafanya biashara sana kwa sababu mzunguko utakuwa mkubwa maana umeme ndo kila kitu.”

Mwenyekiti wa kijiji cha Rukuba Kibhasa Kibhasa, alithibitisha kupokea vifaa hivyo na kupata matumaini ya kuongeza fursa za ajira kijijini hapo na uchumi kukua.

“Naziona fursa nyingi za ajira katika kisiwa chetu iwapo umeme utawaka, leo tu vijana wamepata kipato kwa kazi ya kuhamisha vifaa hivi kutoka ziwani hadi sehemu husika, lakini pia natumaini kuwa shughuli zote za ujenzi wa nyumba hiyo, vijana wetu watakuwa wanahusika katika shughuli hizo na hatua nyingine zitakazo fuata” alisema mwenyekiti Kibhasa.

Mbali na hilo, Mwenyekiti Kibhasa alisema umeme ukiwaka, wanatarajia kupata wawekezaji wakubwa kwenye miradi mbalimbali, hivyo maendeleo yatapatikana kwa mtu mmoja mmoja na hata kijiji kizima.

             BUSEKERA WAEZEKA CHUMBA KIMOJA CHA DARASA

Na. Fedson Masawa

SERIKALI ya kijiji cha Busekera kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho wameanza zoezi la kuezeka chumba kimoja cha darasa kati ya vyumba viwili na ofisi moja vilivyojengwa na wananchi wa kijiji hicho katika shule ya msingi Busekera.

Zoezi hilo la uezekaji ni sehemu ya muendelezo wa msaada wa Mbunge wa jimbo hilo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo aliyechangia mabati 54 na mifuko 60 ya saruji.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mtendaji wa kijiji cha Busekera Dorika Tongora alisema, baada ya kupokea mabati 54 kutoka kwa mbunge, kijiji kilichangia ununuzi wa mbao na vifaa vingine kwa ajili ya kukamilisha uezekaji wa chumba hicho.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Zakayo Mayuya, ameshukuru jitihada zinazofanywa na Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini katika kutekeleza, kusimamia na kufuatilia maendeleo ya jimbo lake na kuahidi kumuunga mkono kuhakikisha wanapambana kufa na kupona katika kumaliza tatizo sugu la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Busekera.

“Ninamshukuru sana Mbunge kwa jitihada anazozifanya kuleta maendeleo jimboni, ni mtekelezaji, mfuatiliaji na msimamizi mzuri wa maendeleo, hivyo na sisi tutapambana kuhakikisha tunamaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa hapa kwetu” alishukuru Mayuya.

Mayuya aliongeza kuwa, kijiji cha Busekera kinatambua vilivyo mchango wa Prof. Muhongo katika shule hiyo na kijiji kwa ujumla kwani mbali na kuwapatia msaada wa saruji na mabati, alitoa madawati 75 ambayo yalimaliza kabisa tatizo la upungufu wa madawati katika shule ya Busekera bila kumchangisha mzazi yeyote.

“Ukiachilia mbali msaada wa mabati 54 na mifuko 60 ya saruji, Prof. Muhongo ametuondolea upungufu wa madawati 75 hapa shuleni bila mzazi kutoa hata hela yake, tunamshukuru sana Mheshimiwa” aliongeza na kushukuru Mayuya.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Busekera, Saimon Kidili alisema Prof. Muhongo ana nia ya dhati ya kuinua kiwango cha elimu jimboni, hivyo ni lazima jamii imuunge mkono na si kumkatisha tamaa.

“Kwa hakika Prof. Muhongo anayo nia ya dhati kuinua elimu jimboni mwake, kwa hiyo jamii haina budi kumuunga mkono kwa hali na mali. Nasisi kama walimu tunatarajia kutumia vyema mazingira yanayoandaliwa shuleni kwetu na kuhakikisha wanafunzi pia wanatimiza majukumu yao ili kuleta mapinduzi katika elimu jimboni” alisema na kusisitiza Mwalimu Kidili.

SHULE YA MSINGI BUSAMBA WAANZA UJENZI WA MAKTABA

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la maktaba.

Na. Juma Shabani

UONGOZI wa shule ya msingi Busamba, wananchi kwa kushirikiana na Ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini wamefanikiwa kuanza ujenzi wa maktaba ya shule hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwalimu mkuu wa shule hiyo Mabura Emmanuel alisema, shule hiyo tangu ianzishwe haijawahi kuwa na maktaba, hivyo kila mara wamekuwa wakikosa mgao wa vitabu kutoka kwa wadau mbalimbali kutokana na kukosa sehemu ya kuviweka.

“Ni muda mrefu sana tunakosa vitabu kutoka kwa wadau mbalimbali na hata sisi tunaponunua tulikosa mahali pa kuviweka, tulilazimika kuviweka kwenye ofisi ya mwalimu mkuu, hivyo havikuwa vinadumu kwa muda mrefu” alisema mwalimu Emmanuel.

Mwalimu huyo alisema, wananchi wamehamasika kuchangia ujenzi wa jengo hilo lililojengwa kwa kiwango kizuri, huku wakipata msaada mkubwa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Busamba, Kadenge Maanya mbali na kumshukuru mbunge na wananchi kwa msaada waliotoa kufikia hatua hiyo, alisema mbali na maktaba wamefanikiwa kujenga chumba kimoja kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya awali.

“Tumekamilisha chumba kimoja cha darasa la wanafunzi wa awali ambalo hadi hivi sasa linatumika, na pili chumba cha maktaba kimefikia hatua ya kumwaga renta na mafundi bado wapo wanaendelea na zoezi la ukamilishaji wa boma” alisema mwenyekiti huyo.

Aidha, mwenyekiti Maanya alisema wakati mafundi wanaendelea kukamilisha boma hilo, yeye na viongozi wenzake wanapanga mikakati ya kutafuta michango kwa ajili ya kutafuta mbao za kuezeke jengo hilo.

“Tunaomba msaada kwa ofisi ya mbunge ili tuweze kumalizia ujenzi huu ili kwa awamu nyingine vitabu vikifika na sisi tuwe miongoni mwa shule zinazopokea vitabu, tumesha kosa vitabu mara nyingi sana kutoka sehemu mbalimbali, tumebakisha muda mchache kumalizia jengo hili” alisisitiza mwenyekiti Kadenge Maanya.

 

KASI YA KUEZEKA VYUMBA VYA MADARASA YAONGEZEKA 

Na. Mwandishi wetu

KASI ya uezekaji wa vyumba vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi na msaada wa vitendea kazi kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo imeongezeka.

Hayo yamebainishwa na msaidizi wa Mbunge Mwalimu Ramadhani Juma alipokuwa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kwikuba katika mkutano wa hadhara ambapo alisema, hadi sasa jumla ya vyumba 24 vya madarasa vimekamilika.

Mwalimu Juma alisema, hadi wanafikia hatua hiyo wamepokea msaada wa mabati 1,296 kutoka kwa mbunge na kugawanywa katika shule za msingi na sekondari.

Kwa mujibu wa Mwalimu Juma, shule za msingi zilizopata mgao huo ni; Muhoji, Rukuba, Bukwaya, Mkapa, Burungu, Bwenda, Nyasaungu, Butata, Busekera, Rwanga, Kasoma “B”, Chumwi, Kaburabura “A”, Mwiringo na Rusoli “A.”

Nyingine ni Tegeruka “B” Jitirola, Mugane, Bwai, Kambarage, huku shule za sekondari zilizonufaika na mgao huo ni Bulinga, Mugango na Mabui.

“Hadi sasa tumepiga hatua kubwa sana katika ujenzi wa madarasa, tulipoanza zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa yalikuwepo maboma 60 tu katika shule zote za msingi na sekondari, lakini kufikia Mei mosi tumefikisha maboma 205 katika shule zote za msingi na sekondari, na bado zoezi linaendelea” alifafanua msaidizi huyo.

“Tunachowaomba wananchi ni kuongeza juhudi na ushirikiano katika zoezi hili tunaloendelea nalo la ujenzi wa vyumba vya madarasa, tuna imani mkitoa ushirikiano wa kutosha kwa Mbunge zoezi hili litamalizika kwa wakati. Halmashauri yetu  inaupungufu wa vyumba vya madarasa 748, hivyo Mheshimiwa Mbunge amejitolea kupambana na changamoto hiyo kwa kutoa vifaa vya ujenzi kama saruji na mabati” alisisitiza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa Kijiji cha Kwikuba walimshukuru Mbunge kwa juhudi zake na michango yake katika maendeleo ya Jimbo hilo.

“Huyu ni Mbunge wa mfano hatujawahi kumpata Mbunge wa aina hii katika Jimbo letu tangu nchi yetu ipate Uhuru. Tuna ahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika juhudi zake za kulikomboa Jimbo” alisema ndugu Mtyama Masinde.

SHULE YA MSINGI RUKUBA WAPIGA HATUA MUHIMU KATIKA UJENZI WA MADARASA

Jengo la shule ya Msingi Rukuba likiwa kwenye hatua ya kuezekwa bati.

Na. Mwandishi Wetu

ZOEZI la kuezeka vyumba vya madarasa linaendelea kwenye shule ya msingi Rukuba kwa ushirikiano wa mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini na wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza kijijini hapo, Mwenyekiti wa kijiji cha Rukuba kibhasa Kibhasa alisema, kutokana kuwezeshwa mabati ya chumba kimoja cha darasa kutoka ofisi ya mbunge, wameanza kuezeka vyumba vingine.

Mwenyekiti huyo alisema, wananchi wamehamasika na kujitolea kuchangia na kupata bati za vyumba viwili na mbao, hivyo kukamilisha vyumba vitatu vya madarasa.

“Tulikuwa na upungufu wa vyumba vinne vya madarasa, ila kutokana na juhudi za mbunge wetu Prof. Sospeter Muhongo kujitolea kwa kutoa saruji mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo, tuliweza kukamilisha ujenzi huo wa maboma manne” alisema Kibhasa na kuongeza kuwa, kwasasa wameezeka vyumba vitatu na kimebaki chumba kimoja.

Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho, Hamza Masatu, alitoa shukrani zake kwa Prof. Muhongo, viongozi wa kijiji na wananchi kwa kujitolea kushiriki ujenzi huo na kufika hatua ya kuezeka bati.

“Zoezi lilikuwa gumu sana, lakini kwa ushirikiano wa wananchi na viongozi wenzangu tumeweza kuezeka vyumba vitatu vya madarasa, ilikuwa changamoto kubwa sana kupata mbao za kuezekea maboma haya ila nashukuru kwa hatua tuliyofikia” alisema Masatu.

Hata hivyo, Masauti alisema, bado wanaendelea na ujenzi wa nyumba mbili za walimu, nyumba moja tayari ikiwa hatua ya renta na nyingine ikiwa hatua ya madirisha.

Shule ya msingi Rukuba ni moja ya shule zilizokidhi vigezo vya upokeaji wa bati 52 kutoka ofisi ya mbunge baada ya kuwa tayari wamepata mbao za kuezeka chumba kimoja cha darasa.

 

KURUKEREGE WAKAMILISHA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA

Mafundi wakiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vya shule ya msingi Kurukerege.

Na. Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Kurukerege wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ikiwa ni hatua ya kukabiliana na upungufu wa madarasa unaoikabili shule ya msingi ya kijiji hicho.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kurukerege Erasto Masige, alisema shule yao ni moja ya shule zilizopokea mifuko ya saruji 60 kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo na wameitumia kwenye ujenzi huo.

Mwalimu Masige alisema, wananchi wa kijiji hicho wametoa ushirikiano mkubwa ambao umefanikisha kukamilika kwa ujenzi huo ambao unawapa matumaini ya kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa.

“Tuna upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa shuleni hapa ila kwa sasa tayari tumepata vyumba viwili, hivyo wale wanafunzi waliokuwa wakisomea chini ya miti basi tayari wamepata madarasa wakitoka likizo ya pasaka watafikia madarasani” alisema mwalimu Masige na kuongeza kuwa, vyumba hivyo vimejengwa kwa kiwango kizuri na tayari vimeshapigwa ripu nje na ndani na sakafu.

“Pia kuhusu madawati tayari yapo madawati ya kutosha tuliyopokea kutoka ofisi ya mbunge, hivyo hatuna upungufu wa madawati” alisema mwalimu Masige huku akimshukuru mbunge wa jimbo hilo.

Diwani wa kata Nyegina, Majira Mchele aliwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano walitoa hadi kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa.

“Ni jambo la faraja sana, watoto wetu kusomea nje ilikuwa ni tatizo kubwa ila sasa hatutakuwa na tatizo la watoto kusomea nje. Mbunge Prof. Sospeter Muhongo anajitolea kwa juhudi kubwa kutupatia vifaa vya ujenzi hivyo basi tuvitendee haki” alisema diwani Mchele.

Hata hivyo, diwani Majira Mchele aliwahimiza wananchi wake kuendelea kutoa ushirikiano ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vingine viwili ambavyo ujenzi wake umeanza.

VYUMBA VYA MADARASA VYAENDELEA KUEZEKWA

Mafundi wakiendelea na shughuli ya kupaua moja ya majengo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Bwenda.

Na Fedson Masawa

VYUMBA vya madarasa vinavyoendelea kujengwa kwa jitihada za mbunge wa jimbo Prof. Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na wananchi, vipo kwenye hatua nzuri.

Hatua hii imefikiwa kikamilifu baada ya baadhi ya shule kufikia vigezo muhimu vya kukabidhiwa mabati kwa ajili ya uezekaji wa vyumba hivyo.

Shule ya msingi Bwenda B ni moja kati ya shule ambazo zimetimiza vigezo hivyo vya kuanza ujenzi na kukabidhiwa mabati 54 kutoka ofisi ya Mbunge.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bwenda B, Grace Tambo alisema kwa sasa wanaanza zoezi la uezekaji wa chumba kimoja cha darasa kati ya vinne vilivyopo kutokana na upungufu wa mbao walionao.

Mwalimu Grace alisema, malengo yao ni kukamilisha kuezeka vyumba vyote vinne, lakini upatikanaji wa mbao ni tatizo kubwa ambalo linakwamisha ukamilikaji wa zoezi hilo na wanaendelea kupambana kwa kile kinachowezekana.

Mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Bwenda B,  Juma Biseko alianza kwa kumshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kwa mchango mkubwa anaoutoa kwa jamii nzima ya jimbo hilo na kusema kuwa, wataendelea kumuunga mkono ili kuhakikisha wanaondoa matatizo sugu katika sekta zote zinazowazunguka.

“Namshukuru Prof. Muhongo kwa juhudi zake kwani yeye ndiye anayesababisha hadi tunafikia hatua hii jimboni kwake. Na sisi tutazidi kumuunga mkono hata kwa nguvu kazi ili kuhakikisha matatizo yanayozikabili sekta zote jimboni yanakoma” alisema Biseko.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa kijiji cha Buanga Kejile Eyembe, alielezea mikakati waliyonayo ili kufanikisha uezekaji wa maboma matatu yaliyosalia.

“Mikakati tuliyonayo sasa hivi ni kupita kwa wananchi ili wachangie chochote na wafadhili watakaoguswa ili tuweze kufanikisha zoezi letu. Pia kwa sasa tayari tumenunua mbao za chumba kingine na sasa tunatafuta fedha za kumlipa fundi” alifafanua Eyembe.

 

UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA MURANGI KUKAMILIKA BAADA YA MIEZI MITATU

Untitled

Ujenzi unaoendelea wa nyumba ya wafanyakazi wa Kituo cha afya cha Murangi ambao ni sehemu ya mradi wa uboreshaji wa huduma za afya kwenye kituo hicho, mradi ambao unafadhiliwa na ubalozi wa Japan.

UPANUZI na uboreshaji wa huduma za afya kwenye kituo cha afya Murangi umeanza baada ya kupokea jumla ya shilingi milioni 170 kutoka ubalozi wa Japan.

Miradi mingine ambayo itatekelezwa kwenye kituo hicho cha afya ni ujenzi wa nyumba ya wafanyakazi (yenye uwezo wa kuishi wafanyakazi wawili), choo cha wagonjwa, sehemu ya taka (insireta) na sehemu ya kutupa taka (plasenta) ambapo gharama za mradi ni shilingi 163, 136, 180/=.

Msimamizi wa mradi huo Coelestina Kato, akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, wamekubaliana kukamilisha kazi hiyo kwa siku 90 (miezi mitatu) ingawa ameahidi kumaliza mapema zaidi kutokana na kasi waliyonayo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Murangi, Hamisi Nyamamu alisema lengo la ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa kituo cha afya Murangi ni kuwaondolea wafanyakazi adha ya ukosefu wa makazi.

“Tumekubaliana na mkandarasi kukamilisha kazi mapema, nitahakikisha nashirikiana na wananchi ili kufanikisha miradi hiyo na kuikamilisha kwa wakati” alisema Nyamamu.

Naye mganga mkuu wa kituo cha afya Murangi Dk. Naomi Muyeri alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan katika miradi inayoendelea kituoni hapo.

Dk. Naomi alisema, uwepo wa makazi kituoni hapo kutasaidia wafanyakazi wanaokaa nje ya kituo hicho kufanya kazi kwa umakini na ubunifu mkubwa hasa wanapokuwa kwenye majukumu yao huku akipongea uamuzi wa kuboresha sehemu ya kutupa taka taka ambayo awali ilikuwa haikidhi mahitaji.

WANANCHI WA KIJIJI CHA NYASAUNGU WAJENGA OFISI 

Untitled

Jengo la ofisi ya kijiji cha Nyasaungu ambalo ujenzi wake unaelekea kukamilika.

Na Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Nyasaungu kata ya Ifulifu wapo mbioni kukamilisha ujenzi wa jengo moja la ofisi ya serikali ya kijiji hicho.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Magesa Chacha, amesema ujenzi huo upo kwenye hatua nzuri na wanatarajia utakamilika wakati wowote kutokana na ushirikiano wanaopata kutoka kwa wananchi wake ambao wamejitolea kushiriki hatua mbalimbali za ujenzi huo.

“Natoa shukrani zangu kwa wananchi wa kijiji hiki kwa kujitolea kwa juhudi zao zote ikiwa ni michango ya kifedha na shughuli za usombaji wa mchanga na maji kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo hili ambalo kwa sasa limebaki kuweka sakafu, ripu, madirisha na milango ili liweze kutumika” alisema Chacha.

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema, wamejenga ofisi inayokidhi shughuli zote za kijiji ikiwa ni ukumbi wa mikutano, ofisi ya mwenyekiti, mtendaji na stoo.

“Wazo la kuanza ujenzi huu lilitokana na kero tuliyokuwa tunaipata, kwa miaka mingi tumekuwa tukikodi chumba kama ofisi ya kijiji, hivyo ilikuwa kero kubwa sana kijijini hapa ila sasa muda si mrefu tutakuwa tumetatua kero hiyo” alisema Magesa Chacha.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Joseph Marwa, aliwapongeza wananchi wenzake kwa hatua iliyofikiwa na kukubali kujinyima ili kujenga ofisi hiyo.

“Nawapongeza sana wananchi wenzangu kwa kujinyima na familia ili kuchangia ujenzi wa jengo hili la ofisi ya kijiji, maana tumekuwa tukipata tabu kumpata mwenyekiti na mtendaji pindi mtu anapopata shida, ila kwa sasa nina imani kabisa kuwa tutakuwa tukiwapata viongozi wetu kwa urahisi sana”

           UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KIJIJI CHA KASOMA WAENDELEA KWA KASI

Untitled

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu shule ya msingi Kasoma iliyopo kijiji cha Kasoma unaojengwa kwa nguvu za wananchi.

Na. Verediana Mgoma

WANANCHI kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji cha Kasoma, wamejitolea katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya kijiji hicho ili kupunguza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa.

Mtendaji wa kijiji cha Kasoma Faustine Majura, alisema kijiji hicho kina shule tatu zenye uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na mpaka sasa wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Kukosekana kwa vyumba vya kutosha vya madarasa, inaleta usumbufu mkubwa sana kwa walimu, na wakati mwingine inabidi kuchanganya wanafunzi na hivyo kuwa na mwingiliano wa walimu wakati wa ufundishaji” alisema Mtendaji Majura.

Mmoja wa walimu wa shule hiyo,  Thomas Malima akizungumzia ujenzi huo unaoendelea alisema, shule hiyo ya Kasoma ina vyumba vichache vya madarasa na kutokana elimu kuwa bure, wazazi wengi wamejitokeza kuandisha watoto wao, hivyo inawalazimu wanafunzi kusomea chini ya mti.

“Wazazi wamekuwa na muamko wa kuandikisha watoto na ongezeko hilo limepelekea upungufu wa vyumba vya madarasa, vyumba vilivyopo ni 11 na upungufu ni vyumba 13, kutokana na wingi wa wanafunzi shule ya msingi Kasoma imegawanywa kuwa A na B” alisema mwalimu Malima.

Aidha, mwalimu huyo mbali na kuelezea changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, alisema shule hiyo inakabiliwa na vifaa vya kufundishia, kujifunzia pamoja na upungufu wa walimu.

Hata hivyo, alimshukuru Mbunge wa Musoma vijijini Prof. Muhongo kwa kumaliza tatizo la upungufu wa madawati na kuahidi kumuunga mkono katika kuinua elimu ya jimbo hilo.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Nyamrandirira Ruteli  Maregesi, alisema kata yake ina jumla ya shule 10; moja ya sekondari na tisa za msingi, katika shule hizo kuna upungufu wa mkubwa vyumba vya madarasa hasa kwenye shule za msingi.

“Kuna mikakati tumeiweka ili kukabiliana na changamoto hii, mimi kama kiongozi mkuu wa kata, nitahakikisha wanafunzi wote wanasomea darasani na siyo chini ya mti tena, wala kubadilishana madarasa, lengo letu kuu ni  wanafunzi wote wakae darasani” alisema diwani Maregesi.

Aliendelea kusema: “tunamshukuru mbunge wetu kwa juhudi zake anazoendelea kuzionyesha kwa sasa hatuna tena upungufu wa madawati, pia kuna vitabu tulivyo pokea kutoka ofisi ya mbunge, vimesaidia kuongeza maarifa kwa shule zote za msingi na sekondari. Pia  tumepokea mgao wa saruji jimboni, kwenye kata ya nyamrandirira tumepokea jumla ya mifuko 420 ya saruji” alisema.

Diwani huyo alisema, saruji  hiyo kutoka ofisi ya mbunge imegawanywa kwa shule saba, kati ya shule 10 walizonazo, mpaka sasa kwenye mgao huo wamejenga vyumba 12 na bado wanaendelea na ujenzi.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunamaliza kabisa changamoto ya  upungufu wa madarasa uliopo, changamoto nyingine ni upungufu wa walimu na ahidi kulifanyia kazi kwa kupeleka maombi kwenye halmashauri yetu kwa utekelezaji. Tuna imani elimu ndio njia pekee ya kupambana na ujinga, maradhi na umaskini hivyo kuelimisha watoto wetu watajikomboa katika nyanja ya jamii na umaskini” alimaliza diwani Ruteli  Maregesi.

WANANCHI WA KIJIJI CHA ETARO WAANZISHA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI

Untitled

Moja ya mabwawa makubwa ya samaki lililojengwa kwenye kijiji cha Etaro

Na Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Etaro, kata ya Etaro wameanzisha mradi wa ufugaji wa samaki ili kuinua hali zao kiuchumi.

Wakizungumza kijijini hapo, baadhi ya wananchi hao wamesema, wamehamasika kuanzisha mradi huo baada ya kugundua uhaba wa samaki unaowakabili watu wanaoishi kando ya ziwa Viktoria kikiwemo kijiji chao.

Mmoja wa wananchi hao Jerad Kuyenga alisema, hali ya upatikanaji wa samaki imebadilika tofauti na ilivyokuwa zamani, hivisasa idadi ya samaki wanaovuliwa ni ndogo hivyo wanaofanikiwa kupata kitoweo hicho ni wachache.

“Nimeamua kufuga samaki kutokana na upungufu ya samaki ziwani, nimefuga samaki aina ya sato na nimepandikiza vifaranga elfu 10 vya samaki ndani ya bwawa. Nina matumaini makubwa hawa samaki siku za usoni nitajipatia kipato changu cha kutosha na kitoweo cha kila siku, maana ufugaji wa samaki ni mradi mzuri na ambao mtu anaweza kupata pesa nyingi” alisema Kuyenga.

Aidha Kuyenga aliwahimiza vijana na akinamama kuunda vikundi vya ufugaji wa samaki ikizingatiwa ufugaji huo ni rahisi na masoko yapo ya kutosha.

“Samaki ni zao ambalo huwezi kutoka kwenda kutafuta masoko, ila wanunuzi ndo watakuwa wakikufuata wenyewe. Niko radhi kabisa kutoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa mwananchi yeyote atakae kuwa tayari kufuga samaki.” alisema Kuyenga.

Naye Tatu Manyama ambaye alisema amefika kwa kijana huyo kupata elimu ya ufugaji wa samaki, alisema amehamasika na atajitosa kwenye mradi huo.

“Nimekuja kwa kijana huyu kupata mafunzo ya ufugaji wa samaki na utengenezaji wa bwawa la samaki, kwa sasa naendelea vizuri na nikitoka hapa nitaenda kuanza kutengeneza bwawa la kufugia samaki, maana kwa kweli samaki wana faida kubwa na wana soko” alisema Tatu Manyama na kutoa wito kwa akinamana wenzake kuanzisha mradi huo wa ufugaji wa samaki.

KIJIJI CHA MUHOJI WAANZA UJENZI WA MADARASA NA OFISI YA WALIMU

muhoji

Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu wa shule ya Msingi Muhoji.

Na. Hamisa Gamba

WANANCHI wa kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema wamejitolea kujenga vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Muhoji, Joseph Chinga akizungumza kijijini hapo alisema, kwa muda mrefu wanakabiliwa na uhaba wa madarasa, hivyo hatua hiyo ya wananchi inaonyesha nia yao ya dhati ya kukabiliana na tatizo hilo.

“Wazazi wameona ni aibu watoto wao kuendelea kusoma chini ya miti, hivyo wameamua kuunga mkono jitihada za mbunge katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu jimboni” alisema Chinga na kuongeza kuwa: “hali imekuwa mbaya sana baada ya ongezeko kubwa la wanafunzi wa darasa la awali, hivyo ujenzi huu umekuja wakati mwafaka.”

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Werema Magesa alisema, jitihada za kufanikisha ujenzi huo zimetokana na ushirikiano wa wananchi na viongozi wao, hivyo wanaamini watakamilisha ujenzi huo haraka ili wanafunzi wasome kwenye mazingira mazuri.

Hata hivyo, diwani wa Kata ya Bugwema Ernest Maghembe na Ofisi ya Mbunge jimbo la Musoma Vijijini wameahidi kuunga mkono jitihada za wananchi hao ambapo mbunge wa jimbo hilo ameahidi kutoa mabati yatakayotosha kuezeka jengo hilo.

WANANCHI KIJIJI CHA KUSENYI WAPAMBANA NA UHABA WA MADARASA

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kusenyi wakiwa katika shughuli ya umwagaji wa zege katika ujenzi unaoendelea wa vyumba vya madarasa.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kusenyi wakiwa katika shughuli ya umwagaji wa zege katika ujenzi unaoendelea wa vyumba vya madarasa.

Na. Verediana Mgoma

WANANCHI wa jimbo la Musoma vijijini wanaendelea kuongeza kasi katika suala la maendeleo hususani katika vijiji vyao baada ya kupata motisha kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo.

Mratibu elimu Kata ya Suguti Leonard Magoti, akizungumzia ujenzi unaoendelea wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya msingi Kusenyi alisema, pamoja na suala la madawati kushughulikiwa na kukamilika, changamoto ya vyumba vya madarasa imekuwa kubwa.

Mratibu huyo alisema, hali hiyo imetokana na uandikishaji wa watoto wanaojiunga na elimu ya msingi ambapo idadi yao imeongezeka zaidi ya vyumba vilivyopo, hivyo hatua hiyo ya kuanza ujenzi wa vyumba vinne itasaidia kupunguza changamoto hiyo.

Naye, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kusenyi, Bernadetha Musomi alisema, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 688, mpaka sasa shule ina vyumba vinane na upungufu shuleni hapo ni vyumba tisa.

“Imetubidi kutumia madarasa ya nje (chini ya miti) katika ufundishaji kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, kuna wakati inawabidi wanafunzi kusoma kwa kuhama hama kutafuta mahala penye kivuli kwa ajili ya masomo” alisema mwalimu Bernadetha.

Hata hivyo, mbali ya changamoto hiyo za madarasa, mwalimu mkuu huyo alimshukuru Prof. Muhongo kwa juhudi zake katika suala la kuinua taaluma ikiwemo kuwapelekea vitabu na madawati.

“Kwasasa hatuna tena upungufu wa madawati, nina vitabu vinavyo wajenga wanafunzi katika suala zima la lugha ya kiingereza pia katika upokeaji wa mifuko ya saruji itakuwa msaada mkubwa kutatua changamoto za vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kusenyi, Magesa Mashauri ameeleza jinsi wanavyoshughulikia changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, ambapo amekiri wamepiga hatua baada ya wananchi kuhamasika na kutoa michango.

“Tuliamua kugawana madaraka katika vitongoji ili kufanya zoezi la kuhamasisha uchangiaji wa ujenzi wa madarasa, mpaka sasa tuna jumla ya tofali 2500,  na msaada wa mifuko  ya saruji 120 tuliopokea kutoka ofisi ya mbunge utasaidia kuinua  maboma” alisema mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa, watakamilisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa mwishoni mwa mwezi huu.

 

KIJIJI CHA KOME WAJENGA VYUMBA 10 VYA MADARASA NA OFISI ZA WALIMU

Untitled

Shughuli ya ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika ufukwe wa kijiji cha Kome.

Na Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Kome kata ya Bwasi, wameendelea kushirikiana kwa pamoja katika shughuli za kimaendeleo hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi wote wa shule zote za Musoma vijijini wanasomea ndani tofauti na ilivyokuwa awali.

Hatua hiyo ni matokeo mazuri ya mchango mkubwa uliotolewa na Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kutoa mifuko ya saruji mwanzoni mwa mwaka huu, katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya msingi Kome B na kuagiza mifuko hiyo itumike katika ujenzi wa vyumba vya madarasa tu.

Ili kuhakikisha kasi ya Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini inaleta matunda makubwa ndani ya jimbo la Musoma vijijini, wananchi katika kijiji cha Kome wameonesha mfano bora kwa kujenga vyumba 10 vya madarasa na ofisi tano za walimu.

Wakizungumza na msaidizi wa mbunge baada ya kuwasili kijijini hapo, kufuatilia matumizi sahihi ya saruji hiyo iliyotolewa na mbunge, wananchi wa kijiji hicho kwa kauli moja wamethibitisha kuwa, wamejipanga kujenga vyumba vya madarasa na si vinginevyo.

Mmoja wa wakereketwa wa maendeleo kijijini hapo Kasigwa Manumbu, alisema neema iliyowashukia haiwezi kupotea bure, kwani ni wabunge wachache ambao wanaweza kubeba dhamana ya jimbo zima kwa kufanya maendeleo makubwa.

“Hii ni neema kwetu, haiwezi kupotea hivi hivi, kwa maana ni wabunge wachache wanaofanya mambo kama anayoyafanya Muhongo. Tutapambana kufa na kupona kuhakikisha hatumuangushi na tunaleta maendeleo yanayoonekana” alisema Kasigwa.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kome senta Andrea Matage alisema: “Tulichelewa kumpata kiongozi bora kama huyu na bado tukawa wavivu wa maendeleo. Ndio maana watoto leo wako nje, na hii ni kwa namna fulani tu ya kukosa maono na sasa tumempata kiongozi bora, watoto watasomea ndani, hatumuangushi mbunge”

Kwa upande wake, mwenyekiti  wa kitongoji cha Busasa, Kabende Bituro hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mbunge wao kwa mfumo mzuri anaoutumia wa kusimamia mipango yake jimboni.

“Maendeleo bora ni usimamizi bora, hii inaonekana wazi kwa utaratibu anaoutumia mbunge wetu wa kusimamia na kufuatilia mimi nashukuru. Ni dhahiri kabisa kuwa tunajenga kwa wakati na kukamilisha kwa wakati tena bila malumbano miongoni mwa wananchi na viongozi kama kipindi cha nyuma” alishukuru na kuweka wazi Kabende.

Diwani wa kata ya Bwasi, Masatu Nyaonge, amewashukuru wananchi wa kijiji cha Kome kwa mwitikio mzuri waliouonesha katika jukumu la ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuhakikisha kufikia Februari mwishoni, ujenzi wa vyumba 10 utakuwa umekamilika.

“Nitoe shukrani zangu za pekee kabisa kwa wananchi wa Kome kwa namna mlivyoguswa na jambo hili la upungufu wa vyumba vya madarasa. Kwa maana hiyo basi, sitegemei kumuangusha Mbunge wetu” alishukuru na kuahidi Nyaonge.

KIKUNDI CHA SARAGANA WAKARIBIA KUVUNA MAZAO YAO

Untitled

Na Hamisa Gamba

KIKUNDI cha kilimo cha bustani cha Saragana, kipo kwenye hatua za mwisho za kuvuna mazao waliyopanda ikiwa ni msimu wao wa kwanza kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Thobias Kajale alisema, kikundi chao ni kipya na kina miezi nane tangu kianzishwe, ambapo msimu huu wamelima kabichi, nyanya na vitunguu.

“Mwanzo kila mmoja alikuwa analima mwenyewe, lakini hakuna mazao mazuri yaliyopatikana, hivyo tukaamua kuunda kikundi, sasahivi tuna matumaini makubwa ya kupata mazao ya kutosha” alisema Kajale.

Mmoja wa wajumbe wa kikundi hicho Mfungo Felisian alisema,  baada ya kuvuna mazao hayo, wanatarajia kutafuta soko kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya jimbo lao ili baada ya mauzo waandae mashamba kwa ajili ya msimu mwingine.

 

UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI KURUGONGO WAFIKA HATUA NZURI

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu Shule ya msingi Kurugongo “B”katika kijiji cha Bujaga.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu Shule ya msingi Kurugongo “B” katika kijiji cha Bujaga.

Na Fedson Masawa

UJENZI wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya msingi Kurugongo “A” na “B” vinavyojengwa na wananchi wa kijiji cha Bulinga na Bujaga kata ya Bulinga umefikia hatua nzuri.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na mchango wa mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ikiwa ni harakati za kupambana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa visivyopungua 800 kwa shule zote za jimbo lake.

Akizungumza na msaidizi wa mbunge aliyefika kwenye eneo la ujenzi wa vyumba hivyo kwa lengo la kufuatilia zoezi la ujenzi huo, Mwenyekiti wa kijiji cha Bujaga Kalebu Musa, alisema viongozi kwa kushirikiana na wananchi, wamehamasika kutokana na jitihada za mbunge na hivyo wapo tayari kufanya kazi za maendeleo pamoja na Mbunge wao.

Mwenyekiti huyo alisema, isingekuwa nguvu za mbunge, wananchi peke yao wasingeweza kufanikisha ujenzi huo, hivyo uwepo wake ni neema isiyo na mfano.

“Bila Mbunge, wananchi wetu ingekuwa vigumu kuimudu hii kazi kwa kuchangishana fedha. Kwa niaba ya wananchi wetu, mimi nasema kuwa na mbunge kama Muhongo ni neema isiyo na mfano na tutafanya naye kazi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hivyo sasa tunaahidi kukamilisha ujenzi huu ndani ya mwezi huu wa Januari” alimaliza mwenyekiti Kalebu Musa.

MIRADI MIPYA MITATU YATAMBULISHWA MUSOMA VIJIJINI

untitled

Mkurugenzi wa Tanzania Business Creation Company Limited Elibariki Mchau (aliyesimama) akitoa elimu juu ya miradi ya Sungura, mchaichai na kuku kwenye kikao chao na madiwani, wasaidizi wa mbunge na wananchi wa Musoma vijijini.

Na Fedson Masawa

MIRADI mitatu mikubwa ya ufugaji wa sungura, kuku na kilimo cha mchachai inatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni ndani ya jimbo la Musoma vijijini.

Hatua hiyo inakuja baada ya Tanzania Business Creation Company Limited (TBCC) kukutana na wabunge wa Mkoa wa Mara na kukubaliana Mkoa uanzishe miradi hiyo.

Baada ya kikao hicho, TBCC walipata fursa ya kukutana na madiwani na wananchi kwenye kata ya Tegeruka na kuitambulisha miradi hiyo kwa wananchi na madiwani.

Wananchi wa jimbo la Musoma vijijini walionekana kufurahishwa na kuikubali miradi hiyo, ambapo mbunge wao Prof. Muhongo alijitolea kulipia vikundi vitano (5) katika kata ya Tegeruka vitakavyokuwa vinajishughulisha na ufugaji wa sungura.

Mbali na vikundi hivyo, Prof.  Muhongo aliwaomba madiwani wapendekeze vikundi vingine kutoka kata tofauti kwa ajili ya ufugaji wa kuku na kilimo cha mchaichai.

