MUSOMA VIJIJINI IMEDHAMIRIA KUANZA KUWA NA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI KUANZIA MWAKANI (Julai 2022)

Wanafunzi na Walimu wakiwa kwenye MAABARA wakifanya “experiments” kwenye Maabara ya MUGANGO SEKONDARI.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SEKONDARI zote 21 za KATA za Jimbo la Musoma Vijijini zina Miradi ya aina mbalimbali ya ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.
MIRADI hiyo ni pamoja na ujenzi na uboreshaji wa MAABARA za masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry & Biology).
MIRADI mingine ni ya ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa, Maktaba, Mabweni, Vyoo na Nyumba za Walimu.
SHULE 2 za Sekondari za Binafsi, zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki (RC) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA),  nazo zinaboresha Miundombinu yake ya Elimu.
SEKONDARI mpya 12 zinazojengwa au zilizopangwa kujengwa zitakuwa na Miundombinu kama hiyo ya Elimu.
UKAMILISHWAJI WA MAABARA 3 ZA MASOMO YA SAYANSI
Baadhi ya Sekondari zetu tayari zimekamilisha na kutumia Maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia.
SEKONDARI hizo ni:
*Kiriba
*Mugango
*Rusoli
*Bugwema (zinakamilika Sept 2021)
Kwa hiyo, MIPANGO ya ujenzi wa “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya Sayansi utaanza kwenye SEKONDARI 4 zilizotajwa hapo juu kwa kuanza kujenga:
*Vyumba vipya vya Madarasa ya “High School”
*Bweni la Wanafunzi wa “High School”
*Bwalo la Chakula & Jiko lake
MUHIMU:
Michango ya awali kabisa inatolewa na WANANCHI WENYEWE ambao ni Wanavijiji na Viongozi wao, na Wazaliwa wa Vijiji vyenye MIRADI ya ujenzi – “KUJITOLEA”
UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA MUGANGO SEKONDARI
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo imeishatoa taarifa za MAABARA 3 ya Sekondari za Kiriba na Rusoli. Leo inatoa taarifa za MAABARA za Mugango Sekondari
MKUU wa Mugango Sekondari, Mwl Chacha Ragita ameeleza yafuatayo:
*Sekondari ilifunguliwa Mwaka 1999
*ina Wanafunzi 800
*Mahitaji  ya Walimu ni 25, waliopo ni 18
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 20, vilivyopo ni 16
*Mahitaji ya Matundu ya Vyoo ni 34, yaliyopo 24
*Nyumba 18 za Walimu zinahitajika, zilizopo ni 4
MIUNDOMBINU iliyokamilika:
*Maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia zote zipo zinatumika
*Maktaba ipo
*Matundu 2 ya Vyoo vya Walimu yapo.
MICHANGO ya Miradi ya ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Sekondari hii inatolewa na:
*Serikali Kuu
*Wanavijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Wadau wa Maendeleo
*WANAVIJIJI:
na Viongozi wao wa Kata na Vijijini wanachangia fedha taslimu na NGUVUKAZI za kusomba mawe, mchanga, kokoto na maji ya ujenzi.
*SERIKALI KUU:
imetoa michango mingi tokea Mwaka 1999, na hivi karibuni:
(i) TAMISEMI imetoa vifaa vyote vya Maabara zote tatu.
(ii) TAMISEMI imetoa Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana – ujenzi umeanza
*MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amechangia:
(i) Saruji Mifuko 130
(ii) Vitabu zaidi ya 2,000 vya Maktaba
*MRADI wa MAJI (BADEA) umeunganisha Bomba la Maji kwenye Sekondari hii.
*SHIRIKA la Water Aid Tanzania limetoa Matenki 2 ya Maji yenye ujazo wa lita 5,000 kwa kila moja.
UFAULU WA MITIHANI YA KIDATO CHA IV (2020)
*Watahiniwa: 83
Div I – 4    Div II – 5
Div III-14  Div IV – 39
Div 0 – 21
MATOKEO YA KIDATO CHA II (2020)
*Watahiniwa: 175
Div I – 8    Div II – 11
Div III-19  Div IV – 121
Div 0-16
OMBI: WADAU wa MAENDELEO tujitokeze kutoa MICHANGO ya ujenzi wa “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya Sayansi Jimboni mwetu.