
Taarifa kutoka REA:
Bajeti ya Mwaka 2023/2024: Mkandarasi wa pili amekamilisha kazi za awali, na sasa anajitayarisha kuanza kusambaza umeme kwenye VITONGOJI 15 - orodha imeambatanishwa hapa
Tusisahau:
Bajeti ya Mwaka 2022/2023: Mkandarasi wa kwanza anaetekeleza Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili "C" anaendelea na usambazaji wa umeme kwenye VITONGOJI 59 - Madiwani wetu walipewe orodha ya vitongoji vyao
Nyongeza ya VITONGOJI 10: REA imekubali ombi letu na taarifa rasmi tutapewa hivi karibuni
Bajeti ya Mwaka 2024/2025:
REA inatayarisha orodha ya vitongoji vitakavyosambaziwa umeme kwa Mwaka huu wa Fedha.
Mwakilishi wa REA Mkoa wa Mara huwa anakaribishwa kwenye Vikao vya Baraza la Madiwani wa Halmashauri yetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 16 Jan 2025