Vikundi vilivyopendekezwa ni kutoka kata za Kiriba, Murangi na Nyegina (ufugaji wa kuku) na Mugango, Bugwema na Seka (kilimo cha mchaichai). Vikundi hivi vyote vilipendekezwa kuwa vikundi vya majaribio jimboni.

Ili kuwahakikishia wananchi na viongozi wa Musoma vijijini kuhusu miradi hiyo, Prof. Muhongo aliwaagiza madiwani, wasaidizi wake na wananchi wakutane na TBCC kwa ajili ya mazungumzo zaidi pamoja na kutoa elimu juu ya miradi hiyo kwa wananchi wa Musoma Vijijini.

Awali akielezea Mradi wa sungura, Mkurugenzi wa TBCC, Elibariki Mchau alisema, sungura wanazo faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkojo wake ni kiwatilifu kwa ajili ya kupambana na wadudu waharibifu wa mazao, kinyesi cha sungura ni mbolea iliyo bora kwa mazao yote hasa mbogamboga na nyama ya sungura ni moja ya nyama iliyo bora kwa afya.

Mchau alisema, sungura mmoja huwa na uzito wa kilo 3-5 na kilo 1 hununuliwa kwa 8,000/= na sungura 1 mzazi anao uwezo wa kuzalisha sungura 60-100 kwa mwaka na kumpatia mfugaji kipato cha 1,440,000/=  hadi 2,400,000/=. Kwa kuwa ufugaji huu hufanywa kwa jozi yenye sungura jike 6 na dume 1, Mchau alisema mfugaji atajipatia kipato cha 8,640,000/= hadi 14,400,000/= kwa jozi 1 kwa mwaka.

Pamoja na faida hizo, Mchau aliongeza kuwa, kampuni hutoa mafunzo kwa wafugaji/wakulima na kutafuta mazao yenye tija kwa kipindi chote cha mkataba ambacho ni miaka mitano. Mchau pia alisema, ili kuanza mradi huu, ni lazima mfugaji apate mafunzo, sungura wazazi, mabanda bora, vyakula, ughani, mkataba wa ufugaji na soko la uhakika.

Akihitimisha ufafanuzi wa mradi wa sungura, mchau aliweka wazi gharama za kufanikisha mradi huu kuwa ni; jozi 1 ya sungura 7 (6 jike na 1dume) ni 595,000/= na banda la kufugia (kutoka nje) ni 480,000/= likiwa kamili na vifaa vyake vyote na chakula mifuko miwili ni 110,000/= cha kulishia sungura wazazi kwa miezi 4. Hivyo unaweza kuanza mradi huu ukiwa na 1,185,000/=

Akizungumzia MRADI WA KUKU (super solomony) Mchau alisema, huu ni mradi wa kufuga kuku ambaye anatoa mazao ya kuku aina tatu; Kuku wa nyama (broiler), Kuku wa kienyeji (kwa ajili ya supu na kupika majumbani) na Mayai.

Akiainisha faida za mradi wa kuku, Mchau alisema, kuku wa nyama (broiler) huvunwa ndani ya wiki tano tangu siku ya kwanza ya kuanza kumfuga. Kuku hawa kampuni inawanunua kwa bei ya 5,000/= kila mmoja akiwa hai. Kuku wa nyama (kuku wa kienyeji) wanaovunwa kuanzia wiki 12 hadi wiki 15 tangu siku ya kuanza kufugwa nao hununuliwa na kampuni kwa kati ya 7,000/= 9,000/= kila mmoja.

Pia mayai ya kuku (super solomony) huanza kupatikana baada ya kumfuga kuku huyu kwa kipindi cha wiki 22, kuku huyu anao uwezo wa kutaga mfululizo kwa miezi 18-20 bila kukoma na baada ya hapo, uzalishaji huanza kushuka. Kampuni hununua trei moja ya mayai hayo kwa 9,000/= ambapo mtaji kwa ajili ya mradi huo ni 1,000,000.

Awali akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa mchaichai, alisema kuwa, mchaichai hulimwa kwa ajili ya viungo vya chai, vyakula na mafuta ya mchaichai (essential oil/perfume).

Aliongeza kuwa, mchaichai mkavu hutoa kilo 700 kwa ekari 1 ambapo kilo 1 hununuliwa na kampuni kwa bei ya 1000 – 1500 ambayo itategemea bei ya sokoni. Pia amebainisha kuwa, ekari moja ya mchaichai hutoa mavuno ya majani mabichi kilo 4,000 ambapo kampuni hununua kwa Tsh 400/= kwa kilo moja ambayo ni sawa na shilingi 1,600,000/= kwa ekari na kwa mwaka mmoja huvunwa mara 3 ambapo atajipatia  Tsh 4,800,000/= kwa mwaka kwa ekari 1.

Akizungumzia gharama za kuanzisha mradi huu, mkulima anatakiwa kuwa na shamba ekari 1 au zaidi, maji ya uhakika, mbegu za ekari 1 ambayo kila moja inagharimu 650,000/= ikiwa ni pamoja na shughuli za ugani, mbolea ya viwatilifu 200,000/=

Akihitimisha kikao hicho, Mkurugenzi wa Tanzania Business Creation Company Limited, Elibariki Mchau amewaomba viongozi na wananchi kujitahidi kuhamisishana ili kuongeza idadi ya wahitaji na kufanikisha mradi huu na kuufanya uwe endelevu ndani ya jimbo la musoma vijijini.

Kwa upande wake mjasiliamali kutoka kata ya Tegeruka, Kubwera Rutende, alimpongeza Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kwa kuibua fursa mbalimbali jimboni mwake na yeye kuonekana kuwa mwanzilishi kwa kuamua kuvidhamini vikundi na kuwataka vijana kuchangamkia fursa hizi ili kuondokana na utegemezi.

“Mimi nampongeza sana mbunge wetu kwani ana nia ya kutusaidia. Ana uwezo wa kuona fursa na kuleta jimboni na yeye anakuwa wa kwanza kutudhamini. Ni jambo la kuchangamkiwa sana na vijana wetu” alisema mzee Rutende.

WANANCHI WA KIJIJI CHA KABONI WAJENGA OFISI 

kaboni

Mtendaji wa kijiji cha Kaboni Veronica Burure akiwa mbele ya jengo la ofisi ya kijiji ambalo ujenzi wake unaendelea.

 Na. Verediana Mgoma

WANANCHI kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Kaboni kilichopo kata ya Nyamrandirira, wameanza ujenzi wa jengo la ofisi ya kudumu ya kijiji hicho.

Mtendaji wa kijiji hicho Veronica Burure alisema, kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia jengo la kukodi, hivyo kuanza kwa ujenzi huo ni moja ya hatua kubwa ya maendeleo katika kijiji chao.

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi huo, Mtendaji wa kata ya Nyamrandirira, Joseph Lyakurwa alisema unaendelea vizuri na amehamasika kuhimiza ujenzi wa ofisi kama hiyo kwenye vijiji vingine vilivyopo ndani ya kata yake kwani ni jambo zuri viongozi kuwa na ofisi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Isack Simion mbali na kufurahishwa na hatua nzuri za ujenzi huo, alisema wanakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa jengo hilo.

“Licha ya maendeleo kuwa mazuri, lakini tuna changamoto ya kumalizia jengo hili ikiwemo upauaji, ila tunaendelea kuhimiza wananchi katika uchangiaji, pia tunaomba msaada kutoka kwa  mbunge ili kukamilisha jengo hili mapema zaidi” alisema mwenyekiti huyo.

UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA WAANZA MUGANGO

untitled

Mkuu wa shule mwalimu Samweli Samike (kushoto) akiwa na msaidizi wake mwalimu Charles Farafata wakiteta jambo kuhusu ujenzi wa madarasa walipotembelewa na msaidizi wa mbunge.

Na. Ramadhani Juma

WANANCHI wa Kata ya Mugango wameanza zoezi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa baada ya kukamilisha zoezi la ufyatuaji matofali zaidi ya 3,000.

Ujenzi huo unatokana na kuwepo kwa upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa, ambapo vyumba hivyo vikikamilika vitapokea watoto zaidi ya 250 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2017.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Samwel Samike, alisema shule ina upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa hii ni kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

Aidha, mwalimu Samike aliwashukuru viongozi na wananchi wa Kata ya Mugango kwa jinsi walivyoona umuhimu wa kuongeza idadi ya vyumba ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.

“Nawahakikishia wana Mugango kuwa nitatoa ushirikiano wa kutosha ili tuweze kufanikisha ujenzi huu kwa muda mwafaka” aliahidi mwalimu Samike.

Kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Charles Farafata alimuomba msaidizi wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini aliyefika shuleni hapo kulipeleka suala hilo katika ofisi ya mbunge ili kuweza kupata msaada wa kupaua.

“Wananchi wamejitolea kujenga boma kwa kutoa michango ya fedha, sina uhakika kama wanaweza kujenga hadi kukamilisha jengo hili. Hofu yangu ni kwamba yawezekana wakaishia kwenye ujenzi wa boma tu. Hivyo tunakuomba umweleze mbunge kama inawezekana atusaidie kazi ya kupaua” alisema mwalimu Farafata.

VIJANA WACHANGAMKIA KILIMO CHA MAHINDI KIJIJI CHA KUSENYI

mahindi-2

Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mahindi kwa njia ya umwagiliaji wakiandaa bomba kwa ajili ya kumwagilia mazao yao. Kushoto ni Gidion Max akiwa na Mafuru Kachepe.

Na. Verediana Mgoma

VIJANA wa kijiji cha Kusenyi, jimbo la Musoma vijijini wamejitosa kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuinua uchumi wa familia zao na kijiji wanachoishi.

Mmoja wa vijana hao Gidion Max alisema, wamehamasika katika kilimo hicho cha mahindi kwa umwagiliaji kutokana na thamani ya zao hilo na uhakika wa soko.

“Ukitaka kufanikiwa kulima zao la mahindi kwa umwagiliaji ni kutafiti msimu mzuri wa kulima zao hilo; kati ya kiangazi au masika, japo sisi tumelima wakati wa kiangazi, kingine ni kuangalia soko linahitaji mahindi kwa ajili ya chakula (uji na ugali)  au mahindi ya kuchoma” alisema Max.

Kwa upande wake Masinde Mjarifu, ambaye ni Bwana shamba wa kijiji hicho alisema amekuwa akiwatembelea mara kwa mara vijana hao na kuwapa elimu ya kilimo na wamekuwa wakizingatia maelekezo wanayopewa.

“Kilimo cha mahindi wakati wa  kiangazi hakina ugumu endapo tu wahusika wakiwa na eneo la kutosha, maji, mbolea na udhibiti wa wadudu” alisema Mjarifu.

Akizungumzia kuhusu soko la mahindi ya kuchoma ambalo vijana hao wamelilenga, Mjarifu alisema, mahindi hayo hulimwa kwa mtaji mdogo na yanawapatia watu wengi fedha za kutosha kukidhi mahitaji yao.

Naye mtendaji wa kijiji cha Kusenyi, Arodia Geatamwa alisema vijana wengi hivi sasa wameacha shughuli ya uvuvi wa samaki ambayo walikuwa wanaifanya na kugeukia kilimo cha umwagiliaji.

“Vijana wengi wameamua kutumia fursa ya kilimo cha umwagiliaji, hivi sasa idadi ya wakulima imeongezeka na kufikia kijiji kimoja kuwa na vikundi zaidi ya 25 wanaojishughusha na kilimo cha umwagiliaji, wapo wanaolima mahindi na wengine bustani za mboga mboga na matunda” alisema mtendaji huyo.

Hata hivyo, mtendaji Arodia alielezea changamoto zinazokabili vikundi hivyo ni pamoja na upungufu wa mashine za umwagiliaji, pembejeo na masoko, ingawa wanaendelea kuhamasisha vijana wawe na utayari, uthubutu na kuwa wafatiliaji wa fursa na kujifunza ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

WANANCHI MUGANGO WAONGEZA KASI YA UJENZI WA ZAHANATI

mchanga

Wananchi wa Kata ya Mugango wakisomba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Na. Ramadhani Juma

ZOEZI la ujenzi wa kituo cha afya Mugango limechukua sura mpya baada ya wananchi kuamua kufanya kazi mchana na usiku ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Mwandishi wa habari hizi ambaye pia ni msaidizi wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, alishuhudia wananchi wakifanya shughuli mbalimbali za ujenzi huo ikiwemo kusomba mchanga na maji.

