WANAKIJIJI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUONGEZA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE S/M BULINGA

MATUNDA ya USHIRIKIANO wa WANAKIJIJI na SERIKALI kwenye ujenzi na ukamilishaji wa Vyumba vipya 3 vya Madarasa na Choo chenye Matundu 6 kwenye S/M BULINGA B ya Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI BULINGA B ilifunguliwa Mwaka 2014. Shule hii ipo Kijiji cha Bugunda, Kata ya Bwasi.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwalimu Marwa James ameelezea yafuatayo kuhusu Vyumba vya Madarasa vya Shule hiyo:
*Idadi ya Wanafunzi ni 672
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 15, vilivyopo ni 6.
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa. Kwa mfano, Darasa la IV lina Wanafunzi 145 kwenye chumba kimoja cha darasa.
MCHANGO WA SERIKALI WA KUTATUA TATIZO LA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA
Serikali kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa Tsh MILION 65.5 kwa ajili ya ujenzi wa:
*Vyumba vipya 3 vya Madarasa
*Choo chenye Matundu 6
*Ununuzi wa Madawati 69
*Ununuzi wa Matenki 3 ya Maji
MTENDAJI KATA wa Kata ya Bwasi,  Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAKIJIJI wameshiriki vizuri sana kwenye MRADI huu kwa kufanya yafuatayo:
*kuchimba msingi wa Vyumba vipya 3 vya Madarasa
*kuchimba shimo la choo
*kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi
VIONGOZI na WANAKIJIJI wa Kijiji cha Bugunda wanaishukuru sana SERIKALI kwa mchango wake ambao utapunguza tatizo la uhaba wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule ya Kijijini mwao.
MICHANGO MINGINE ILIYOTOLEWA KWENYE S/M BULINGA B
*PCI Tanzania imechangia:
(i) Ujenzi wa Matundu 6 ya choo
(ii) Huduma ya chakula shuleni hapo
*MBUNGE wa Jimbo,  Profesa Sospeter Muhongo ameishachangia:
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Madawati 70
(iii) Vitabu vingi vya Maktaba
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
WAZALIWA wa Kijiji cha Bugunda na Kata ya Bwasi kwa ujumla wake, WANAOMBWA  wachangie MAENDELEO na nyumbani kwao.
UFAULU WA MITIHANI KWENYE S/M BULINGA B
*MATOKEO ya Darasa IV (2020)
Watahiniwa 82
Waliofaulu 70
MATOKEO ya Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 55
Waliofaulu   27
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini