Mwigombe Technical Secondary School
Jimbo la Musoma Vijijini:
Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
Idadi ya Sekondari:
+Sekondari 30 za Kata
+Sekondari 2 za Binafsi (Katoliki & SDA)
+High Schools 3 (Kasoma, Suguti & Mugango)
Idadi za Sekondari za Ufundi:
+Nyamrandirira Sekondari ya Amali (mpya)
+Mwigombe Tech Sec School (inajengwa na wanakijiji)
Ujenzi wa Sekondari ya Ufundi:
Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba chenye Vitongoji sita (6) wamewashawishi wakazi wa kijijini kwao kujenga sekondari ya ufundi itakayoitwa, "Mwigombe Technical Secondary School."
Michango ya ujenzi imeanza kutolewa na:
+Wakazi wa Kijiji cha Kiriba
+Wazaliwa wa Kijiji cha Kiriba
+Mbunge wa Jimbo
+Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki za NMB na CRDB
Usimamiaji wa ujenzi:
Kamati ya ujenzi inayoongozwa na Ndugu Machupa Lyamena inasimamia ujenzi.
Ujenzi ulipofikia:
Boma moja lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katikati limekamilika. Upauaji utakamilika kabla ya tarehe 30.4.2026
Mchango wa Familia Mashenene:
Wanafamilia Mashenene wameamua kujenga chumba kimoja cha darasa ikiwa ni mchango wa familia hiyo kwenye ujenzi wa sekondari hii. Familia Mashenene inaanza kupau chumba chao cha darasa wiki ijayo.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa kwenye eneo la ujenzi wa "Mwigombe Technical Secondary School" kijijini Kiriba. Hiyo ilikuwa jana, Alhamisi, 18.3.2026
SHUKRANI:
Wananchi wa Kijiji cha Kiriba wanatoa shukrani nyingi sana kwa benki za NMB na CRDB kwa kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa sekondari ya ufundi ya kijijini mwao.
Sekondari hii ikikamilika itakaribisha vijana wa kutoka vijiji vingine vya Jimboni mwetu kuchukua elimu ya ufundi itakayotolewa hapo.
Ombi: Wanakijiji wa Kiriba wanakuomba mchango wako uchangie ujenzi wa sekondari hii. Michango ipelekwe kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kiriba:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300894
Jina: Serikali ya Kijiji Kiriba
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Date: Fri, 19 March 2026