HARAMBEE IMEFANIKIWA SANA: KISIWA CHA RUKUBA CHAANZA UJENZI WA SEKONDARI YAKE

Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Etaro. Wanafunzi wa sekondari kutoka Kisiwani humo wanasoma nchi kavu kwenye sekondari ya Kata yao (Etaro Sekondari).

Wanafunzi hao wanakumbuna na matatizo mengi mno ambayo yanadhoofisha sana maendeleo yao kielimu. Kwa hiyo, wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kujenga sekondari yao Kisiwani humo.

Harambee yenye mafanikio makubwa
Harambee iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini siku ya Jumatano, 27.9.2023 ilishirikisha Viongozi wote wakuu wa Wilaya ya Musoma na Halmashauri yake (Musoma DC).

Wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakiwemo Walimu Makada ya CCM walishiriki. Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM nayo ilishiriki - ilikuwa ni Harambee ya kipekee kufanyika Kisiwani humo!

Michango iliyopatikana kwenye Harambee hiyo
*Wakazi na Wazaliwa wa Kisiwa cha Rukuba:
Saruji Mifuko 167
*Kamati ya Siasa ya Kata (CCM):
Saruji Mifuko 22
*Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM):
Saruji Mifuko 15
*DED na wenzake: Saruji Mifuko 20
*DC na wenzake: Saruji Mifuko 62
*Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200
*Fedha taslimu: Tsh 248,000
(zikiwemo Tsh 105,000 za Walimu Makada wa CCM)

Karibuni tujenge Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini.

Furaha & Shauku ya ujenzi wa Sekondari Kisiwani Rukuba
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO ya kutoka Kisiwani Rukuba iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 30.9.2023