UJENZI NA UBORESHAJI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI VYAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA MASOMO HAYO

Mkuu wa Shule & Diwani wakiwa ndani ya Maabara ya Biolojia

Tarehe 7.8.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
*MALENGO YETU:
(i) SEKONDARI zote 21 za Kata/Serikali za Jimbo la Musoma Vijijini ziko kwenye UJENZI & UBORESHAJI wa MAABARA 3 za  Masomo ya FIZIKIA, KEMIA na BIOLOJIA.
Kazi hiyo imepangwa ikamilike kabla ya Disemba 2022.
(ii) SEKONDARI 2 za Binafsi (Kanisa Katoliki & SDA) nazo zimeshawishiwa kufanya hivyo
(iii) SEKONDARI 10 mpya zinazojengwa au zitakazoanza kujengwa hivi karibuni zitakuwa na MAABARA hizo 3 & MAKTABA
(iv) SEKONDARI zilizokamilisha ujenzi na uboreshaji wa MAABARA hizo 3 zianze matayarisho ya kuwa na “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya SAYANSI
(v) KAMPENI maalumu zianzishwe za kushawishi na kuvutia WANAFUNZI kupenda kusoma MASOMO ya SAYANSI
*RUSOLI SEKONDARI
Sekondari hii ni ya Kata ya Rusoli. Ilifunguliwa Mwaka 2010 kuhudumia Wanafunzi wa kutoka Vijiji 3 (Buanga, Kwikerege na Rusoli) vya Kata hii.
MKUU wa Sekondari ya Rusoli, Mwl Tausi Juma ameeleza yafuatayo kuhusu Shule hii:
(i) Ina Wanafunzi 444
(ii) Mahitaji ya Walimu ni 15,  waliopo ni 13 na kati ya hao 6 ni wa Masomo ya Sayansi
(iii) Ina MAABARA 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia
(iv) Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 12, vilivyopo ni 10
UJENZI & UBORESHAJI WA MAABARA ZA RUSOLI SEKONDARI
Ujenzi na uboreshaji wa MAABARA hizi unashirikisha:
*Serikali
*Wanavijiji (NGUVUKAZI)
*Wazaliwa wa Kata ya Rusoli
*Mbunge wa Jimbo
MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI
MKUU wa Rusoli Sekondari, Mwl. Tausi Juma ameeleza kuwa Serikali kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa:
(i) SHILINGI MILIONI 30 kwa ajili ya:
*ukamilishaji wa Maabara ya FIZIKIA na samani zake
*ujenzi wa TENKI la  kuvunia maji ya mvua ya kutumia kwenye Maabara
*kukamilisha uwekaji wa mfumo wa gesi na umeme kwenye Maabara.
(ii) SHILINGI MILIONI 25 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara ya KEMIA
(iii) VIFAA vya Maabara vilitolewa na TAMISEMI
*Inakadiriwa kwamba Asilimia 75 (75%) ya Wanafunzi wa Kidato vya I & II wa RUSOLI SEKONDARI  wamehasika na kuvutiwa sana na MASOMO ya SAYANSI ya VITENDO (practicals) kwenye MAABARA zao.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHATOLEWA RUSOLI SEKONDARI
(i) WAZALIWA wa Kata ya Rusoli kupitia Kikundi chao kiitwacho, “YEBHE CHIKOMESHE” kimetoa MICHANGO MINGI kwenye Sekondari hii ikiwemo ya VIFAA vya MAABARA, COMPUTER, PRINTER & PHOTOCOPY
Kikundi hiki kinaongozwa kwa umahiri mkubwa na Ndugu JEFF MAKONGO.
Vilevile, “Yebhe Chikomeshe” kimejenga NYUMBA (two in one) ya WALIMU wa Sekondari hii.
Kimechimba KISIMA cha MAJI kwa matumzi ya Kijiji cha Rusoli. – AHSANTE SANA SANA “YEBHE CHIKOMESHE” – Kikundi cha Maendeleo yanayoonekana!
(ii) MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amechangia:
*Saruji Mifuko 70
*Posho ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi
*Vitabu zaidi ya 2,000 vya Maktaba
DIWANI wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeula na Viongozi wengine wa Kata na Vijiji wanaendelea kutoa SHUKRANI NYINGI SANA kwa MICHANGO & MISAADA wanayopokea kutoka SERIKALINI na kutoka kwa WADAU wengine wa MAENDELEO ya Kata yao, hasa kutoka kwa Mbunge wao wa Jimbo, na Kikundi cha, “Yebhe Chikomeshe.”
UFAULU WA MITIHANI WA RUSOLI SEKONDARI
*MATOKEO YA KIDATO CHA II (2020)
Watahiniwa: 107
Div I= 6     Div II= 9
Div III=26   Div IV =66
*MATOKEO YA KIDATO CHA IV (2020)
Watahiniwa: 64
Div I= 1     Div II= 6
Div III= 7   Div IV= 44
Div 0= 6
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini