WANAVIJIJI WAITIKIA MWITO WA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI

Ujenzi wa chumba kimoja cha Darasa (Form I) cha Rusoli Secondary School kitakachokamilishwa kabla ya tarehe 15 Februari 2020.

Jumatano, 29.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Veredian Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SEKONDARI zote za  Jimboni zenye UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa ZITATATUA tatatizo hilo kabla ya tarehe 30 Machi 2020. Sekondari hizo ni  Bugwema (Vyumba 3), Bulinga (3), Kasoma (3), Nyakatende (2) na Rusoli (1).
Kwa sasa Jimbo letu lina Sekondari 20 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi. Kata pekee (IFULIFU) isiyokuwa na Sekondari yake, kwa sasa inajenga SEKONDARI 2 (zinajengwa kwenye Vijiji vya Nyasaungu na Kabegi).
RUSOLI SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Rusoli (Vijiji 3 – Buanga, Kwikerege na Rusoli) ilianzishwa Mwaka 2010 ina Jumla ya Wanafunzi 422 na Walimu 13 akiwemo H/M Mwalimu Tatu Juma.
Jumla ya WANAFUNZI 132 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza hapo Rusoli Sekondari. Mwalimu Mkuu huyo amesema hadi leo, WANAFUNZI 113 wameripoti Shuleni na 2 wamehama.
UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU NA UPATIKANAJI WAKE
* WANAFUNZI 132 wa Form I wanahitaji Vyumba 3 vya Madarasa. Vipo 2 na kimoja kinajengwa na kitakamilishwa kabla ya tarehe 15 Februari 2020.
VIFAA VYA UJENZI wa Chumba kimoja hicho vimetolewa na WAZALIWA wa Kata ya Rusoli ambao ni: (1) Profesa Lawrence Mseru (2) Ndugu William Makunja (3) Belias Mkama na (4) Ndugu Laitoni Samamba. Vilevile, (5) Kanisa la Wasabato Rusoli nalo limechangia
Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 50 ya kupigia lipu Jengo hilo.
UPANUAJI WA VYOO VYA WANAFUNZI
*Wazazi WAMEKUBALI kuongeza Matundu ya Vyoo vya Wasichana kufikia 10 (toka manne) na Wavulana kufikia 10 (toka manne). Kazi hii itakamilika kabla ya tarehe 30 Mai 2020.
Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeula na VIONGOZI wengine wa Kata na Vijiji wanaendelea kuwashawishi na kuwahimiza WANANCHI washiriki ipasavyo kwenye ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Rusoli Sekondari.
MICHANGO YA WAZALIWA WA KATA YA RUSOLI
Kikundi cha WAZALIWA wa Kata ya Rusoli kijulikanajo kwa jina la “YEBHE CHIKOMESHE” kimetoa MICHANGO MIKUBWA kwa ustwai wa ELIMU na MAENDELEO ndani ya Kata hiyo. Kimechangia KISIMA CHA MAJI kwa Shule za Sekondari na Msingi, Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (two in one), Uboreshaji wa Maabara, Computer, Printer, Photocopier, Projector, n.k.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alishachangia SARUJI MIFUKO 70 kwa ajili ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Rusoli Sekondari. Vilevile, Mbunge huyo amewapatia VITABU vingi vya Maktaba yao.