Wananchi hao walikiri kufanya uzembe kwa kuchelewa kuitikia wito wa kushiriki kwenye ujenzi huo, lakini sasa wanasema wapo tayari kufanya kazi za ujenzi bila kuchoka ili kumaliza jengo hilo ambalo hadi sasa hatua ya ujenzi wa msingi wa jengo la wodi ya mama na mtoto unaelekea kukamilika.

“Tumeamua kufanya kazi mchana na usiku ili kunusuru vitendea kazi tulivyopewa na mbunge visije kuharibika kwa mfano saruji, haitakiwi kukaa sana bila kufanyiwa kazi” alisema Masatu Magwegwe, mmoja wa wananchi aliyehamasika kushiriki ujenzi huo.

Naye msimamizi mkuu wa shughuli hiyo ya ujenzi ambaye ni diwani wa Viti Maalum, Kadogo Kapi alisema baadhi ya kazi walizotumia fedha hapo mwanzo sasa zinafanywa na wananchi, hivyo fedha hizo zitatumika kwenye shughuli nyingine za ujenzi huo.

“Mwanzoni tulisomba mchanga kwa kutumia gari, lakini kwa sasa wananchi wameamua wasombe wenyewe kwa kutumia ndoo. Hali hiyo imetupunguzia gharama za ujenzi” alisema diwani Kadogo.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo, Yahaya Chikomati amekiri kuwa juhudi za wananchi walizozionyesha zimeongeza chachu katika ujenzi huo.

“Zoezi hili sasa linaenda kwa kasi, ni imani yangu kwamba ndani ya miezi miwili tutakuwa tumekamilisha ujenzi. Nawasihi wananchi waendelee na juhudi zao ili kumaliza ujenzi wa jengo hilo kwa muda muafaka” alisisitiza Chikomati.

UJENZI WA CHOO CHA KISASA WALETA CHANGAMOTO KWIBARA

choo

Moja ya choo cha kisasa kilichojengwa kwenye shule ya msingi Mugane (Picha na Ramadhani Juma)

Na. Mwandishi Wetu

KASI ya ujenzi wa vyoo vya kisasa katika baadhi ya shule za msingi za Jimbo la Musoma vijijini imeongezeka ambapo tayari vyoo 38 kati ya 45 vimejengwa na kusababisha kuwepo kwa changamoto ya ujenzi wa madarasa yatakayoendana na vyoo hivyo.

Vyoo hivyo vimejengwa kwa muda wa miezi miwili ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa vyoo bora na vya kisasa unaofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la PCI wenye lengo la kukabiliana na upungufu na matundu ya vyoo kwenye shule mbalimbali za jimbo hilo.

Wananchi wa kijiji cha Kwibara wakiongea na mwandishi wa habari hizi wamelipongeza shirika hilo kwa jinsi walivyotekeleza mradi huo katika shule yao ya msingi Mugane ambayo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa matundu ya vyoo.

“Tunawashukuru PCI kwa kukamilisha ujenzi wa choo bora katika shule yetu, hakika PCI wametusaidia sana, tusingekuwa na uwezo wa kujenga choo cha aina hiyo” alisema Kambarage Mwikwabe, mkazi wa kijiji cha Kwibara.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mugane Kasian Erasto amekiri kwamba ujenzi wa choo hicho ni chachu ya maendeleo katika shule yao, hivyo amewaomba wazazi washiriki kikamilifu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Itakuwa ni aibu jengo zuri shuleni iwe ni choo hivyo tuna kila sababu ya kujenga vyumba vizuri vya madarasa vitakavyoendana na ubora wa choo hicho” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Kwibara John Wetare amesisitiza juu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule tatu zilizopo katika kijiji hicho huku akiweka wazi ahadi ya ofisi yake katika kufanikisha ujenzi huo.

“Nimeguswa sana na jinsi wafadhili hawa walivyoamua kututengenezea vyoo vya gharama kubwa wakati hatuna madarasa, mimi na serikali yangu ya kijiji tumeamua kujenga vyumba saba (7) katika shule zetu tatu za msingi. Serikali yangu imetoa mifuko mia moja kwa kila shule kwa ajili ya ujenzi wa vyumba bora vya madarasa.  Nimeamua tujenge madarasa yenye ubora zaidi ya choo tulichopewa ufadhili” alisisitiza Wetare.

Hadi sasa serikali ya kijiji cha Kwibara imeshafyatua matofali zaidi ya 8000 yatakayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi tatu; Kwibara “A”, Kwibara “B” na Mugane.

WAKULIMA WA BUSTANI WAZIDI KUONGEZEKA MUSOMA VIJIJINI

Wakulima wa bustani wakiwa katika bustani yao ya nyanya wakiitikia wito wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo anayewahimiza kujiajiri kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda

Wakulima wa bustani wakiwa katika bustani yao ya nyanya wakiitikia wito wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo anayewahimiza kujiajiri kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda.

Na. Ramadhani Juma

WANANCHI wa Jimbo la Musoma vijijini wameendelea kujitokeza kwa wingi katika kilimo cha bustani za mboga na matunda.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakulima hao walisema, wameamua kujitokeza kwenye kilimo hicho baada ya kugundua kilimo cha kutegemea mvua hakina tija hivyo ni bora wajikite kwenye kilimo cha umwagiliaji hususani bustani za mboga na matunda.

“Nimepata mafanikio makubwa katika kilimo hiki cha bustani ukilinganisha na kilimo cha pamba, ninatumia muda mfupi katika kuzalisha na kipato changu kinazidi kuongeza siku hadi siku, hakika kilimo cha bustani hakina usumbufu na mazao yake yana soko muda wote,” alisema Jumanne Tera, mkulima wa bustani.

Pamoja na mafanikio wanayoyapata, mkulima mwingine Nyafuru Nyang’aya alisema zipo changamoto ambazo wanakumbana nazo ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi hususani pampu za umwangiliaji.

“Tunaomba msaada wa vitendea kazi hivyo kutoka ofisi ya mbunge kama inawezekana. Tulimuona Mbunge akiwezesha baadhi ya vikundi vya kilimo cha bustani, hivyo nasi ambao hatukupata msaada huo ni muda mwafaka sasa wa kuweza kusaidiwa,”alisema Nyafuru Nyang’aya.

WANAFUNZI NYAMBONO WAOMBA MSAADA WA KUMALIZA JENGO LA MAABARA

nyambono

Jengo la ofisi ya kata ya Nyambono ambalo ujenzi wake unaendelea.

Na. Hamisa Gamba

WANAFUNZI wa shule ya msingi Nyambono wamemuomba mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuwasaidia ukamilishaji wa jengo la maabara ambalo limesimama kwa muda mrefu bila kuendelezwa.

Akitoa ombi hilo mbele ya mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, na Mwalimu Mkuu Emmanuel Daudi, mwanafunzi Vumilia Paul kwa niaba ya wanafunzi wenzake alisema jengo hilo limekaa kwa takribani miaka mitano bila ujenzi wake kuendelea na kuwakosesha fursa ya kujifunza kwa vitendo.

“Tunaomba nguvu ya Mbunge kugusa katika jengo hili ili tuweze kuonyesha ushindani wa ufaulu wa mitihani ya taifa katika masomo ya sayansi” alisema Vumilia.

Wakati huo huo wananchi wa kata ya Nyambono inayoundwa na vijiji viwili Nyambono na Saragana wameanza ujenzi wa ofisi mpya ya kata hiyo baada ya ofisi ya awali kuharibika.

Diwani wa kata hiyo Mkoyongi Masatu alisema, wapo kwenye harakati za kuhakikisha ofisi hiyo inakamilika na kuanza kutumika kwa shughuli za utawala.

“Nawasihi viongozi wote wa kata na wananchi kwa ujumla  kuweka juhudi zao katika kuhakikisha ofisi hii inakamilika na kuanza kutumika” alisisitiza diwani Masatu.

Aidha, mbali na ujenzi huo, diwani Masatu amewahimiza wananchi wa kata ya hiyo kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye kata yao kwa kuwa maendeleo yanamgusa kila mwananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Nyambono, Luti Malima aliahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wengine akiwemo diwani katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kusimamia miradi inayotelekezwa kwa uaminifu.

 

KATA YA MABUI WAANZA UJENZI WA CHOO CHA SHULE YA SEKONDARI

untitled-mabui

Mafundi wakiwa katika ujenzi wa choo cha shule ya sekondari Mabui Merafuru.

Na. Verediana Mgoma

UONGOZI wa Kata ya Mabui Merafuru kwa kushirikiana na wananchi wake, wamejitolea kwenye ujenzi wa choo cha walimu katika shule ya sekondari ya kata hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mtendaji wa Kata ya Mabui Merafuru, Doricas Tongoro alisema wameamua kuanza ujenzi huo baada ya choo cha awali cha shule ya sekondari ya Mabui Merafuru kuharibika.

Mtendaji Tongoro alisema, wao kwa upande wa serikali wamejitolea kujenga matundu mawili ya choo huku wananchi wamejitolea nguvu zao kwa kukusanya mawe na mchanga.

Naye mratibu elimu kata, Mahendeka Kasanje alithibitisha kupokea kiasi cha fedha kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho huku akipongeza ushirikiano wanaotoa wananchi wa kata hiyo.

“Mpaka sasa kwa fedha kutoka halmashauri tumenunua saruji, mabati, mabomba, nondo na mbao, kwahiyo tuna uhakika wa kumaliza ujenzi huu mapema” alisema Mahendeka Kasanje.

WANANCHI NYEGINA WASHIRIKI KUJENGA VYUMBA VINNE VYA MADARASA

untitled4

Ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea kwenye shule ya msingi Nyegina ‘B’

Na Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Nyegina wamejenga vyumba vinne vya madarasa ili kukabiliana na upungufu uliokuwa unaikabili shule ya msingi Nyegina ‘B’ na kusababisha wanafunzi wa shule hiyo kusomea nje.

Akizungumza kijiji hapo, mmoja wa wananchi waliojitolea kushiriki ujenzi huo Shabani Magesa alisema kutokana na tatizo la upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa kwa muda mrefu, wameamua kujitolea kwa nguvu zao kujenga vyumba vya madarasa.

“Nina imani vyumba hivi vitasaidia kupunguza tatizo la watoto kusomea nje, hatutakubali kuona watoto wetu wakiendelea kusomea nje, tutahakikisha tunajitolea kuongeza vyumba vingine vya madarasa” alisema Magesa.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyegina, Majira Mchele aliwashukuru wananchi wa kata yake na serikali ya kijiji hicho kwa kumpa ushirikiano katika kutafuta maendeleo ikiwemo kushiriki kwenye ujenzi huo wa vyumba vya madarasa.

“Tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa lilikuwa sugu, lakini sasa tutahakikisha tunapambana kumaliza tatizo hili, ninachoomba mbunge wetu ndugu Sospeter Muhongo atuunge mkono kwa kutusaidia mbao, mabati na misumari, kwa ajili ya kupauwa jengo hili ili watoto wetu wapate mahali pazuri pa kusomea” alisema diwani Majira Mchele na kuahidi kuongeza vyumba vingine vya madarasa katika shule zote za kata yake.

KATA YA BULINGA NA BUJAGA WAANZA KUBORESHA ELIMU

untitled

Thereza Rusweka (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na mwenyekiti wa kijiji cha Bulinga Maira Masaule (wa pili kutoka kushoto) aliyesimama kulia ni Mtendaji wa kata ya Bulinga Gudrack Mazige, na kushoto ni Obadia Sendi, Mtendaji wa kijiji cha Bulinga.

Na Fedson Masawa

MIFUKO 100 ya saruji iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo imekabidhiwa katika uongozi wa vijiji viwili ndani ya kata ya Bulinga na tayari zoezi la ufyatuaji wa tofali kwa ajili ya ujenzi limeanza.

Vijiji vilivyokabidhiwa mifuko hiyo ni Bulinga; ambacho kilikabidhiwa jumla ya mifuko 50 na Bujaga kilichokabidhiwa mifuko 50.

Mifuko hiyo 100 ya saruji ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbili ambazo ni shule ya Msingi Kurugongo “A” na “B” ambapo ujenzi huo wa vyumba vya madarasa ni sehemu ya mipango ya Prof. Muhongo ya kuboresha sekta ya elimu jimboni mwake.

Mtendaji wa kijiji cha Bulinga, Obadi Sendi amethibitisha kuanza kwa zoezi la ufyatuaji wa matofali na kuahidi kukamilika ndani ya siku mbili zijazo kutokana na ari wananchi ambao wamejitolea kushirikiana na mbunge katika mipango yake yote ndani ya jimbo lao.

