SERIKALI YATOA TSH MILIONI 50 KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANAKIJIJI KWENYE UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO

Hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira, Kata ya Nyegina.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 lina Huduma za Afya zifuatazo:
*Hospitali ya Wilaya ya Serikali, ujenzi unaendelea kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
*Vituo Vya Afya 3 vya Serikali vinatoa Huduma za Afya. Vituo hivi ni:
^ Murangi
^ Mugango
^ Bugwema (Ujenzi wa upanuzi wa Zahanati ya Masinono kuwa Kituo cha Afya unakamilishwa)
*Zahanati ya Makojo imepewa fedha (Tsh 250m) na Serikali kupanuliwa iwe Kituo cha Afya, hivyo kitakuwa Kituo cha Afya cha nne (4) Jimboni mwetu.
*Zahanati 23 za Serikali zinatoa Huduma za Afya
*Zahanati za Binafsi zipo 4, nazo pia zinatoa Huduma za Afya.
*Zahanati Mpya 16 zinajengwa na Wanavijiji. Serikali imeanza kuchangia ujenzi wa baadhi ya Zahanati hizi.
UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA
Kijiji cha Mkirira kiko Kata ya Nyegina, inayoundwa na Vijiji 3 (Kurukerege, Mkirira na Nyegina). Kijiji hiki kina jumla ya Wakazi 5,696.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira ulianza Mwaka 2016. Ujenzi huu unaendeshwa kwa kutumia MICHANGO ya WANAKIJIJI, SERIKALI KUU (TAMISEMI), MBUNGE WA JIMBO, na WADAU WENGINE wa MAENDELEO.
WACHANGIAJI WA UJENZI:
WANAKIJIJI:
*Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkirira, Ndugu Sabina Chacha amesema kuwa hadi hapo ujenzi ulipofikia nguvu za WANANCHI ni za thamani ya Tsh. Milioni 16. Hii inajumuisha nguvu kazi za kusomba maji, mchanga, mawe, kokoto na michango ya fedha taslimu.
Wanakijiji walikubaliana kuchangia Tsh. 15,850/= kwa kila mkazi wa Kijijini hapo na mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
SERIKALI KUU:
*Serikali Kuu (TAMISEMI) imechangia Tsh. Milioni 50. Hii ni kwa ajili ya ukamilishaji (finishing) wa Zahanati hii ya Mkirira. SHUKRANI NYINGI SANA kwa SERIKALI yetu.
MBUNGE WA JIMBO:
*Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechangia  SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa Zahanati hii.
MICHANGO YA WADAU WENGINE  WA MAENDELEO
*Mhe Amina Makilagi
   Saruji Mifuko 180
*Benki ya NMB
   Mabati 180
*Nyanza Road Works Ltd
   (i) Kokoto tripu 6
   (ii) Saruji Mifuko 50
*Mhe Majira Mchele (Diwani wa Kata ya Nyegina) amechangis Tsh 700,000/=
*Kikundi cha WAZALIWA wa Kijiji cha Mkirira wamechangia:
    (i) Kokoto tripu 3
    (ii) Saruji Mifuko 30
    (iii) Nondo 4
MIUNDOMBINU inayojengwa kwenye Zahanati ya Kijiji cha Mkirira ni:
* Opd
* Chumba cha  Daktari
* Maabara
* Wodi la Mama & Mtoto
* Wodi la Wagonjwa wengine
* Chumba cha Wajawazito (leba)
* Chumba cha Uzazi wa Mpango
* Chumba cha dawa
* Chumba cha chanjo
LENGO WALIOJIWEKEA WANAKIJIJI:
*Kwakuwa Wanakijiji wa Kijiji cha Mkirira wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa kilomita 8-10 kwenda kupata Huduma za Afya kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Nyegina, WANAKIJIJI hao wameamua kukamilisha ujenzi wa Zahanati yao ifikapo Novemba 2021. Hayo yameelezwa na Ndugu Paschal Maerere, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini