SERIKALI YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANAVIJIJI KWENYE UJENZI WA VITUO VIPYA VYA AFYA VYA MUSOMA VIJIJINI

Ujenzi unaoendelea wa Kituo kipya cha Afya cha Kata ya Makojo kinachojengwa Kijijini Makojo.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68, lina Kata 3 zenye Vituo vya Afya vinavyofanya kazi. Vituo hivyo ni vya:

*Murangi
*Mugango
*Bugwema

Serikali inaendelea kutoa fedha kwenye ujenzi wa Vituo vipya vya Afya, ambavyo ni:

*Kisiwa cha Rukuba
*Makojo
*Kiriba

Kwenye ujenzi huo, Serikali ilitoa Tsh 250m kwa kila Kituo kuanza ujenzi wake.

Serikali imetoa tena Tsh 250m kuendeleza ujenzi wa Vituo hivyo vipya. Fedha hizo za awamu ya pili zitapelekwa kwenye Kata husika siku chache zijazo.

Mchango wa Tsh 500m kwa kila Kituo Kipya kinachojengwa Jimboni mwetu ni mchango mkubwa. Tunaishukuru sana Serikali yetu na kipikee kabisa tunamshukuru sana Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha fedha za utekelezaji wa miradi hii na mingine zinapatakina – Ahsante sana!

Jumla ya ZAHANATI zinazotoa huduma za Afya Jimboni mwetu ni:

*22 za Serikali
*4 za Binafsi

Jumla ya ZAHANATI mpya zinazojengwa ni:

*15 zinajengwa na WANAVIJIJI na baadhi zimepokea
michango ya fedha kutoka Serikalini.

MICHANGO ya NGUVUKAZI za WANAVIJIJI inaombwa iendelee kutolewa hadi kukamilika kwa ujenzi wa VITUO VIPYA VYA AFYA na ZAHANATI zinazojengwa.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 12.6.2022