“Wananchi wamejipanga vizuri na tunatarajia baada ya siku mbili zijazo, tutakuwa tumemaliza kufyatua matofali na kuanza shughuli za uchimbaji wa msingi. Hii ni kwa sababu wananchi wangu wamejipanga vyema na wananipa moyo katika kuendana na kasi ya mbunge wetu” alisema mtendaji huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Bulinga, Maira Masaule aliomba ofisi ya mhandisi isije ikaonesha namna yoyote ya ucheleweshaji wa ujenzi huu na kama ikitokea hali hiyo, basi wananchi hawatosita kuanza ujenzi kama watakavyoshauriwa na mafundi wao.

“Tunachokiomba sasa ni ofisi ya mhandisi kufanya jitihada za kuwahi kufika kwenye ‘site’ kwani tayari tumeshawafikia, na endapo wakionesha kila dalili ya kutukwamisha basi sisi tutaanza ujenzi kwa kuwasikiliza mafundi wetu” alisema mwenyekiti Masaule.

Naye mtendaji wa kijiji cha Bujaga, Frank Anatori alisema, tayari wameshafyatua matofali 989 na wanatarajia kukamilisha mapema kabla ya mwezi Novemba haujakwisha.

Sambamba na hayo pia, Mtendaji wa Bujaga alisema kijiji chake tayari kimeshaanza ujenzi wa choo kimoja kikubwa kwa ajili ya shule ya msingi Kurugongo “B” na wanatarajia kuanza kuchimba msingi wa vyumba viwili vya madarasa.

“Tayari tumeshafyatua matofali 989 na tunatarajia kuyakamilisha ndani ya mwezi huu yale yaliyobakia. Vilevile tumeanza ujenzi wa choo kikubwa na msingi upo tayari tutakamilisha hatua ya msingi wa vyumba vya madarasa ndani ya wiki hii” alisema Frank Anatori.

untitled3

Ujenzi wa choo cha wanafunzi ukiendelea katika eneo itakapojengwa shule ya msingi Kurugongo “B”

KASI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA YAONGEZEKA

untitled-2

Vyumba viwili vya madarasa vinavyojengwa shule ya msingi Kataryo (Picha na Ramadhani Juma).

KASI ya ujenzi wa vyumba vya madarasa imeongezeka maradufu katika baadhi ya kata za jimbo la Musoma vijijini.

Kasi hiyo imedhihirika katika kijiji cha Kataryo kilichopo kata ya Tegeruka, baada ya wananchi wa kijiji hicho kujenga vyumba viwili vya madarasa na nyumba moja ya mwalimu kwa muda wa mwezi mmoja.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho, diwani wa kata ya Tegeruka Benjamin Maheke alisema, ahadi na kauli zinazotolewa na mbunge wao ni chachu kwa maendeleo yao.

“Mbunge wetu ameahidi kutoa misaada katika maeneo ambayo wananchi wamekwishaanza shughuli husika. Kauli hiyo imepelekea sisi viongozi wa Kata ya Tegeruka, viongozi wa vijiji na wananchi kwa ujumla kuanza ujenzi wa miundombinu ya shule zetu kwa kasi ili tuweze kupata misaada kutoka kwa mbunge wetu” alisema diwani Maheke.

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Kataryo, Juma Muyemba aliahidi hadi 15, Disemba mwaka huu, vyumba viwili vya madarasa pamoja na nyumba ya mwalimu vitakuwa vimekamilika.

“Nakuhakikishia kuwa, tumejipanga kukamilisha ujenzi wa maboma hayo ifikapo disemba 15, siku ukifanya tena hapa Kataryo utakuta tumekamilisha ujenzi huo, matofali yapo ya kutosha na pesa za mafundi pia zipo. Tunakuomba umfikishie mbunge salamu zetu na kumwomba msaada wa upauaji wa majengo haya” alisisitiza Muyemba mbele ya msaidizi wa mbunge.

Hadi sasa majengo hayo yamefikia usawa wa ‘linta’ na wananchi wanaendelea na juhudi za ukusanyaji wa matofali kwa ajili ya ukamilishaji.

KIKUNDI CHA MAENDELEO DAIMA WAJIVUNIA MAFANIKIO YA KILIMO CHA BUSTANI 

untitled

Viongozi wa kikundi cha Maendeleo Daima wakiwa kazini. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Makweba Majura na Maiga Malima (Picha na Ramadhani Juma).

Na Ramadhani Juma

MAKUNDI ya vijana kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Musoma vijijini yameendelea kujitokeza kwa wingi katika kilimo cha bustani.

Kilimo hicho ambacho kimehasishwa na mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo, kinaendeshwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo ambapo vikundi 15 vya vijana na akina mama vilivyokuwa vinajishughulisha na kilimo cha bustani za mboga na matunda vimewezeshwa.

Hadi sasa kilimo hicho kimekuwa shughuli endelevu ndani ya jimbo hilo na zaidi ya vikundi 214 vimekuwa vikilima nyanya, vitunguu, kabichi na matikiti maji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wa Kikundi cha Maendeleo daima (NYANG’OMA) walisema, licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, lakini wameanza kupata mafanikio ya kilimo hicho.

“Tupo vijana sita katika kikundi chetu, na huu ni msimu wa pili wa uzalishaji, mara ya kwanza tulilima nyanya na kuvuna mwezi wa nane, hakika tunamshukuru Mungu kwani tulipata zaidi ya shilingi milioni mbili ndani ya miezi mitatu na nusu, hayo ni mafanikio makubwa kwetu” alisema Mafuru James, mmoja wa viongozi wa kikundi hicho na kuongeza kuwa:“kwa sasa tumelima eneo kubwa zaidi, hivyo matarajio yetu ni kupata mara mbili ya kile tulichopata awamu ya kwanza.”

Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho Makweba Majura alielezea changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni ukosefu wa vitendea kazi, upungufu wa madawa pamoja na wanyama waharibifu wakati wa usiku.

“Tunamwagilia bustani yote kwa kusomba maji kwa ndoo, hii ni kutokana na kutokuwa na pampu ya kusukuma maji, pia kipindi mazao yakikaribia kukomaa tunalala shambani kwa ajili ya kulinda wanyama waharibifu, kiukweli ni kazi ngumu sana” alisema Makweba.

Makwebwa aliendelea kusema: “Tunaomba mheshimiwa mbunge atuangalie kwa jicho la pili katika uongozi wake, atusaidie vifaa kama alivyowasaidia wale wa mwanzo, yeye ndiye aliyetuonyesha hii njia ya kujiletea maendeleo yetu. Hakika tunampongeza kwa juhudi anazozionesha ndani ya jimbo”

 

KAULI YA PROF. MUHONGO YALETA MABADILIKO KWIBARA

kwibara-2

Vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu inayojengwa kwenye kijiji cha Kwibara.

Na Ramadhani Juma

KAULI ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuwataka wananchi wake kujituma na kutafuta maendeleo yao wenyewe, imeanza kuzaa matunda baada ya wananchi wa kijiji cha Kwibara kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Mwenyekiti wa kijiji hicho John Wetare, alikiri kwamba kauli ya mbunge wao imeleta chachu ya maendeleo jimboni humo na wananchi wanajituma na kutoa ushirikiano kwa serikali ya kijiji bila kusubiri wafadhili au serikali.

“Tulijisahau sana, tukiamini kuwa serikali italeta kila kitu, tumejikuta tukiwa nyuma kimaendeleo sasa mambo yamebadilika. Tuliamua na wananchi wangu tuokoe watoto wetu wanaosomea nje kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule zetu tatu zilizopo katika kijiji chetu” alisema Wetare.

Mwenyekiti huyo alisema, tayari wamekamilisha vyumba viwili vya madarasa ya shule ya Kwibara A, na sasa wanaelekeza nguvu kujenga vyumba viwili katika shule ya msingi Mugane.

“Tumefanikisha ujenzi kwa kutumia mapato ya fedha za ruzuku, makusanyo ya ushuru pamoja na michango ya wananchi” alisema mwenyekiti Wetare.

Naye diwani wa kata ya Kwibara Charles Magoma alisema, ndani ya kata yake hivisasa wapo kwenye kasi ya kukalimisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya, uboreshaji na ujenzi wa shule ya sekondari Mugango.

“Kazi zote hizi za ujenzi nina uhakika zitakamilika ndani ya miezi mitatu ijayo, misaada tunayopata kutoka kwa mbunge, ni lazima tuitendee haki” alisema kwa kujiamini Charles Magoma.

 

                                                JIMBO LA MUSOMA VIJIJIJINI – UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA MASHULENI.
(1) Jumla ya S/Msingi: 111
(2) Jumla ya S/Sekondari: 20
(3) Jumla ya Vijiji: 68/Kata: 21
(4)Jumla ya Vyumba vya Madarasa vilivyopungua: 748
(5)Jumla ya Majengo yanayohitaji kuezekwa: 88

Ndugu zangu Wanavijiji na Viongozi wa ngazi zote na Washiriki wetu tunapaswa kukamilisha kazi ya ujenzi huo kwa njia ya kujitolea na kujituma sisi wenyewe.
Hakuna Kushindwa.
S Muhongo, Mbunge

UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KIGERA MBIONI KUKAMILIKA

kigera

Jengo la zahanati linaloendelea kujengwa na wananchi wa kijiji cha Kigera kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya kata na kijiji.

Na Juma Shabani

WANANCHI wa kijiji cha Kigera Etuma wapo kwenye hatua za mwisho za kumaliza jengo la zahanati ambalo wanajenga kwa michango yao na ufadhili kutoka kwa watu mbalimbali.

Diwani wa kata ya Nyakatende Rufumbo Rufumbo alisema, wananchi kwa kushirikiana na uongozi wa kata na kijiji wanapambana kwa hali na mali kukamilisha jengo hilo, ambapo kazi iliyobaki ni kupiga ripu na kuweka milango kwenye vyumba vya zahanati hiyo.

“Tunapambana na ujenzi kwa nguvu za wananchi kwa kutoa michango na kujitolea kwa kusogeza mawe, mchanga na matofali, hivyo kwa pamoja ndo maana tumefika hatua hii. Tayari hadisasa tumekamilisha choo chenye matundu manne kwa kiwango kizuri sana na tayari kipo tayari kwa kutumika” alisema diwani Rufumbo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa kijiji cha Kigera walisema, wanashukuru hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi huo na wana matumaini utakamilika na kuwapunguzia mateso waliyopata kwa miaka mingi ya kufuata huduma za afya kilomita 25 kutoka kijijini kwao.

“Nyakati za usiku tumekuwa tunateseka sana pale unapopata mgonjwa, kuna wakati unashindwa kabisa kumpeleka mgonjwa kupata matibabu, kwa ujenzi huu wa jengo hili la zahanati imekuwa ni furaha kubwa sana tunatamani hata likamilike kesho tuanze kupata huduma hapa” alisema Majura Makobha, mwananchi wa Kigera.

Hata hivyo, Makobha alimshukuru Mbunge wa Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa jitihada za kupunguza vifo vya akinamama jimboni humo kwa kupeleka gari za wagonjwa ambazo zinawasaidia kusafirisha wagonjwa kwa wakati mwafaka na kupatiwa matibabu.

“Kwa kweli mbunge wetu katusaidia sana kwa hizi gari za wagonjwa alizoleta, zimekuwa mkombozi mkubwa maana kabla ya hapo akinamama wajawazito walikuwa wanapoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma, ila sasahivi wanawahi, Mungu ampe uwezo zaidi na kutusaidia watu wa Musoma vijijini” alisema Majura Makobha.

kigera-choo

Jengo ya choo chenye matundu manne kikiwa tayari kwa matumizi.

SERIKALI YA KIJIJI, WANANCHI WAJENGA SHULE ILIYOHARIBIWA NA UPEPO

mabui

Pichani ni jengo la vyumba viwili vya madarasa na ofisi mbili za walimu wa shule ya msingi Mabui zinazojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Mabui Merafuru (Picha na Verediana Mgoma).

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wa kijiji cha Mabui Merafuru wamejitolea kushiriki katika ujenzi wa vyumba viwili  vya madarasa na ofisi mbili za walimu wa shule ya msingu Mabui.

Mtendaji wa kijiji hicho Mugeta Kaitira alisema, ujenzi huo umeanza baada ya majengo ya awali kuezuliwa na upepo na kuwalazimu wananchi kukusanya nguvu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo jipya na imara ili watoto wao waweze kuendelea na masomo.

