KATA YA BUKUMI INAYOJENGA ZAHANATI 3 NA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA YAPEWA SARUJI MIFUKO 200

Jumatano, 3.8.2022 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ametoa SARUJI MIFUKO 200 (mia mbili) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Zahanati 3 na Vyumba vipya 2 vya Madarasa ndani ya Kata ya Bukumi.

Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne (Buira, Bukumi, Buraga na Busekera) ina Zahanati moja tu, ambayo iko kwenye Kijiji cha Buraga, Kitongoji cha Kurugee.

Vijiji vingine vitatu vimeamua kujenga Zahanati zake na ujenzi tayari umeanza kwa kasi ya kuridhisha.

MICHANGO ya WANAVIJIJI ni:

*Nguvukazi
*Fedha taslimu, Tsh 10,000 – 15,000

DIWANI wa Kata, Mhe Munubhi Musa amechangia Tsh 100,000 (laki moja) kwa kila Zahanati. Jumla Tsh 300,000 (laki tatu).

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa kila Zahanati na MIFUKO mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa ya S/M Busekera.

Kwa hiyo, Mbunge huyo amechanga jumla ya SARUJI MIFUKO 200 yenye thamani ya Tsh 4.5 million.

MICHANGO mingine ya Mbunge huyo kwenye Sekta ya Afya ndani ya Kata hiyo ni kama ifuatavyo:

*Gari la Wagonjwa (Ambulance) kwa Zahanati ya Kurugee, Kijijini Buraga

*Saruji Mifuko 100 (mia moja) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bukumi inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kukema Burungu.

HUDUMA ZA AFYA NDANI YA JIMBO LETU:

Jimbo letu lina Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68. Huduma za Afya zinatolewa na:

*Hospitali ya Wilaya ambayo bado inaendelea kujengwa

*Vituo vya Afya: 3

*Zahanati za Serikali: 23
*Zahanati Binafsi: 4

UJENZI UNAOENDELEA:

*Vituo vya Afya: 3

*Zahanati za Vijiji zinazojengwa: 17

OMBI KUTOKA KATA YA BUKUMI

Wana-Kata ya Bukumi na rafiki zetu tunaombwa tujitokeze kuchangia miradi hii ya ujenzi iliyoanzishwa na inatekelezwa kwa nguvukazi na michango ya fedha taslimu kutoka wanavijiji wenyewe.

PICHA za hapa zinaonesha:

*Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wakikabidhi SARUJI MIFUKO 200 kwa Viongozi wa Kata ya Bukumi. Hii ilitokea leo, Jumatano, 3.8.2022, Musoma Mjini.

*BOMA la Zahanati ya Busekera

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 3.8.2022