Taarifa mpya (update):
Bonde la Bugwema, Musoma Vijijini
MRADI WA UMWAGILIAJI WA BUGWEMA KUKABIDHIWA MKANDARASI MWEZI HUU
Tarehe ya tukio:
Jumamosi, 18.4.2026
Muda: Saa 4 asubuhi
Mahali:
Kijijini Bugwema
Kata ya Bugwema
Jina la Mkandarasi:
China Railway Bureau Ltd
Gharama za mradi:
Tsh bilioni 48 (Tshs 48b)
Historia fupi ya Mradi:
Mradi huu ulianzishwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1974.
Tarehe 6.2.2022, Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliombwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini afufue mradi huu - Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akakubali na kuagiza Wizara ya Kilimo itekeleze uamuzi wake. Ahsante sana Mhe Rais, tunashukuru sana sana!
Matayarisho ya Mkandarasi kukabidhiwa mradi yanaendelea na taarifa zaidi zitatolewa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Date: Sat, 4 April 2026