KAMPENI KABAMBE YA UPANDAJI MICHE YA MITI NA MATUNDA WAANZA MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akigawa MICHE 10,000 kwa Wanafunzi na Wanavijiji wa Jimboni mwetu.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ANASHIRIKIANA na VI Agroforestry Project ya AIC (African Inland Church) kupanda miche ya MITI na MATUNDA vijijini mwetu, zikiwemo shule zetu zote na Madhehebu ya Dini zote. Wakulima binafsi nao wanapewa miche ya miti na matunda.

Miche ya miti na matunda inatolewa bure na iwapo inapaswa kununuliwa (k.m. miche ya mivule), Mbunge huyo anainunua na kuigawa bure.

Jana, Jumatano, 18.5.2022, Mbunge huyo aliambatana na Mtaalamu wa Misitu, Ndugu Jacob Malima wa VI Agroforestry Project KUGAWA MICHE 10,000 (miche elfu kumi) kwenye vijiji vya kando kando mwa Ziwa Victoria (Vijiji vya Kurwaki, Kiriba, Bwai Kumsoma), kikiwepo Kisiwa cha Rukuba (miche 4,500)

MVUA ZA VULI ZA MWEZO OKTOBA

Mipango inawekwa na DC (Dr Haule) na DED (Ndugu Palela) wetu kwenye UPANDAJI mkubwa wa MITI na MATUNDA ndani ya vijiji vyetu 68 ikiwemo Milima yetu (k.m. Nyaberango na Mtiro) ambayo kwa sasa ni vipara vitupu.

Malengo yetu ni kupanda MICHE 100,000 (miche laki moja) wakati wa mvua za vuli za Oktoba 2022.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 19.5.2022