Jimbo la Musoma Vijijini limeamua kuongeza idadi ya "High Schools" hasa za masomo ya sayansi kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu kwa baadhi ya sekondari zake za Kata.

Idadi ya "High Schools" Jimboni mwetu:

(i) Kasoma - masomo ya "arts"
(ii) Suguti - masomo ya sayansi, kuanzia 2025
(iii) Mugango - masomo ya sayansi, kuanzia 2025

Sekondari za Kata zinazojipanga kuanzisha "High Schools" za masomo ya sayansi ni: Mtiro, Makojo, Kiriba, Etaro, Nyakatende na Bugwema

Uanzishwaji wa "Mtiro High School:"

Mtiro Sekondari ni ya Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne - Buira, Bukumi, Buraga na Busekera

Miundombinu muhimu inayohitajika kwenye uanzishwaji wa "high school" ya masomo ya sayansi ni:

(i) maabara 3 za masomo ya sayansi
(physics, chemistry & biology labs)

Mtiro Sekondari inajenga maabara hizo kwa michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kutoka Halmashauri yetu, Mfuko wa Jimbo, Mbunge wa Jimbo, Diwani wa Kata, Wadau wa Maendeleo na baadhi ya wanavijiji wa Kata ya Bukumi

(ii) Bweni la wanafunzi wa "High School"

Mtiro Sekondari imepokea fedha kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa bweni hilo

(iii) Bwalo la chakula & Jiko

Mtiro Sekondari wanajitayarisha kuanza ujenzi huu kwa kupitia Harambee za Mbunge wa Jimbo

(iv) Vyumba vya madarasa na vyoo vya kutosha

Mtiro Sekondari imepokea fedha kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa mindombinu hiyo

(v) Maji ya bomba na umeme

Mtiro Sekondari inavyo vyote hivyo hapo shuleni

OMBI:
Wana-Musoma Vijijini tunakaribishwa kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya uanzishwaji wa "Mtiro High School."

Mawasiliano ya kuchangia:
Headmaster, Mtiro Secondary School
Tel: 0758 487 478

Picha iliyoambatanishwa hapa:
Boma ya maabara ya masomo ya sayansi yanayojengwa Mtiro Sekondari, Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 9 Dec 2024