Kaitira alisema, baada ya kupata maafa hayo shule ilipata ufadhili wa vyumba vitatu vya madarasa ya muda katika jengo la Kanisa Katoliki ambako wanafunzi wanaendelea kutumia madarasa hayo wakati wakiwa kwenye harakati za umaliziaji wa vyumba hivyo vya madarasa.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu shule ya msingi Mabui, Kimodoi Nyauri amekiri kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo hali ambayo inasababisha wanafunzi kubadilishana zamu za kuingia shuleni hapo.

“Mpaka sasa shule ina vyumba vitatu tu na vingine ni vya Kanisa ambavyo tunatumia kwa muda, endapo ujenzi utakamilika unaweza kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapa” alisema mwalimu Nyauri.

Aidha, mwalimu mkuu huyo alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa msaada waliopewa kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya maafa.

“Tunamshukuru sana mbunge kwa msaada wake ambao umetusaidia kufikia hatua ya mwisho ya ujenzi na hivi karibuni madarasa yataanza kutumika na pia imesaidia kwani tumeongeza ofisi mbili za walimu” alisema Kimodoi Nyauri.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mabui Julius Tumbo, ameeleza uhamasishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa unapokelewa vizuri na  jamii nzima kupitia vikao mbalimbali vinavyofanyika kijijini hapo.

“Kupitia mikutano yetu huwa tunahimiza wazazi kuchangia nguvu zao katika maendeleo, tunashukuru pia msaada aliotoa mbunge ambao umeendelea kuleta hamasa ya uongozi wa shule kwa kushirikiana na wananchi kujipanga katika ujenzi wa vyumba vingine  vya madarasa” alisema mwenyekiti huyo.

 

                              WANANCHI WA KIJIJI CHA SUGUTI WAANZA UJENZI WA MADARASA

Na Verediana Mgoma

WANANCHI wa kijiji cha Suguti wameanza kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Suguti ambayo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Wakati wa sherehe za nane nane zilizofanyika kijijini hapo, mwalimu mkuu wa shule hiyo Yasinta John alimuomba mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo kuwasaidia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ili kumudu idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo.

Kutokana na ombi hilo, mbunge huyo alianza kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo huku akiahidi kutoa mifuko 100 ya saruji na mabati 100 ambapo tayari ametimiza ahadi yake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa kijiji hicho Sondo Bundara, alikiri kupokea vifaa hivyo na kusema zoezi la ujenzi limeanza kwa hatua ya awali ya ufyatuaji wa matofali.

Mtendaji wa Kata ya Suguti Danford Gaudance alisema, wananchi wanaendelea kuhamasika kuchangia maendeleo kutokana na mwongozo wa mbunge wao.

“Wananchi wanachangia maendeleo kwa kuona mfano bora kutoka kwa mbunge wao na mbinu alizotumia kuwashirikisha wadau mbalimbali kama madiwani, viongozi kutoka sekta tofauti na wakazi wa eneo husika kuchangia harambee kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Suguti” alisema Gaudance.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Yasinta John alimshukuru mbunge Prof. Sospeter Muhongo kwa utekelezaji wa ahadi zake ikiwemo kuwapatia vitabu vya watoto kujifunzia, mbegu za alizeti; ambapo shule hiyo imebadili kilimo walichozoea (pamba na mahindi).

“Tunamshukuru mbunge kwa mifuko ya saruji na mabati tuliyopokea kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ametekeleza ahadi ya madawati shuleni hapa ambapo mpaka sasa shule yetu haina tena upungufu wa madawati na watoto wote wanakaa kwenye madawati” alisema mwalimu mkuu huyo.

Naye mwananchi wa kijiji cha Suguti Mussa Charles alisema, jinsi wananchi na viongozi wa kijiji hicho walivyo na mwamko wa maendeleo kuhakikisha wanamuunga mkono mbunge wao kwa hatua anazochukua katika utekelezaji wa ahadi ya kuboresha mazingira ya elimu jimboni humo.

 

SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI ZANUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA VYOO VYA KISASA
shule-45

Mafundi wakiendelea na zoezi la ujenzi wa vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Mugane.

SHULE za msingi 45 za jimbo la Musoma vijijini zimenufaika na mradi wa ujenzi wa vyoo vya kisasa unaotekelezwa na shirika lisilo la Serikali la PCI linalofadhiliwa na Wamarekani.

Ujenzi wa vyoo hivyo unaotarajia kukamilika Disemba mwaka huu, utasaidia kupunguza uhaba wa matundu ya vyoo katika shule hizo za msingi.

Akifafanua mbele ya msaidizi wa mbunge baada ya kufanya ziara katika baadhi ya shule zinazotekeleza mradi huo, Afisa Taaluma wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini, David Chombo alisema kwa awamu hii shule 45 ndio zimebahatika kupata mradi huo.

Afisa huyo ambaye pia ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo alisema, mbali na kujenga vyoo na matanki 28 ya kuhifadhia maji kwenye shule hizo, shirika hilo lina mradi mwingine wa kutoa chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi 73.

“Tunawashukuru sana PCI, wameweza kutusaidia mambo mengi, wametusaidia kutoa chakula cha wanafunzi katika shule 73 kati ya shule 111 tulizonazo, wametusaidia vifaa vya kufundishia hususani vitabu, wametusaidia vifaa vya michezo, na pia wametoa mafunzo mbalimbali kwa walimu juu ya masuala ya uongozi na mbinu za ufundishaji hali inayopelekea kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi,” alisema Chombo.

Chombo aliendelea kusema: “mradi huu utakuwa wa awamu; awamu ya kwanza ya mradi tulijenga vyoo 20, awamu ya pili tunajenga vyoo 25, hivyo basi awamu ya tatu inayotarajia kuanza mwezi Januari 2017 tutamalizia vyoo 28,”alisisitiza Chombo.

Aidha, David Chombo alisema vyoo hivyo vinajengwa kwa gharama kubwa ambapo kila choo kina matundu 10 na kinagharimu jumla ya shilingi milioni 31, hivyo aliwaomba walimu wasimamie kwa makini utunzaji wake na kuvifanyia ukarabati pindi inapotokea uhitaji.

 

WANANCHI KIJIJI CHA LYASEMBE WAJENGA NYUMBA YA WALIMU

untitled

Nyumba ya walimu wa shule ya msingi Lyasembe inayojengwa kwa nguvu za wananchi, ambapo Mtendaji wa kijiji hicho Martha John anasema, nyumba moja wanaweza kuishi walimu watatu huku Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Japhet Nyambea akikiri ujenzi huo ukikamilika utasaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa nyumba za walimu iliyopo sasa inayowalazimu walimu wengi kuishi nje ya kituo hicho cha kazi (Picha na Verediana Mgoma).

CHIRORWE WAANZA UJENZI WA ZAHANATI, WAOMBA MSAADA

chirorwe-2

UONGOZI wa kijiji cha Chirorwe, Halmshauri ya Musoma vijijini kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kujenga zahanati kwa lengo la kusogeza karibu huduma za afya.

Mtendaji wa kijiji hicho Rahabu Mahanga amesema, awali wananchi hao walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata zahanati iliyokuwa mbali na kijiji chao.

Mtendaji huyo alisema wakikamilisha ujenzi huo, itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Chirorwe hasa watoto, akinamama wajawazito ambao hadisasa wanalazimika kupata huduma za kujifungua, matibabu na kliniki kwenye kijiji cha jirani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Msai Maingu aliomba msaada wa kumalizia ujenzi huo kwa wadau mbalimbali ili kuondoa hadha ya wakazi wa kijiji hicho kuwa mbali na huduma za afya.

“Sisi viongozi tunaendelea kusisitiza na kuhamasisha maendeleo kijiji hapa na kwa kweli mpaka sasa tunaendelea vizuri na tunapiga hatua kubwa kimaendeleo” alisema mwenyekiti Maingu.

WANANCHI WAENDELEA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA MSINGI BUKWAYA

bukwaya

Pichani ni vyumba vitatu vya madarasa vilivyokamilika na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bukwaya.

Na Juma Shabani.

WANANCHI wa kijiji cha Kurukerege kitongoji cha Esira kata ya Nyegina, wanaendelea kuchangia ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu mkuu katika shule ya msingi Bukwaya.

Mwalimu mkuu wa shule ya hiyo, Rutolio Hitira akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, shule ya msingi Bukwaya ni mpya katika jimbo la Musoma vijijini iliyopata usajili mwaka huu 2016 ina wanafunzi wa darasa la kwanza 135, na wanafunzi wa awali 36, hivyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa madarasa.

“Shule hii tumeianzisha ikiwa na chumba kimoja cha darasa tulilokuwa tunatumia kama darasa la awali, lakini kwa juhudi za wananchi wa kitongoji cha Esira waliamua kufanya harambee na kuanza ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu mkuu” alisema mwalimu Hitira.

Mwalimu huyo alisema, tayari vyumba hivyo na ofisi ya mwalimu ipo kwenye hatua nzuri na kilichobaki sasa ni uwekaji wa milango, kupiga ripu, sakafu na madirisha.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Esira, Msiru John alisema watahakikisha wanajitoa kwa hali na mali kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika.

“Tunataka kuona shule hii inakuwa na mwonekano mzuri kama shule nyingine, maana watoto wetu walikuwa wanapata shida sana kutokana na kutembea umbali mrefu takiribani kilomita 6 kufika kwenye shule iliyo mbali na hapa, hivyo tunahakikisha tunasimamia vizuri michango ya wananchi na kuendelea kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa shule yetu” alisema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wa kitongoji alimshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo na wasaidizi wake kwa kuwafikishia mgao wa madawati na vitabu na kuahidi kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo watapambana kuhakikisha wanasukuma mbele gurudumu la maendeleo.

UJENZI WA OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI CHA MWIRINGO WAFIKIA HATUA NZURI

2

Mtendaji wa kijiji cha Mwiringo Abeid Ndagara akiwa amesimama mbele ya jengo la ofisi ya kisasa inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo mtendaji huyo anasema wamefikia hatua hiyo baada ya kuhamasisha wananchi kuchangia na kujitolea kupitia mikutano ya hadhara.

WAKULIMA WA BUSTANI ZA MBOGA NA MATUNDA WAONGEZEKA MUSOMA VIJIJINI

 

 

untitled-1

Baadhi ya wakulima wa kikundi cha Jitume Ufanikiwe kushoto ni Mwita Mayega na kulia ni Boazi Tore wakiwa katika moja ya bustani zao.

Na Ramadhani Juma

BAADA ya Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kuhamasisha kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda, idadi ya vikundi vya wakulima inazidi kuongezeka.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia vikundi mbalimbali katika Kata ya Busambara vikiwa kwenye harakati za kutunza bustani zao za vitunguu, nyanya, kabichi na matikiti maji ambapo vingine vinatajwa kuwa ni vikundi vipya.

“Tumejifunza mengi kutoka kwa wenzetu walioanza kilimo hiki, yaani kikundi kilichopata msaada kupitia mfuko wa jimbo, wao walilima vitunguu takribani ekari moja na nusu, na kupata zaidi ya milioni tatu ndani ya miezi mitatu na nusu. Hayo ni mafanikio makubwa sana. Hakika bidii ndiyo nguzo ya mafanikio” alisema Mwita Mayegi aliyejitambulisha kuwa ni mkulima mpya wa bustani.

Pamoja na juhudi hizo, vijana hao wamebainisha changamoto wanazopambana nazo kuwa ni ukosefu wa pampu za umwagiliaji, bei kubwa ya mbegu pamoja na madawa ya kunyunyuzia mazao yao ili yasishambuliwe na wadudu waharibifu.

“Tunatumia muda mwingi kumwagilia bustani zetu kwani tunasomba maji kwa ndoo, tunaanza kumwagilia saa kumi na mbili alfajiri na kumaliza saa sita mchana. Tunamuomba mbunge wetu atusaidie pampu za umwagiliaji ili turahisishe kazi yetu na kuokoa muda” alisema Boazi Tore mkulima mwingine mpya wa kilimo cha bustani.

Naye Maiga Masatu alisema: “tunapata shida kubwa kipindi hiki cha mvua kwani unaweza kumaliza kunyunyuzia dawa na mvua inanyesha muda huo, hivyo dawa haifanyi kazi. Hali hii inatulazimu kununua dawa nyingine ambazo nazo bei yake ipo juu”

Hata hivyo, wanakikundi hao walimshukuru Afisa kilimo wa kijiji hicho Masinde Muyengi kwa msaada mkubwa anaowapatia katika shughuli zao za kila siku.

