SEKONDARI YA ISHIRINI NA MBILI (22) YAFUNGULIWA MUSOMA VIJIJINI

WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA wa Seka Sekondari  wakijisomea Madarasani mwao, SEKA SEKONDARI ambayo ni MPYA na imefunguliwa tarehe 5.7.2021. Hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira.

Tarehe 25.7.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374, linaendelea na utaratibu wake wa kutatua MATATIZO ya MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
Vilevile, Jimbo hili linaendelea kutatua tatizo la UMBALI MREFU wanaotembea Wanafunzi kwenda masomoni mbali na wanakoishi.
IDADI YA SEKONDARI ZA MUSOMA VIJIJINI
*22 za Kata/Serikali, ikiwemo MPYA (Seka Sekondari) iliyofunguliwa tarehe 5.7.2021
*2 za Binafsi
*10 zinazojengwa au nyingine ujenzi utaanza hivi karibuni
KATA ISIYOKUWA NA SEKONDARI
Kata ya IFULIFU ndiyo Kata pekee isiyokuwa na Sekondari yake.
Kata hiyo imeamua kujenga SEKONDARI 2 kwa wakati mmoja kwa utaratibu huu:
(i) Kijiji cha Nyasaungu kimeamua kujenga SEKONDARI ya Kijiji chake.
(ii) Vijiji vya Kabegi na Kiemba navyo vinajengwa SEKONDARI ya Vijiji vyao viwili.
SEKONDARI YA 22 YAFUNGULIWA JIMBONI MWETU
Kata ya  NYAMRANDIRIRA yenye Vijiji 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na  Seka) ilikuwa na SEKONDARI MOJA tu (Kasoma Sekondari) kwa Wanafunzi wa kutoka Vijiji vyote vitano.
SEKONDARI ya PILI ya Kata hiyo (Seka Sekondari) imefunguliwa tarehe 5.7.2021 ikiwa na WANAFUNZI 113 wa Kidato cha Kwanza na Walimu 7.
SEKONDARI MPYA YA KATA
(Seka Sekondari)
WANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza wa Kata ya Nyamrandirira kwa sasa wako kwenye SEKONDARI MBILI za Kata yao, yaani, wapo wanaosoma Kasoma Sekondari na wengine wanasoma Seka Sekondari.
Kwa hiyo, MATATIZO ya MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani yaliyoko Kasoma Sekondari yameanza kutatuliwa.
Vilevile, WANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza wa kutoka Vijiji vya Chumwi, Mikuyu na Seka wamepunguza UMBALI wa kutembea kwenda masomoni.
MICHANGO YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA SEKA
(i) WANAVIJIJI:
Wanachangia FEDHA TASLIMU kwa mpangilio huu:
*Kijiji cha Kaboni –  kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
*Kijiji cha Seka – kila Kaya inachangia kati ya Tsh 15,000/= na 20,000/=
*Kijiji cha Kasoma – kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
*Kijiji cha Chumwi – kila Kaya inachangia Tsh 6,500/=
*Kijiji cha Mikuyu – kila Kaya inachangia Tsh 20,000/=
*NGUVUKAZI za Wanavijiji wa Vijiji vyote 5 – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
(ii) MADIWANI 2 wa Kata: Mhe Mwl Nyeoja Wanjara na Mhe Mwl Nyachiro Makweba (Viti Maalum) wamechangia jumla ya Tsh 515,000/=
(iii) MGODI wa MMG uliopo Kijijini Seka umechangia:
*Tsh Milioni 8
*Mawe tripu 20
*Molamu tripu 50
*Mchanga tripu 10
*Utengenezaji wa barabara iendayo Seka Sekondari
(iv) WAZALIWA 22 wa Kata ya Nyamrandirira wamechangia jumla ya Tsh 1,930,000/=
(v) MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo,
amechangia:
SARUJI MIFUKO 250
*MFUKO wa JIMBO umechangia:
SARUJI MIFUKO 450
(vi) HALMASHAURI yetu imechangia:
*Saruji Mifuko 50
*Tsh Milioni 5
(vii) DEO Sekondari, Mwl Majidu Kalugendo amechangia Tsh 60,000/=
SEKA SEKONDARI imefunguliwa ikiwa na miundombinu hii:
*Vyumba 3 – Vyumba 2 ni vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu.
*Matundu 12 ya Vyoo vya Wanafunzi
*Matundu 2 ya Choo cha Walimu
MKUU wa SEKA SEKONDARI, Mwl Isaac Jonathan na VIONGOZI wa Kata na Vijiji vyake vitano, WANAWAOMBA sana WAZALIWA wa VIJIJI vyote 5 vya Kata yao ya NYAMRANDIRIRA, na WADAU wengine wa Maendeleo, waendelee KUJITOKEZA KUCHANGIA UJENZI wa Sekondari hii mpya.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini