SHULE YA MSINGI KAMBARAGE YAENDELEA KUJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YAKE YA ELIMU

ujenzi wa Vyumba vipya viwili vya Madarasa na Ofisi moja ya Walimu unaoendelea kwenye S/M KAMBARAGE ya Kijijini Kakisheri, Kata ya Nyakatende.

Tarehe 31.7.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI KAMBARAGE iko Kijijini Kakisheri, Kata ya Nyakatende.
KIJIJI cha Kakisheri kina jumla ya KAYA 542 na Wakazi wake ni 1,047. Kijiji hiki kina shule moja tu ya Msingi (S/M Kambarage) iliyofunguliwa Mwaka 2001.
MWALIMU MKUU wa S/M Kambarage, Mwl Gerlad Wanyaka ameelezea yafuatayo kuhusu Shule hii:.
*Jumla ya Wanafunzi ni 710.
*Idadi ya Walimu wanaohitajika ni 15, waliopo ni 7
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 16, vilivyopo ni 8
*Idadi ya matundu ya CHOO yanayohitajika ni 22, yaliyopo ni 15
*Nyumba za Walimu zinazohitajika ni 15, zilizopo ni 3.
*Mirundikano ya Wanafunzi Madarasani ni mikubwa, mifano:
(i) Wanafunzi 121 wa Darasa la Awali wanatumia chumba kimoja cha darasa
(ii) Wanafunzi 112 wa Darasa la VI  wanatumia chumba kimoja cha darasa.
MICHANGO YA WANAKIJIJI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VIPYA 2 VYA MADARASA NA OFISI 1 YA WALIMU
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kakisheri, Ndugu Maridadi Magafu ameeleza yafuatayo kuhusu ushiriki wa WANAKIJIJI kwenye ujenzi huo:
*WANAKIJIJI:
(i) kuchimba Msingi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
(ii) kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi
(iii) Michango ya FEDHA taslimu SHILINGI 4,200/= kutoka kwa kila MKAZI wa Kijiji hicho mwenye umri wa zaidi ya miaka 18.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHATOLEWA KWENYE S/M KAMBARAGE
*MBUNGE wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo ameshachangia:
(i) Madawati 100
(ii) Saruji Mifuko 60
(iii) Mabati 54
(iv) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO WA JIMBO
(v) Saruji Mifuko 100
*MDAU wa MAENDELEO, Ndugu Mauza Nyakirang’anyi, alichangia MBAO za KUPAUA Chumba 1 cha Darasa.
UFAULU WA MITIHANI WA S/M KAMBARAGE
*MATOKEO Darasa la IV (2020)
Watahiniwa: 86
Waliofaulu: 82
*MATOKEO Darasa la VII (2020)
Watahiniwa: 50
Waliofaulu: 49
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA KAKISHERI
*UONGOZI na WANAKIJIJI wanatoa wito kwa WAZALIWA wa Kijiji cha Kakisheri na Kata ya Nyakatende kwa ujumla wake, na WADAU wengine wa MAENDELEO kujitokeza kuchangia ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye S/M KAMBARAGE – karibuni tuendelee kumuenzi BABA wa TAIFA kwa pamoja.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini