WAZAZI WA WANAFUNZI WA FORM I WA MUHOJI SEKONDARI WAMEDHAMIRIA SEKONDARI YA KIJIJI CHAO IFUNGULIWE

Wanakijiji wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema wameamua kufanya kwa vitendo:

1. Walianza kujenga sekondari ya kijiji chao wakishirikiana na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo. Baadae, baadhi ya Wazaliwa wa Kijiji hicho nao walichangia ujenzi huo

2. Serikali iliwachangia Tsh milioni 75, bado wakaendelea kujitolea kuchangia nguvukazi zao kwenye ujenzi wa sekondari yao

3. Wameshafisha mazingira ya eneo lote la sekondari ikiwemo kulima barabara ya kuingia shuleni hapo

4. Wamenunua madawati ya watoto wao (Form I) kutoka kwa fundi anayeyatengeneza kijijini (Muhoji) hapo (angalia picha ya hapa)

5. Wazazi wa wanafunzi wa Form I wamekubaliana kuchangia chakula cha mchana cha wanafunzi hao (watoto wao)

6. Wazazi wamekubaliana kuhakikisha kwamba panakuwepo na mahusiano mazuri kati yao (wazazi) na walimu, na kati ya wanafunzi (watoto wao)
na walimu

Kijiji cha Muhoji kinaendelea kutoa somo muhimu kwa Wana-Musoma Vijijini! Hongereni Muhoji!

Muhoji Sekondari ni sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema. Kata hii ina vijiji vinne (4).

Tunakoelekea, Musoma Vijijini, kila kijiji kiwe na sekondari yake, na kila kijiji kiwe na zahanati yake. Tunafanikiwa!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 17 Jan 2025