SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1942 YAPATA MCHANGO WA SERIKALI WA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Ujenzi wa Vyumba Vipya viwili vya Madarasa na Ofisi moja ya Walimu unaoendelea kwenye S/M BULINGA ya Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi. 

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIJIJI cha BUGUNDA kilichoko Kata ya Bwasi kina SHULE MBILI za MSINGI – S/M Bulinga na S/M Bulinga B
MWALIMU MKUU wa S/M Bulinga, Mwl Alexander Materu ameeleza yafuatayo kuhusu Shule hiyo:
*Ilifunguliwa Mwaka 1942 na kwa sasa ina jumla ya Wanafunzi 662
*Idadi ya Walimu wanaohitajika ni 15, waliopo ni 7
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 14, vilivyopo ni 6
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa sana, kwa mfano, Wanafunzi 147 wa Darasa la III wanatumia chumba kimoja cha darasa.
*Jumla ya WANAFUNZI 214 wanasomea nje, chini ya miti.
MCHANGO WA SERIKALI WA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA
*SERIKALI kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa SHILINGI MILIONI 40 kwa ajili ya kukamilisha Vyumba vipya viwili vya  Madarasa, Ofisi 1 ya Walimu na ununuzi wa Madawati.
MICHANGO YA WANAKIJIJI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA YA SHULE YAO
*MTENDAJI KATA, Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAKIJIJI  wanashiriki katika ujenzi huo kwa kufanya yafuatayo:
 (i) kuchimba Msingi wa Vyumba vipya  2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
(ii) kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHATOLEWA KWENYE S/M BULINGA
*PCI Tanzania ilijenga Matundu 8 ya Choo cha Wanafunzi
*MBUNGE wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo ameshachangia:
(i) Madawati 46
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO
(iii) Mabati 54
*Halmashauri yetu ilishachangia Shilingi Milioni 5.
UFAULU WA MITIHANI WA S/M BULINGA
*MATOKEO Darasa la IV (2020)
Watahiniwa 85
Waliofaulu  85
*MATOKEO Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 32
Waliofaulu  31
SHUKRANI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
*Wanakijiji na Viongozi wao wanaishukuru sana SERIKALI kwa MCHANGO wake wa SHILINGI MILIONI 40.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
*WAZALIWA wa Kijiji cha Bugunda na Kata ya Bwasi kwa ujumla wake, na WADAU wengine wa MAENDELEO wanaombwa wachangie ujenzi wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya SHULE KONGWE (S/M Bulinga) iliyofunguliwa Mwaka 1942.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini