KATA ISIYOKUWA NA SEKONDARI YAKE YAPOKEA SHILINGI 470 MILIONI KWA AJILI WA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA HIYO

Kikao cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, na VIONGOZI wa ujenzi wa Ifulifu Sekondari ya Kata ya Ifulifu. Kikao kilifanyika Kijijini Kabegi, ktk eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata.

Kata ya IFULIFU ya Jimbo la Musoma Vijijini ndiyo KATA PEKEE isiyokuwa na Sekondari yake.
Wanafunzi wa Sekondari wa Kata hii wanasoma Sekondari za Kata jirani za Nyakatende na Mugango.
Kata hii ina VIJIJI 3 vya Kabegi, Kiemba na Nyasaungu.
Kijiji cha Nyasaungu kiko mbali na vijiji vingine na wakazi wake wengi ni wafugaji. Taarifa za ujenzi wa Sekondari ya Kijiji hiki cha Wafugaji ilitolewa jana, Ijumaa, 22.1.2022
*UJENZI WA IFULIFU SEKONDARI*
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba vilianza ujenzi wa Sekondari yao JUNI 2017
*MICHANGO ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:
(i) Wanavijiji – fedha taslimu na nguvukazi
(ii) Mbunge wa Jimbo – fedha zake binafsi
*MAJENGO yaliyokamilishwa kwa nguvu za WANAVIJIJI na MBUNGE wao:
(i) Vyumba viwili vya Madarasa
(ii) Msingi wa Jengo la Utawala umekamilika
(iii) Matofali 1,200 yametengenezwa
*FEDHA ZA UVIKO- 19/IMF ZIMEPOKELEWA*
Kata ya IFULIFU inayojenga Sekondari yake ya Kata tokea JUNI 2017, imepokea kwa shukrani nyingi mno SHILINGI MILIONI 470 kutoka Serikali Kuu.
*Wanavijiji na Viongozi wa Kata ya Ifulifu wanatoa shukrani nyingi sana kwa Mhe Rais wao, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuimbuka Kata yao ambayo haina Sekondari yake, na ujenzi waliouanza unasuasua kwa ukosefu wa fedha. Fedha zimepatikana – KAZI IENDELEE!
Juzi, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alienda Kijijini Kabegi kufuatilia ujenzi wa Ifulifu Sekondari na kujadili na Viongozi wa Kata hiyo kuhusu matumizi bora ya TSH MILIONI 470 walizozipokea kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
*USHAURI ULITOLEWA NA MBUNGE WA JIMBO*
*Vijiji 2 vya Kabegi na Kiemba vifanye VIKAO vya WANAVIJIJI kuwaeleza juu ya malengo ya fedha hizo (Tsh 470m) walizozipokea Katani
*Matumizi ya fedha hizo yawekwe wazi sana kwa wanavijiji
*Wanavijiji waendelee kuchangia nguvukazi ili miundombinu muhimu ya elimu ipatikane kutokana na fedha hizo.
*Ujenzi uende kwa kasi kubwa na kwa ubora unaokubalika
*Ifulifu Sekondari ifunguliwe Julai 2022., na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na kutoka Vijiji vya Kabegi na Kiemba waendelee na masomo yao kwenye Sekondari yao ya Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini