KISIWA CHA RUKUBA KIMEKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Majengo ya Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba, Musoma Vijijini.

Kisiwa cha Rukuba kiko ndani ya Kata ya Etaro yenye vijiji vinne (Busamba, Etaro, Mmahare na Kisiwa cha Rukuba).

Kisiwa hiki cha Musoma Vijijini kina Shule ya Msingi yenye vyumba vya madarasa vya kutosha ikiwepo ziada ya vyumba viwili. Madawati yapo ya kutosha kwa wanafunzi wote. Ofisi mbili (2) za Walimu zipo.

Maktaba ya shule ipo. Kila Mwalimu amepatiwa makazi mazuri. Wana-Rukuba na Mbunge wao wa Jimbo wameanza ujenzi wa Sekondari hapo Kisiwani.

Kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Afya:
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waliamua kupanua Zahanati yao iwe Kituo cha Afya.

*Upanuzi huo ulianza kutekelezwa kwa kutumia michango ya fedha na nguvukazi za wananchi na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.

Tsh Milioni 500 kutoka Serikalini:
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wao wanaishukuru sana Serikali kwa kuwapatia Tsh Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya hapo Kisiwani

*Kituo cha Afya kimekalika na kiko tayari kutumika. Majengo manne (4) na miundombinu yake yaliyokamilika ni:
(i) Mama & Mtoto
(ii) Maabara
(iii) Upasuaji
(iv) Ufuaji

Jengo la OPD litatumika lile la Zahanati wakati Jengo jipya likiwa linakamilishwa.

Ombi la Wafanyakazi & Vifaa Tiba:
Wakazi wa Kisiwani Rukuba wanaiomba Serikali (TAMISEMI & Wizara ya Afya) iwapelekee Wafanyakazi na Vifaa Tiba ili Kituo hicho kianze kutoa huduma za Afya Kisiwani hapo - Wakazi wa hapo Kisiwani wanataka wapunguze sana kusafirisha wagonjwa mahututi na mama wajawazito kwenye mitumbwi kwenda Musoma Mjini kwa matibabu!

SHUKRANI
Wananchi wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wote wa Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani zao za dhati kwa Serikali yetu na kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini mwao.

Tafadhali usiache kutembelea TOVUTI yetu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 8.7.2023