KIJIJI CHA NYASAUNGU CHADHAMIRIA KUFUNGUA SEKONDARI YAKE JANUARI 2024

Kikao cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifuli, Musoma Vijijini.

Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ametembelea Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

Miradi inayotekelezwa Kijijini hapo ni ya:
*Ujenzi wa Sekondari
*Ujenzi wa Zahanati
*Uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule yao ya msingi (S/M Nyasaungu)

Kero zilizotolewa na kupata majibu kutoka kwa Mbunge huyo ni kuhusu upungufu mkubwa kwenye upatikanaji wa:
*maji
*umeme
*chakula (ukame)
*walimu wa S/M Nyasaungu

*Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari
Kata ya Ifulifu haikuwa na Sekondari yake, na inashukuru Serikali kuchangia kwa kiasi kikubwa sana ujenzi wa Sekondari ya Kata (Ifulifu Sekondari), Kijijini Kabegi.

Kijiji cha Nyasaungu ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu. Kijiji hiki kiko pembezoni na mbali na vijiji vingine vya Kata hii. Vilevile, jiografia yake (mito, vichaka, n.k.) inakifanya kuwa na ugumu wa kufikika, hasa wakati wa mvua - mazingira haya ni hatarishi kwa wanafunzi!

Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari umeanza kwa kutumia michango ya:
*Wanakijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Mfuko wa Jimbo

Halmashauri inaombwa ianze kuchangia ujenzi wa Sekondari hii ambayo watumiaji wake wengi watakuwa watoto wa wafugaji wa Kijiji cha Nyasaungu.

Nyasaungu Sekondari kufunguliwa Januari 2024
Ujenzi umefikia hatua ya kukamilisha:
*Vyumba 3 vya Madarasa
*Choo cha Matundu 6
*Jengo la Utawala

Michango ya Mbunge wa Jimbo
Mbunge wa Jimbo ataendelea kuchangia ujenzi huu kama alivyofanya hapo awali.

Wanakijiji wameamua kuendelea na ujenzi wa Sekondari yao kuanzia tarehe 10.6.2023. Wakianza ujenzi tarehe hiyo Mbunge huyo atawachangia saruji na mabati.

Kwa sasa, Jimbo letu linajenga Sekondari nne (4) mpya, ambazo ni:
*Nyasaungu Sekondari
(Kata ya Ifulifu, sekondari ya pili ya Kata)
*Muhoji Sekondari
(Kata ya Bugwema, sekondari ya pili ya Kata)
*Wanyere Sekondari
(Kata ya Suguti, sekondari ya pili ya Kata)
*Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
(Kata ya Etaro, sekondari ya pili ya Kata)

Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374, lina jumla ya Sekondari 27 (25 za Kata, na 2 za binafsi)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 30.5.2023