
Hayati Prof David Massamba, Gwiji la Lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa, ameenziwa kwa kujenga, "David Massamba Memorial Secondary School" kijijini kwao Kurwaki mahali alipopumzishwa penye utulivu wa milele (Amen)
Wanakijiji wa Kurwaki wakishirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, walianza ujenzi wa sekondari hiyo. Baadae, Serikali ilitoa mchango mkubwa wa Tsh milioni 584, na tayari sekondari imefunguliwa.
Hii ni sekondari ya pili ya Kata ya Mugango yenye vijiji vitatu.
DC Mhe Juma Chikoka:
Mgeni Rasmi wa sherehe za ufunguzi wa, "David Massamba Memorial Secondary School" ya Kijijini Kurwaki alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe Juma Chikoka
Shukrani kutoka Kijijini Kurwaki:
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa yenye shukrani tele kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Msemaji wa mwisho kwenye CLIP/VIDEO hiyo ni DC Mhe Juma Chikoka
Jimbo la Musoma Vijijini limeamua kujenga sekondari moja kwa kila kijiji, kwenye vijiji vyake 68!
Hadi leo hii, Jimbo hili lenye Kata 21, lina jumla ya sekondari 30 za Kata/Serikali na mbili (2) za Madhehebu ya Dini. Ujenzi wa sekondari mpya 12 umeanza na unaendelea vizuri!
Vilevile, uanzishwaji wa "high schools" za masomo ya sayansi unatiliwa mkazo mkubwa sana, mbili zinafunguliwa Julai 2025!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Ijumaa, 14 May 2025