SHULE ZA MSINGI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAANZA KUJENGA MAKTABA

MAKTABA ya S/M RUKUBA

UBORESHAJI WA kiwango cha ELIMU ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini na HALMASHAURI yake UNAENDELEA kwa KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwa SHULE zote za Msingi na Sekondari.
Mbali ya kuwepo MIRADI ya ujenzi wa  VYUMBA VIPYA vya MADARASA kwenye SHULE za MSINGI za SERIKALI (jumla: 111 za Msingi & 11 Shikizi), UJENZI WA MAKTABA UMEANZA kutiliwa mkazo.
MAKTABA MPYA KWENYE SHULE ZA MSINGI
S/M RUKUBA ya Kisiwani Rukuba ndiyo ya kwanza kujengwa na kuanza kutumiwa. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo,  ameweka VITABU VINGI vya kutumiwa na WANAFUNZI, WALIMU, WAKAZI na WAGENI wa hapo Kisiwani.
WANANCHI wa Kisiwani Rukuba na baadhi ya WADAU wao wa Maendeleo WALICHANGIA ujenzi wa MAKTABA hiyo. Mbunge wa Jimbo alichangia MABATI 57 ya kuezekea Jengo la MAKTABA hiyo.
MAKTABA MPYA ZINAZOJENGWA
MAKTABA za S/M BURAGA (Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi) na S/M BUIRA (Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi) zinajengwa kwa kutumia MICHANGO ya  WANAVIJIJI wenyewe. MICHANGO ya kukamilisha MIRADI hii ya ujenzi inakaribishwa.
BAADHI ya SHULE ZA MSINGI za Jimboni mwetu, k.m. S/M BUSEKELA na S/M RUSOLI zimetumia MAJENGO yaliyopo Shuleni mwao kutengeneza MAKTABA za SHULE zao. Mbunge wa Jimbo amegawa VITABU VINGI vya MAKTABA kwa SHULE ZOTE za Msingi na Sekondari za Jimbo la Musoma Vijijini.
MATOKEO MAZURI yaanza kuonekana ambapo MWAKA JANA (2019) HALMASHAURI ya WILAYA ya MUSOMA (Musoma DC) yenye JIMBO la Musoma Vijijini ILIKUWA YA KWANZA MKOANI MARA kwenye Mitihani ya Darasa la Nne (IV).
KARIBUNI TUJENGE MAKTABA KWENYE SHULE ZETU