WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WAJENGEWA VYUMBA VIPYA 2 VYA MADARASA NA OFISI 1 YA WALIMU

hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa VYUMBA VIPYA vya Madarasa na OFISI ya Walimu kwenye S/M NYAMBONO B yenye Wanafunzi wenye MAHITAJI MAALUM 

Tarehe 3.8.2021
Jimbo la Musoma Vijijiji
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WANAFUNZI wenye Mahitaji Maalumu wanajengewa Vyumba viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu kwenye Shule wanayosoma, S/M NYAMBONO B, Kijijini Saragana.
Kijiji cha Saragana kina Shule 2 za Msingi, ambazo ni S/M Nyambono na S/M Nyambono B. Kijiji hiki ni kimoja kati ya Vijiji 2 (Nyambono & Saragana) vya Kata ya Nyambono.
KAIMU MWALIMU MKUU wa S/M Nyambono B, Mwl Salum Abdalah ameelezea yafuatayo kuhusu Shule hiyo:
*Ilifunguliwa Mwaka 2010 na ina jumla ya Wanafunzi 809.
*Wanafunzi 22 ni wale wenye Mahitaji Maalum (wenye matatizo mbalimbali ya kiafya).
*Shule hii ina Walimu 9, kati ya hao, Walimu wawili  (2) wanafundisha Wanafunzi 22 wenye Mahitaji Maalum.
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 12, vilivyopo 4
*Matundu 32 ya Vyoo yanahitajika, yaliyopo ni 8
*Choo cha Walimu chenye Matundu 2 kipo.
*Zinahitajika nyumba 9 za Walimu, ipo 1 tu.
UFAULU WA MITIHANI WA S/M NYAMBONO B
*DARASA la IV (2020)
Watahiniwa: 89
Waliofaulu: 89
*DARASA la VII (2020)
Watahiniwa: 58
Waliofaulu: 48
WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WAJENGEWA MADARASA
MWALIMU KIONGOZI wa Kitengo cha Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum, MWL ABEID PAUL ameelezea YAFUATAYO kuhusu hali za Wanafunzi hao:
*Wanafunzi wenye ulemavu kwenye ubongo (intellectual impairment) ni 16
*Wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia (hearing impairment) ni 6
MICHANGO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM
SHIRIKA la BMZ la UJERUMANI linatoa MISAADA mingi kwa Wanafunzi hao ikiwemo:
*Vifaa vya Shule mbalimbali, k.m. mabegi, madaftari na kalamu
*Matibabu ya bure, yakiwemo ya upasuaji (operations) kwenye Hospitali Teule ya Shirati.
Ofisi ya Miradi ya SHIRIKA la BMZ ipo Hospitali Teule ya Shirati
*Vifaa Maalum vya (kimatibabu) vinavyohitajika, k.m. baiskeli maalum, miwani, vifaa vya kuongeza usikivu, fimbo maalum za kutembelea na miguu bandia
AHSANTE SANA SANA BMZ (Ujerumani)
WACHANGIAJI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA S/M NYAMBONO B
(i) WANAKIJIJI:
Wanachangia NGUVUKAZI za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
(ii) SERIKALI YA KIJIJI:
Mapato ya ndani (20%) ya Serikali ya Kijiji cha Saragana yanachangia ujenzi huu.
(iii) TASAF:
*Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Madawati 32
*Vifaa vya Shule  (mabegi, madaftari na kalamu)
kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum.
(iv) MBUNGE wa JIMBO:
Prof Sospeter Muhongo amechangia kama ifuatavyo:
*Madawati 75
*Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA SARAGANA
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Saragana, Ndugu Ernest Jama Kamori anawaomba WAZALIWA wa Kijiji cha Saragana, na WADAU wengine wa MAENDELEO wajitokeze KUCHANGIA ujenzi na ukamilishaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule zao za Msingi na Sekondari zilizopo Kijijini hapo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijiji