KISIWA CHA RUKUBA KUSHIRIKI SHEREHE ZA CCM

WAKAZI wa KISIWA cha RUKUBA wakishiriki katika kusomba SARUJI iliyonunuliwa Musoma Mjini na kusafirishwa hadi Kisiwani humo.

Kesho, tarehe 5.2.2022 BOTI KUBWA 2 za kuchukua ABIRIA 80 zitaondoka Kisiwani Rukuba saa 10 alfajiri kuleta WAWAKILISHI wao kwenye sherehe za CCM zitakazofanyika Musoma Mjini.

Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji 3 vya Kata ya Etaro ya Jimbo la Musoma Vijijini.

WAKAZI wa Kisiwa cha Rukuba wanaendelea kutoa SHUKRANI nyingi sana kwa RAIS wao, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia SHILINGI MILIONI 250 kujenga Kituo cha Afya kisiwani humo.

UJENZI umeanza na WAKAZI wa Kisiwani humo wamechangia ifuatavyo:

(i) NGUVUKAZI:
*wanasomba mawe, kokoto na maji ya ujenzi. Vilevile, wanachimba misingi ya majengo yote.

(ii) SERIKALI YA KIJIJI/KISIWA
*Imetumia mapato yake kununua vifaa vya kutumiwa kwenye ujenzi – pump 2 za kuvutia maji kutoka Ziwani na mipira yake, mapipa ya kutunzia maji ya ujenzi.

FEDHA za UVIKO/IMF:
Fedha ziko kwenye Akaunti ya Zahanati yao na tayari zimeanza kutumika kununua:

*Saruji Mifuko 599
*Nondo 210
*Mbao 32 za 1×8
20 za 2×2
*Dawa ya kuua mchwa

TAARIFA hiyo hapo juu imetolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa, Ndugu Japhari Ibrahim Kabasa

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
4.2.2022