WANAVIJIJI WAPATA MATUMAINI MAKUBWA YA KUANZA KUTUMIA MAJI YA BOMBA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijinini, Prof Sospeter Muhongo akiongea na WANANCHI wa Vijiji 3 (Tegeruka, Mayani na Kataryo) vya Kata ya Tegeruka. Hiyo ilikuwa siku ya Jumapili, 11.6.2023 wakati Mbunge huyo alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo.

Kata nne (4) zenye jumla ya Vijiji 12, za Jimbo la Musoma Vijijini, zina miradi ya kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Mradi wa Bomba Kuu la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Gharama za Mradi: Tsh bilioni 70.5
*Uwezo wa uzalishaji: Lita milioni 35 kwa siku
*Mitambo ya kusukuma maji inayotengenezwa China, Hungary na Turkey italetwa nchini hivi karibuni

Ujenzi wa Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka Bomba Kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama

Kata za Tegeruka na Mugango
*Gharama za Mradi: Tsh bilioni 4.75
*Ujenzi umeanza tokea wiki iliyopita na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alienda kukagua ujenzi huo

*Mitaro ya urefu wa takriban km 15 tayari imechimbwa na bomba zitaanza kutandazwa hivi karibuni

*Tenki lenye ujazo wa LITA 135,000 linajengwa Kijijini Kataryo. Hili tenki litapokea maji kutoka kwenye Tenki la Kijijini Kiabakari lenye ujazo wa LITA MILIONI 3

Kata za Busambara na Kiriba
*Tenki la ujazo wa LITA 500,000 limejengwa kwenye Mlima wa Kong'u, Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango

*Vijiji 6 vya Kata za Busambara na Kiriba vitapata maji ya bomba kutoka kwenye Tenki hili.

*Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata hizi mbili itaanza kujengwa, hivi karibuni, August 2023

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba vijijini mwetu. Kila kijiji kinao mradi wa maji! Ahsante sana!

PICHA
Picha hapo juu  inamuonesha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijinini, Prof Sospeter Muhongo akiongea na WANANCHI wa Vijiji 3 (Tegeruka, Mayani na Kataryo) vya Kata ya Tegeruka. Hiyo ilikuwa siku ya Jumapili, 11.6.2023 wakati Mbunge huyo alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 14.6.2023