PROF MUHONGO AWEZESHA UWEKAJI WA UMEME KWENYE JENGO LA CCM LA WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI

MAFUNDI wa TANESCO wakiweka UMEME kwenye Jengo (Ukumbi na Vyumba 4) la CCM Kijijini Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.

Jumatano, 22.1.2020
CCM Wilaya ya Musoma Vijijini
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameombwa na Chama (CCM) na kukubali kugharamia uwekaji wa UMEME kwenye Jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) lililopo Kijijini Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.
JENGO hilo lina Ukumbi na Vyumba 4.
TANESCO wamekamilisha ZOEZI LA KUWEKA umeme ndani ya SIKU 2 tu! TANESCO Mkoa (Mara) wanapongezwa kwa KAZI NZURI waliyoifanya na kwa muda mfupi sana!
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge, Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Steven Koyo ametoa shukrani zake za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa kukubali ombi la Chama la kuweka umeme katika Jengo la CCM ambalo litaanza kutumika rasmi wiki ijayo kama OFISI YA MUDA ya CCM Wilaya  ya Musoma Vijijini wakati Chama (CCM)  kikiwa kinajenga JENGO LAKE LA KUDUMU Kijijini Murangi. Ujenzi unaanza Mwezi ujao (Februari 2020).
Wanachama wa CCM na rafiki zao wanakaribishwa KUCHANGIA UJENZI wa Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini KIJIJINI MURANGI – KARIBUNI.