SEKONDARI MPYA ZAONYESHA UBORA WA MIUNDOMBINU YA ELIMU VIJIJINI MWETU

Wanafunzi wa Form I wa Busambara Secondary School wakiwa ndani ya moja kati ya Vyumba vyao vya Madarasa.

Ijumaa, 24.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Hatimae USHIRIKIANO kati ya WANANCHI  na SERIKALI wazaa MATUNDA MAZURI kwenye Sekta ya Elimu – Sekondari Mpya za VIWANGO vizuri ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Tarehe 14 Januari 2020, WANAFUNZI wa Kidato cha kwanza wa  BUSAMBARA SEKONDARY SCHOOL walianza MASOMO yao.
BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL imejengwa kwa USHIRIKIANO wa:
* Wanavijiji wa Vijiji 3 vya Kata ya Busambara ambavyo ni Kwikuba, Maneke na Mwiringo. Hawa walichangia NGUVUKAZI na FEDHA.
* Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. Hawa walichangia FEDHA na USHAURI
* Wazaliwa wa Kata ya Busambara. Baadhi yao walichangia FEDHA na USHAURI. Majina yataandikwa kwenye ubao na kutunzwa shuleni hapo.
*Serikali ikiwemo  Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. MICHANGO hapa ni FEDHA, USHAURI na UONGOZI chini ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma (Dr Vicent Naano Anney) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu (Ndg John Lipesi Kayumbo). HONGERENI sana Viongozi wetu.
*Mtendaji Kata ya Busambara, Ndugu Victor Kasyupa na TIMU yake ya Watendaji wa Vijiji na Afisa Elimu Kata WANASTAHILI PONGEZI kwa kazi kubwa yenye UBUNIFU na UTELEKEZAJI wa uhakika.
MICHANGO YA MADAWATI
* Benki ya NMB inapewa SHUKRANI NYINGI za dhati kwa KUCHANGIA Madawati 80 na Viti 80. AHSANTENI SANA.
HAKUNA MISANGAMANO MADARASANI
*Wanafunzi 142 wa Form I wanatumia VYUMBA 3 vya MADARASA. Kila mmoja analo DAWATI lake na KITI chake.
OFISI 2 ZA WALIMU
* Kwa sasa wapo WALIMU 6, yaani Headmaster na Walimu wake 5. Ofisi 2 zenye meza, viti na kabati zinawatosha.
WALIMU WA KUJITOLEA
* Wazaliwa wa Kata ya Busambara WAMEJITOLEA kuchangia POSHO za Walimu wa KUJITOLEA. Ndugu zetu hawa, Ndugu Joseph Chikongoye, Saidi Chiguma na Robert Cheumbe wanapewa PONGEZI NYINGI na SHUKRANI za dhati.
VYOO VYA WANAFUNZI
* Mashimo 8 ya Wasichana, 6 ya Wavulana na 2 ya Walimu yanatosha kwa idadi ya sasa ya Wanafunzi na Walimu.
UJENZI WA VIWANGO BORA UNAENDELEA
* Ujenzi wa Maabara, Madarasa mengine, Maktaba, Nyumba za Walimu na Viwanja vya Michezo UNAENDELEA.
KUJIPONGEZA NA KUENDELEA NA UJENZI KWA ARI MPYA
*Jumamosi, tarehe 29 Februari 2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na WAZALIWA wa Kata ya Busambara WATAFANYA TAFRIJA Shuleni hapo (Busambara Secondary School) ya KUWAPONGEZA WANAVIJIJI wa Kata ya Busambara kwa hatua hiyo waliyoifikia kwenye ujenzi wa Sekondari yao ya Kata – hawakuwa nayo!
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 kwa sasa (Jan 2020) lina Sekondari 20 za Kata/Serikali, 2 za Binafsi (SDA & KATOLIKI)  na zinajengwa 9 mpya.