SEMINA ELEKEZI NA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA YA TSH 116.5 MILIONI VYATOLEWA KWENYE HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA (MUSOMA DC)

Jumatatu, tarehe 2.12.2019 HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA yenye Jimbo la Musoma Vijijini ILITOA SEMINA ELEKEZI kwa WENYEVITI WAPYA wa Vijiji juu ya UENDESHAJI WA SERIKALI ZA VIJIJI.
SEMINA hiyo imehudhuriwa na Wenyeviti 64 kati ya 68 (Mahudhurio 94.12%, Wenyeviti 4 wameomba udhuru).
Baadhi ya masuala muhimu yaliyotolewa MAFUNZO ni juu ya: Sheria ya Serikali za Mitaa, Muundo wa Serikali (Halmashauri) ya  Kijiji, Kamati za Halmashauri ya Kijiji na Majukumu yake, Vikao/Mikutano (Wajumbe wake na Kazi zake), Utungaji wa Sheria ndogo ndogo za Kijiji, Vyanzo vya Mapato, Majukumu ya Mwenyekiti, Taratibu za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Halmashauri wa Kijiji, n.k. Fursa iliyotolewa ya KUULIZA MASWALI.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika ALIKARIBISHWA kutoa salamu za CHAMA kwa WENYEVITI hao. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
SEMINA ELEKEZI kwa WENYEVITI wa VITONGOJI 374 wa Halmashauri hii itatolewa siku chache zijazo.
TSH 116.5 MILIONI – MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WATU WENYE ELEMAVU, VIJANA NA WANAWAKE
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma chini UONGOZI WENYE UBUNIFU MKUBWA wa Mkurugenzi Mtendaji (DED), Ndugu John Kayombo, leo (2.12.2019) IMETOA MIKOPO YA TSH MILIONI 116.5 kwa Makundi hayo matatu.
IKUMBUKWE kwamba hii ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA wa 2019/2020 na tayari HALMASHAURI hii INATEKELEZA KWA VITENDO UTOAJI wa MIKOPO kama ilivyoagizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.
*MIKOPO KWA WATU WENYE ULEMAVU
Vikundi 3 vyenye Jumla ya Wanachama 45 vimepewa Jumla ya  Tsh Milioni 15. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Bukima, Murangi na Nyambono.
*MIKOPO KWA VIKUNDI VYA VIJANA
Vikundi 4 vyenye Jumla ya Wanachama 78 vimepewa Jumla ya Tsh Milioni 21. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Lyasembe, Maneke, Kataryo na Kisiwa cha Rukuba.
*MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANANAWAKE
Vikundi 16 vyenye Jumla ya Wanachama 285 vimepewa Jumla ya Tsh Milioni 80.5. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Murangi (3), Tegeruka (2), Kwikuba (2), Bukima (1), Bujaga (1),  Saragana (1), Kwibara (1), Kataryo (1), Bwai Kwitururu (1), Busungu (1), Mayani (1) na Kome (1). MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
Utoaji wa MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA ni endelevu. Vipo VIKUNDI vilivyopewa Mikopo Mwaka wa Fedha wa 2018/2019 na vingine BADO VITAPEWA mikopo ndani ya Mwaka huu wa Fedha (2019/2020)
WENYEVITI wa Serikali ya Vijiji, VIKUNDI vilivyopokea MIKOPO isiyokuwa na RIBA, na VIONGOZI mbalimbali Waliohudhuria shughuli hizi mbili WAMETOA SHUKRANi nyingi za dhati kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuki na Viongozi wengine wa Chama na Serikali kwa kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenye Utekelezaji wenye MAFANIKIO MAKUBWA wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) ndani ya Jimbo lao.