MKOA WA MARA: TUMERUDI MKIANI KITAIFA, YAANI MKOA WA MWISHO!

Vikao vya pamoja vilivyokwishafanyika vya kutoa mapendekezo ya uboreshaji wa elimu Mkoani Mara:

1. Tarehe 22 Feb 2020, Songe Girls High School, Musoma
Miaka ya nyuma, kabla ya tarehe hiyo, Mkoa wa Mara ulikuwa na matokeo mabaya ya mitihani kwenye shule zetu za Msingi na Sekondari!

Niliwashawishi RC Mara , Ndg Adam Malima na DC Musoma, Dr Vicent Naano Anney, tufanye "intervention" kwa kujadili matatizo yanayotukabiri (Mkoa wa Mara) kwenye Sekta ya Elimu na kupata suluhisho stahiki.

Tarehe 22.2.2020, Mkutano wenye wawakilishi kutoka kila Wilaya (na kila Halmashauri) ulifanyika Songe Girls High School ya Musoma Mjini. Mhe Stephen Wassira alisafiri kutoka Dar es Salaam kuhudhuria mkutano huo.

Ufadhili: 95% (S Muhongo)

SFNA 2020: Matokeo ya Darasa la 4 ya Mwaka 2020 ya Musoma Vijijini - ufaulu wa 98.04%, wa kwanza Mkoani Mara!

Mafanikio: Mkoa wa Mara ukatoka mkiani:

2. Tarehe 21 Agosti 2021
Nilifanya kikao na Wakuu wa Shule za Sekondari za Jimboni/Halmashauri yetu kujadili na kutoa mapendekezo ya uboreshaji wa kufundisha na kujifunza kwenye sekondari zetu

Ufadhili: 100% (S Muhongo)

3. Tarehe 25-27 March 2025
Matokeo ya mitihani ya shule za Jimbo/ Halmashauri yetu yakarudi kuwa mabaya, kama yalivyokuwa miaka ya nyuma.

Nikaamua kutafuta suluhisho la tatizo hili kwa kukaribisha wasomi 2 kutoka UDSM waje Jimboni/Halmashauri yetu kufanya udadisi wa kitaalamu na kutoa mapendekezo yenye kutatua tatizo hili la matokeo mabaya ya mitahani kwenye shule zetu.

Wataalamu: Dr Zablon Kengera na Dr George Kahangwa kutoka UDSM, na Mr. Japhet, "Jeff" Makongo kutoka Ubunifu Associates Ltd waliendesha semina iliyojumuhisha viongozi mbalimbali wa Halmashauri yetu, wakiwemo Madiwani wetu

Ufadhili: 98% (S Muhongo)

Mafanikio: mapendekezo yametekelezwa kwa asilimia ndogo sana (<10%) Mapendekezo hayo yameambatanishwa hapa

Tufanyeje:?

Ninamshauri RC Mara, Mhe Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi kufanya kikao na wataalamu wa UDSM waliotoa mapendekezo ya uboreshaji wa kufundisha na kujifunza kwenye shule za Jimboni/Halmashauri yetu.....yatokanayo na kikao hicho yapelekwe kwa wahusika wa Mkoani mwetu kabla ya kuitisha vikao vya kujadili utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa, yakiwemo yale ya huko nyuma!

Mapendekezo yaliyotajwa hapo juu:
Yaliwekwa wazi mitandaoni, na yametunzwa kwenye Ofisi za Elimu za Mkoa wetu na Halmashauri zake.

Ni aibu kubwa: Mkoa wa Mara tumekuwa wa mwisho tena - untold vicious circle of poor performance!

Sospeter Muhongo
6 Nov 2026