BARABARA KUU PEKEE YA MUSOMA VIJIJINI INAHITAJI KUWEKEWA LAMI: HAIJAPITIKA KIURAHISI KWA ZAIDI SIKU TANO (5)

Eneo la maafa, Kijiji cha Kusenyi, Kitongoji cha Kwikuyu, Musoma Vijijini.

Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)

*Mvua zinazonyeesha wakati huu zinaleta maafa kwa baadhi ya vijiji vilivyoko pembezoni mwa barabara hii.

*Jana usiku na leo asubuhi, Kijiji cha Kusenyi, Kitongoji cha Kwikuyu kimekumbwa na mafuriko makubwa. Wakazi wa hapo wamepoteza mali zao, kikiwemo chakula walichokuwa wamehifadhi majumbani mwao.

*Mkandarasi aliyejenga km 5 kwenye hili barabara la urefu wa km 92 analalamikiwa kwa kuziba vidaraja vidogo vidogo vilivyokuwa vinapitisha maji kwenda ziwani (Ziwa Victoria)

Umuhimu wa barabara ya Musoma-Makojo-Busekera

*Vijiji 68 vya Musoma Vijijini vinaunganishwa na barabara kuu moja tu, ambayo ni hii ya Musoma-Makojo-Busekera

*Barabara hii inaunganisha Musoma Vijijini na Wilaya nyingine za Mkoa wa Mara, na hatimae inaunganisha Musoma Vijijini na Mikoa ya jirani ya Mwanza, Simiyu, Manyara na Arusha

*Barabara hii inaunganisha Musoma Vijijini na Kiwanja cha Ndege cha Musoma Mjini (& Mwanza), na Bandari ya Meli iliyopo Musoma Mjini

Mazao ya uvuvi (dagaa, sangara na sato) yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Mazao ya Kilimo, yaani, mihogo, viazi vitamu, mpunga, mahindi, mtama, matunda, mbogamboga, pamba, alizeti, n.k. yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Dhahabu na madini mengine yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo na Viongozi wengine wa Chama (CCM) na Serikali wanaendelea kuiomba Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi kuipa kipaumbele barabara hili ijengwe kwa kiwango cha lami.

1980 - 2023
Maombi ya Wana Musoma Vijijini na Viongozi wao ya barabara hii kujengwa kwa kiwango cha lami ni tokea Mwaka 1980!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe: Jumatatu, 3.4.2023