“Afisa kilimo amekuwa akitutembelea mara kwa mara, kutuelekeza aina ya mbegu inayofaa, na aina ya madawa yanayostahili kuwekwa kwenye mazao yetu” alisema Nyamisi Mafuru.

Kikundi hicho cha  Jitume Ufanikiwe chenye jumla ya wanachama 10, kwasasa wamelima bustani ya nyanya yenye miche 10544, bustani ya kabichi yenye miche 2068 na bustani ya matikiti maji yenye miche 3256.

Hadisasa zaidi ya vikundi 104 vinajishughulisha na kilimo cha bustani za mboga na matunda ndani ya jimbo la Musoma vijijini ikiwa ni juhudi za mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo kutaka kuinua uchumi wa jimbo kwa kuhamasisha wananchi wake kujituma katika kufanya kazi.

KABURABURA WAONGEZA VYUMBA VYA MADARASA

untitled

Moja ya majengo yanayojengwa na wananchi wa kijiji cha Kaburabura.

 

Na Hamisa Gamba

KUTOKANA na uhaba wa vyumba vya madarasa, wananchi wa kijiji cha Kaburabura kata ya Bugoji  wamehamasishwa kujitolea kushiriki katika shughuli za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Kaburabura A.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Matoke Gaya alisema, shule yao ina vyumba vitatu vya madarasa na iwapo watafanikiwa kumaliza ujenzi huo unaoendelea, watakuwa wamebaki na upungufu wa vyumba viwili vya madarasa.

“Kwa kuwa watoto wana kiu ya kukaa ndani ya darasa, watoto hao wameanza kuhamisha madawati kutoka kwenye miti ambayo wanaitumia kama darasa kufundishiwa na kulitumia jengo hilo kujisomea wakati wa asubuhi” alisema mwalimu Gaya.

Naye diwani wa kata ya Bugoji Ibrahimund Malima alisema amejipanga kufanya kazi kuhakikisha ifikapo mwakani, kero ya wanafunzi kukaa nje itakuwa imekwisha huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kuondoa aibu hiyo.

Wakati huo huo, wananchi wa kijiji cha Kanderema wamekamilisha ujenzi wa msingi kwa ajili ya vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Kanderema B.

VIJANA NYAMBONO WACHANGAMKIA KILIMO CHA BUSTANI 

naymbono

Vijana wa moja ya vikundi vya kilimo cha bustani wakiwajibika

Na Hamisa Gamba

VIJANA wa kijiji cha Nyambono wameungana na vijana wa maeneo mengine ya jimbo la Musoma vijijini kujishughulisha na kilimo cha bustani ili kujikwamua kiuchumi.

Vijana hao ambao wengine wamejiunga kwenye vikundi ambavyo ni mbali na vile vinavyofadhiliwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo, wamehamasika na kilimo cha bustani baada ya kusikia vijana wenzao wameanza kuvuna na kuuza mazao yao.

Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kilimo cha bustani Ibrahim Felesian alisema, vijana wote hawana budi kuwajibika mashambani katika mazao ya chakula na biashara badala ya kurandaranda mitaani bila mwelekeo.

“Sisi tunajishughulisha na kilimo hiki takribani miaka miwili sasa, japo mwanzoni wenzangu walianza kutawanyika wakiona kazi hii ni ngumu, lakini baadaye wamerudi na kuendelea kujumuika pamoja na sasa wana mafanikio” alisema Felesina na kuongeza kuwa, kabla ya kuanza shughuli hiyo wengi walikuwa hawana ajira na walikuwa wakizurura hovyo mitaani.

Kijana huyo aliwahimiza vijana wa jimbo hilo na maeneo mengine nchini kujikusanya kwenye vikundi na kufanya kilimo badala ya kukaa mitaani na kufanya mambo ambayo hayana faida kwao.

“Vijana wajishughulishe, pia wasikae wakisubiri tu misaada, ni lazima waanze kujituma na kuwajibika wenyewe kisha watawezeshwa” alisema Ibrahim Felesian.

              UJENZI WA VYOO VYA SHULE YA MSINGI MURANGI WAANZA

murangi

Pichani ni uongozi wa shule ya Msingi Murangi na uongozi wa kijiji wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya shule Mfungo Magoti, wengine ni Mwalimu Maburuki Matiko, na Mwenyekiti wa kijiji cha Murangi Hamisi Nyamamu. (Picha na Verediana Mgoma).

Na Verediana Mgoma

WANANCHI wa kata ya Murangi wamejitolea katika ujenzi wa vyoo unaoendelea kwenye shule ya msingi Murangi ili kuwaepusha watoto wao na magonjwa ya miripuko.

Wananchi hao tangu ulipoanza ujenzi huo, wameonekana wakizoa mchanga, wakichota maji na kumwagilia msingi ambao umejengwa.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wananchi hao wamesema wapo tayari kushiriki katika suala la maendeleo hasa katika upande wa elimu kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Hamisi Nyamamu alisema, wamejiwekea mikakati ya kufanikisha zoezi la maendeleo ya kata ya Murangi ikiwemo kusimamia ujenzi wa vyoo vyote vilivyopo mashuleni, zahanati na majumbani ili kuepukana na magonjwa hatarishi.

“Mpaka sasa zoezi linaendelea vizuri na tumejipanga kuendelea na maendeleo mengine kwa kushirikiana na wananchi wangu, ila jambo kubwa tunalojitahidi kulifanya ni kuhakikisha wananchi wetu wanaepuka magonjwa ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao au kuwakwamisha katika shughuli za kutafuta maendeleo” alisema Hamisi Nyamamu.

KIJIJI CHA SARAGANA WAANZA UJENZI WA SOKO JIPYA

saragana

Moja ya majengo ya soko jipya la kijiji cha Saragana linalojengwa kwa ushirikiano wa wananchi na serikali yao ya kijiji ambapo ujenzi huo unaendana na ujenzi wa stendi ya mabasi.

Na Hamisa Gamba

WANANCHI wa kijiji cha Saragana wameanza ujenzi wa soko jipya la kijiji hicho kwa ajili ya kufanyia shughuli zao za biashara ikiwemo kuuza mazao wanayozalisha.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Leni Manyama alisema, ujenzi wa soko hilo unakwenda sambamba na ujenzi wa stendi ya mabasi na wananchi wake wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa uongozi wa kijiji hicho.

“Wananchi wamehamasika kuhakikisha wanapata soko jipya na stendi ya mabasi ambayo itawasaidia kibiashara na hata katika kurahisisha masuala ya usafiri wa kuingia kijijini na kutoka” alisema Manyama na kuongeza kuwa, muingiliano huo utasaidia kukuza uchumi wa kijiji hicho na kata nzima ya Nyambono.

Naye mtendaji wa kijiji hicho Muyejanda Kalidushi alipongeza ushirikiano huo wanaotoa wananchi wa Saragana katika jitihada za kupata soko jipya na kuwataka kuendelea kujitolea kwa hali na mali bila kuchoka hadi watakapokamilisha ujenzi huo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyambono alisema, sambamba na juhudi hizo za ujenzi wa soko jipya katika kijiji hicho, wanatarajia kukamilisha zoezi la ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Nyambono ili kuboresha elimu ya masomo ya sayansi shuleni hapo.

Hata hivyo, diwani huyo amewaasa wananchi kujishughulisha kutafuta maendeleo ili kuboresha huduma za nyanja zote katika kata hiyo.

TEGERUKA WAJENGA VYUMBA 10 VYA MADARASA

tegeruka

Baadhi ya vyumba vya madarasa vikiendelea kwenye hatua mbalimbali ya ujenzi katika kata ya Tegeruka

Na Ramadhani Juma

ZAIDI ya vyumba 10 vya madarasa vimejengwa na wananchi wa kata ya Tegeruka katika shule ya msingi Nyaminya, Tegeruka na Kataryo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi mbele ya kikao na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, diwani wa kata ya Tegeruka Benjamin Maheke alisema, vyumba hivyo vimejengwa kwa siku tatu na kuwapongeza wananchi wa kata hiyo kwa jinsi walivyoamua kupambana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa.

“Wananchi wangu wamejitolea kwa hali na mali, wamechangia fedha pamoja na matofali, pamoja na hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo, lakini wameona elimu kwa watoto wao ni bora kuliko njaa ya muda mfupi” alisema diwani huyo.

Diwani Maheke aliongeza: “Hadi sasa shule zangu zimepokea madawati zaidi ya 400 kutoka kwa mheshimiwa Mbunge. Tunashukuru sana kwa msaada huo wa madawati kwani vijana wetu wamekaa chini kwa muda mrefu.

Tutaonekana watu tusio na akili pindi tutakapo tunzia madawati hayo nje, tumejipanga kuhakikisha tunakamilisha ujenzi huo ndani ya mwezi wa tisa na ikiwezekana zoezi la upauwaji lifanyike mwezi wa kumi”

Hata hivyo, diwani huyo mbali na kupongeza jitihada za mbunge wa Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo katika kuinua elimu, aliomba ofisi yake na ofisi ya Mkurugenzi wilaya iwaongezee nguvu katika ukamilishaji wa vyumba hivyo.

WANANCHI MUSANJA WAANZA UTEKELEZAJI MRADI WA CHOO

musanja

Wananchi wa kijiji cha Musanja wakiwa kwenye shughuli za ujenzi wa choo cha shule ya msingi Musanja ambao ni mradi wa Halmashauri ya Musoma vijijini, mradi huo ni wa ujenzi wa matundu nane ya choo (manne ya wasichana na manne wavulana). Mbele aliyebeba tofali ni Mtendaji wa Kijiji hicho DoricaTongoro (Picha na Verediana Mgoma).

 

KIKUNDI CHA ANGAZA WAELEKEA MSIMU WA MAVUNO

angaza

Baadhi ya wanakikundi wa kikundi cha Angaza wakiendelea na shughuli za utunzaji wa bustani yao. Kushoto ni Katibu wa kundi hicho Biseko Mkaka akiwa na Mwenyekiti wake Chamba Daudi (Picha na Fedson Masawa)

Na Mwandishi Wetu

KIKUNDI cha Angaza ambacho ni moja ya vikundi 15 vilivyonufaika na fedha za mfuko wa jimbo la Musoma vijijini chini ya usimamizi wa Mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo, kipo kwenye hatua za mwisho kuvuna mazao waliyopanda.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizo aliyefika shambani hapo, wanachama wa kikundi hicho ambacho kipo kwenye kijiji cha Buraga kata ya Bukumi, wamesema wana matumaini ya kuinua hali zao kiuchumi kutokana na kilimo chao cha mbogamboga na matikiti.

Wanakikundi hao akiwemo mwenyekiti wao Chamba Daudi wamesema, kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, bustani ya matikiti maji yenye idadi ya mashina 2000 itakuwa tayari imekomaa na zoezi la uvunaji litaanza kwa ajili ya kutafuta soko.

“Kwa hapa tulipofikia, tunatarajia mwishoni mwa mwezi huu wa tisa tutakuwa tunaanza kuvuna kwani bustani imefikia hatua nzuri”  alisema Daudi.

Wakizungumzia changamoto za kilimo hicho, wanakikundi hao walisema changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia mazao yao.

“Siku tuliyoenda kukabidhiwa vifaa vya kikundi tulipewa mbegu, mipira na mashine. Dawa tulihoji tukajibiwa kwamba nendeni dawa mtatumiwa kwenye vikundi vyenu wala msisumbuke kurudi huku mjini. Hadi leo hatujaziona dawa na hatujui ni lini tutazipata” alisema Nyamisi Matoto.

Matoto aliendelea kusema: “Pamoja na changamoto hizo hatuwezi kusita kufanya linalowezekana shambani na sasa tunajishika sisi kama kikundi na kununua dawa ya kutusaidia panapowezekana. Tunachoomba sasa ni kutusaidia ninyi viongozi kwani pale Suguti fedha zilizoelekezwa kwenye vikundi Mbunge wetu alisema zitanunua mashine, mbegu, mipira na madawa kwa kila kikundi. Hivyo dawa hizo kama zipo tuzipate”

Hata hivyo, kikundi hicho kimeeleza matarajio yao ya baadae kuwa ni kulima nyanya baada ya mavuno matikiti maji.

“Sisi kama wanakikundi tunatarajia baada ya kuvuna na kuuza tikiti tuanze kulima nyanya za kutosha. Kama alivyosema mwenzetu basi tuweze kutimiziwa tulichoahidiwa ili dawa hiyo angalau itusaidie kwenye nyanya” alisema Mabure Mbogora.