ELIMU NI KIPAUMBELE MUHIMU SANA CHA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – VITONGOJI VYAAMUA KUJENGA SHULE SHIKIZI

Ujenzi wa SHULE SHIKIZI ya KITONGOJI cha BURAGA MWALONI, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
TAKWIMU MUHIMU:
Jimbo la Musoma Vijijiji lina:
*Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
*Shule za Msingi 111 za Serikali
*Shule za Msingi 3 za Binafsi
*Sekondari 21 za Kata/Serikali
*Sekondari 2 za Binafsi
*High School 1 ya Serikali ya Masomo ya “Arts”
MATATIZO YANAYOTATULIWA KWENYE SEKTA YA ELIMU
WANAVIJIJI wakishirikiana na SERIKALI, na WADAU mbalimbali wa MAENDELEO wanaendelea kutatua matatizo yafuatayo:
*Umbali mrefu wa Wanafunzi kutembea waendapo masomoni.
*Mirundikano ya Wanafunzi kwenye Vyumba vya Madarasa
UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
MIRADI inayoendelea Jimboni mwetu:
*Ujenzi wa Maabara 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia kwenye Sekondari zote 21 za Kata/Serikali
*Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa, Maktaba, Ofisi za Walimu, Vyoo na Nyumba za Walimu kwenye shule zetu.
*Ujenzi wa Sekondari  mpya 12. Hatua mbalimbali zimefikiwa
*Ujenzi wa Shule Shikizi 12, ambazo zitapanuliwa na kuwa Shule za Msingi zinazojitegemea.
KITONGOJI CHA BURAGA MWALONI CHAANZA UJENZI WA SHULE SHIKIZI
KITONGOJI cha Buraga Mwaloni kipo Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi. Kata hii inavyo Vijiji vingine vitatu (Bukumi, Buira na Busekera)
KIJIJI cha Buraga kina Shule moja ya Msingi (S/M Buraga) ambayo ina:
*Wanafunzi 690
*Walimu 10
*Vyumba 8 vya Madarasa
*Ilifunguliwa Mwaka 1978
Hayo yameelezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,  Mwl Joseph Paul
WANAFUNZI wa  Kitongoji cha Buraga Mwaloni WANALAZIMIKA kutembea zaidi ya KILOMITA 5 kwenda masomoni kwenye S/M BURAGA. Vichaka vyenye wanyama wakali ni hatari kubwa kwa Wanafunzi!
Wengine wanatembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M CHITARE ya Kijiji cha jirani cha Chitare cha Kata jirani ya Makojo.
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni, Ndugu Steven Wanjara ameeleza kuwa KITONGOJI KIMEAMUA kujenga SHULE SHIKIZI yake na MICHANGO ya ujenzi inatolewa kama ifuatavyo:
WANAKITONGOJI:
*Nguvukazi za kuchimba msingi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
*Nguvukazi  za kusomba mawe, mchanga na maji
*Fedha taslimu, Tsh 19,300/= kutoka kila Kaya
DIWANI WA KATA:
Mhe Munubi Musa ameanza kutoa MICHANGO yake kwa kuchangia Tsh 100,000/= (laki moja)
MBUNGE WA JIMBO:
Prof Sospeter Muhongo ameanza kwa kuchangia:
*Saruji Mifuko 55
*MFUKO wa JIMBO umechangia Saruji Mifuko 50.
OMBI LA MICHANGO linatolewa na Kitongoji cha Buraga Mwaloni kisaidiwe VIFAA vya UJENZI kukamilisha SHULE SHIKIZI yake – Wanafunzi 40 wa Darasa la Awali wanasomea chini ya miti. HALMASHAURI yetu nayo inapaswa kuchangia ujenzi huu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini