FEDHA ZA UVIKO 19 (IMF): KISIWA CHA RUKUBA CHAKUBALI KUCHANGIA NGUVUKAZI KWENYE UJENZI WA KITUO CHAO CHA AFYA

WAKAZI wa KISIWA cha RUKUBA wakisomba MCHANGA kwa ajili ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya KITUO chao cha AFYA.

KISIWA cha RUKUBA kimepokea SHILINGI MILIONI 250 kwa ajili ya ujenzi wa KITUO cha AFYA Kisiwani humo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa hicho, Ndugu Japhari Ibrahim Kibasa, kwa niaba ya WANA-RUKUBA, anatoa SHUKRANI nyingi sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa KUKIKUMBUKA KISIWA CHAO ambacho sasa kitakuwa na HUDUMA nzuri za Afya.
“Safari za MITUMBWI za mchana na usiku za kupeleka wagonjwa mahututi na wajawazito Musoma Mjini, sasa hazitakuwepo tena, ” amesema Kiongozi huyo.
Kisiwa cha Rukuba ni moja kati ya Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini. Kisiwa hiki kiko Kata ya Etaro.
Leo, Ijumaa, tarehe 7.1.2022, WAKAZI wa Kisiwani humo wameanza kusomba mchanga wa ujenzi wa:
*Jengo la Maabara
*Wodi ya Mama&Mtoto
*Kichomea Taka (incinerator)
KISIWA cha RUKUBA kinang’ara sana kimaendeleo. Ndani ya MIAKA 6, Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha yafuatayo:
(1) SHULE YA MSINGI:
*Vyumba vya Madarasa vipo vya kutosha na ziada ya chumba kimoja
(2) MAKTABA YA SHULE YA MSINGI:
*Wakazi wa Kisiwani humo walishirikiana na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo kujenga MAKTABA na kuweka VITABU vya kutosha.
(3) NYUMBA ZA WALIMU:
*Mdau wa Maendeleo Kisiwani humo alishirikiana na Wakazi wa Kisiwa hicho kujenga nyumba za Walimu. Kila Mwalimu amepewa nyumba ya shule, na ipo moja ya ziada.
(4) UMEMEJUA (solar):
*Mradi umeanza kutekelezwa wa utumiaji wa “solar”. Zahanati inatumia “solar”
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini