PROF MUHONGO ATEMBELEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA

ugeni wa Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwenye Tegeruka Sekondari ya Kata ya Tegeruka.

 
 Jumatano, 19.1.2022 Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alitembelea TEGERUKA SEKONDARI akifuatilia:
 
*Wanafunzi waliokwisha fika shuleni hapo kuanza Masomo ya Kidato cha kwanza (2022)
 
Wanafunzi 54 kati ya 184 tayari wameanza masomo ya Kidato cha Kwanza. Leo ni siku ya tatu toka shule ifunguliwe. Prof Muhongo amepiga PICHA na Wanafunzi hao wa Kidato cha Kwanza – baadhi ya Wazazi na Walimu wako kwenye picha hiyo (kiambatanisho)
 
*Ujenzi wa Miundombinu kwenye Sekondari hiyo:
 
(i) Tegeruka Sekondari ilikuwa ya kwanza, ndani ya Jimbo letu, kukamilisha ujenzi wa VYUMBA VIPYA 3 vya MADARASA kwa kutumia fedha za UVIKO 19/IMF zilizopatikana kwa juhudi za Mhe Rais Samia Sukuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SHUKRANI NYINGI SANA kwa Mhe Rais wetu.
 
(ii) Sekondari haina MAABARA na MAKTABA. Mbunge wa Jimbo amekubali kutoa MICHANGO kwa kushirikiana na WANAVIJIJI wa KATA ya TEGERUKA kuanza mara moja ujenzi wa MAABARA 3 za masomo ya SAYANSI (Physics, Chemistry & Biology).
 
TEGERUKA SEKONDARI inahudumia VIJIJI 3, Kataryo, Mayani na Tegeruka. Ina jumla ya WANAFUNZI 509 na WALIMU 12, wakiwemo 5 wa Masomo ya Sayansi.
 
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
19.1.2022