MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA

*Jimbo la Musoma Vijijini:
Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374

*Huduma za Afya Musoma Vijijini

+Hospital ya Halmashauri/Wilaya: 1
+Vituo vya Afya: 7
+Zahanati zinazotoa huduma:
28 za Serikali
2 za Binafsi
+Zahanati mpya zinazojengwa: 11
+Magari ya Wagonjwa (Ambulances): 7

*Kituo cha Afya cha Kata ya Tegeruka:

Kituo hiki cha Afya kinajengwa kijijini Kataryo na kitatumiwa na vijiji vyote vitatu vya Kata ya Tegeruka (Vijiji: Kataryo, Mayani na Tegeruka)

*Ujenzi wa Nyumba ya Daktari:

Mchimbaji Mdogo wa madini, Ndugu Athanace Makorere Motega, mwenye mgodi wa dhahabu kijijini Kataryo amejenga nyumba ya kisasa kwa ajili ya makazi ya Daktari wa Kituo hicho cha Afya - ahsante sana Ndugu Motega!

*Serikali yatoa Tsh milioni 500:

Serikali yetu imetoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Tegeruka

Wanakijiji kwa kushirikiana na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo, walianza kujenga Zahanati ya kijiji cha Kataryo, baadae Serikali ikaamua kujenga Kituo cha Afya kwa ajili ya Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu.

Picha:
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akimpa mkono wa shukrani kubwa Ndugu Athanace Mogeka aliyejenga nyumba ya Daktari wa Kituo cha Afya cha Tegeruka

Majengo ya Kituo cha Afya cha Tegeruka, ujenzi unaendelea

SHUKRANI
Wananchi wa Kata ya Tegeruka na Viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuboresha utoaji wa Huduma za Afya Jimboni mwetu - ahsante sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Date: Mon, 16 March 2026